Je! Mungu ni yule yule?

Unapimaje "intelligence power" ? Computer ikimzidi binadamu "intelligence power" computer hiyo itakuwa binadamu?
Mkuu kitu ulichokitengeneza mwenyewe hakina uwezo wa kukuzidi intelligence maana ni sehemu ya uelewa wako.
Turudi sasa kwenye swali la msingi..mwanzo wa hao wazazi wa kwanza kabla ya sexual reproduction ni nini?
 
Mkuu kitu ulichokiengeneza hakina uwezo wa kukuzidi intelligence maana ni sehemu ya uelewa wako.
Turudi sasa kwenye swali la msingi..mwanzo wa hao wazazi wa kwanza kabla ya sexual reproduction ni nini?
Hujjibu intelligence unaipimaje?

Kuna computer zimewazidi binadamu katika mchezo wa chess.

Stephen Hawkings kaonya kuhusu artificial intelligence kuwa uncontrollable. Utasemaje kitu ulichokitengeneza mwenyewe hakina uwezo wa kukuzidi intelligence kama kina algorithm ya kujifunza haraka kuliko ubongo wako?

Hujajibu wala kujua binadamu ni nani unataka kurudi kwenye swali la mwanzo wa hao wazazi ni nani?

Nikisema sijui, jibu ni lazima liwe mungu?
 
Kwamba mungu amethibitishwa.

Hujajibu swali. Unaweza kuthibitisha mungu yupo?
Kwahiyo wewe kuwepo ama kutokuwepo kwa mungu si suala ambalo litabadili chochote katika mambo unayoyafahamu?
 
Kwanza kabisa.

Binadamu ni nani?

Unamjuaje huyu ni binadamu na huyu si dinadamu?
Umesahau kama umetumia neno "wanadamu" katika maelezo yako hapo mwanzo ajabu tena wewe unakuja kuuliza binadamu ni nani? Ubishi wako ni wa kitoto kweli yani Kiranga.
 
Kwahiyo wewe kuwepo ama kutokuwepo kwa mungu si suala ambalo litabadili chochote katika mambo unayoyafahamu?
Mambo kama yepi? Unaweza kutoa mfano?

Halafu mbona hujibu maswali yangu unataka nikujibu wewe tu?

Unaweza kuthibitisha kwamba mungu yupo?
 
Umesahau kama umetumia neno "wanadamu" katika maelezo yako hapo mwanzo ajabu tena wewe unakuja kuuliza binadamu ni nani? Ubishi wako ni wa kitoto kweli yani Kiranga.
Hapana.

Ni wazi hujawahi kusikia "Socratic method".

Tatizo si kwamba ubishi wangu ni wa kitoto.

Tatizo elimu yako ni ndogo. Ungewahi kusoma hata kitabu kimoja cha Plato usingeshangaa namna ninavyobisha na kuuliza maswali.

Tatizo hujawahi kumsoma Plato, nikikupa inquiry by Socratic method huelewi nafanya nini.
 
Ni kweli nina upungufu mkubwa sana wa kujaza mawazo ya watu kichwani kama ufanyavyo wewe,na ndiyo maana tunabishana hapa maana kama ningekuwa kama wewe basi hata nisingekuwa nabishana na wewe.
Kwahiyo kama hali yangu hii ni udogo wa elimu basi nina elimu ndogo kuliko hata unavyofikiri.
 
Mambo kama yepi? Unaweza kutoa mfano?

Halafu mbona hujibu maswali yangu unataka nikujibu wewe tu?

Unaweza kuthibitisha kwamba mungu yupo?
Mfano watu wenye kuamini kuwa kuna mungu kuna vitu ambavyo huvifahamu kuwa vimeumbwa na mungu kama binadamu,na kuna mambo ambayo huyafahamu kuwa ni katika mipango ya mungu kama kifo.
Kwa hivyo endapo utasema hakuna mungu huelewaji wao wa hayo mambo utakuwa umetatizika,na kwa upande wa wasioamini mungu hali pia itakuwa kama hivyo.
 
