Je! Mungu ni yule yule?

Hahahaha mkuu kweli hutaki mchezo
hahaaa umekuja !!? umeona wameshamkimbia kianga !?? tatizo watu waliokuja kujibu hoja zake niwepesi mnooo "" hii hoja nibora ungeianzisha kule kwenye jukwaa letu LA watu wenye akili nyingi
 
Hivi Kiranga amewahi kuthibitisha kwamba Mungu hayupo? Kuna ushahidi aliokuja nao kuthibitisha kwamba Mungu hayupo? Au ni dhana ile ile iliyozoeleka ya kuzunguka mbuyu!
Alisema huwezi kudhibitisha kitu ambacho hakipo!!! Yeye amesema Mungu hayupo sasa hapo unataka adhibitishe nini?

Wanasema yupo ndio wadhibitishe uwepo wa huyo Mungu

HAYO NDIO MAJIBU YA KIRANGA
 

Swali lako ni Does God Exist? Philosophers bila misingi yao ya imani wanatoa ushahidi kupitia reason na kujibu hilo swali. Wasome uwaelewe ndio ulete humu sio kupoteza muda wetu