Unaweza kutaja kitu kimoja ambacho kitabadilika kwangu?

Dunia ambayo ina mungu wenu huyo ina contradiction. Hiyo ndiyo isiyoeleweka. Kama mungu yupo na amethibitishwa, hizi contradictions mtazielezeaje?

Hao unaosema "watu wenye kuamini mungu" hivyo vitu ulivyovitaja kwamba vimeumbwa na mungu kama binadamu na kifo, ukifuatilia sana utakuta kwamba wanafikiri hivyo kwa sababu ya kukosa uchuinguzi tu.

Mwili wa binadamu una inefficiencies, una produce waste, unaumwa magonjwa etc. Mungu mwenye uwezo wote, upendo wote na ujuzi wote hawezi kuwa kaumba mwili wenye mapungufu kama huu.

Dunia ambayo haina mungu haina mzigo wa kuelezea imperfections, na hivyo haitatizi kuielezea.Kama kuna kitu imperfect, hilo halishangazi, kwani haijaumbwa na a perfect god.

Kinachotatiza Zaidi ni uwepo wa mungu, si kutokuwepo kwa mungu.
 
Una mkakati gani wa kurekebisha hilo?

Mchakato wa kuelimika ni pamoja na kujaza mawazo ya watu na kuchuja ili kubaki na yanayofaa.

Usije kubishana kwa sababu ya kukosa kuelewa mambo bila ya kuwa na mkakati wa kurekebisha tatizo la msingi.
 
Hayo uliyoyaeleza ndivyo unavyoelewa na ndiyo maana nikasema endapo itathibitishwa uwepo wa mungu pengine uelewa wako huo utakuwa tofauti na uelewavyo sasa.
 
Una mkakati gani wa kurekebisha hilo?

Mchakato wa kuelimika ni pamoja na kujaza mawazo ya watu na kuchuja ili kubaki na yanayofaa.

Usije kubishana kwa sababu ya kukosa kuelewa mambo bila ya kuwa na mkakati wa kurekebisha tatizo la msingi.
Sihitaji kumeza mawazo ya watu hali ya kuwa na mimi nina uwezo kufikiri pia.
 
Hayo uliyoyaeleza ndivyo unavyoelewa na ndiyo maana nikasema endapo itathibitishwa uwepo wa mungu pengine uelewa wako huo utakuwa tofauti na uelewavyo sasa.
Endapo haijaenda.
 
Sihitaji kumeza mawazo ya watu hali ya kuwa na mimi nina uwezo kufikiri pia.
Hakuna utakachofikiria ambacho hakijawa mawazo ya watu kimsingi.

Erasto Mpemba aligundua "The Mpemba Effect", watu wakabukua wakakuta kumbe Aristotle alishaandika hayo mambo. Kina Edgar Allan Poe walishandika kuhusu ma black holes kabla hata hayajagunduliwa kisayansi.

Ukifikiri vingine utakuwa unajikweza visivyo.

Unaweza kutaja hata kimoja?
 
Huyu mh yupo wapi??

Ni mtabe sana huyu jamaa
 
Jitahidi kusoma na kuelewa vizuri dhana ya Utatu Mtakatifu kijana utaelewa vizuri
 
Yaan inashangaza sana watu wanaodai mungu hayupo

huku wakisalimu amri kila kitu alichosema mwenyezi mungu maelfu ya miaka iliyopita

Mfano (1) mungu anasema ndani ya kur an binaadamu hajapewa elimu ya roho ndiyo maana tunashuhudia roho inatolewa mbele ya madakitar bingwa lkn wanashindwa kuzuwia

(2) mungu anasema kila nafsi lazima itaonja mauti

Pamoja na maendeleo makubwa ya kielimu iliyopo sasa

Mmeshindwa kukanusha haya


Inaonekana wazi aliye tamka haya ana elimu zaid yetu
Kwan amesema mambo ambayo mpaka leo hakuna aliye kanusha imebaki bra braa tu
 
 
Swadaktaaaaaaaaaaaaaaa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…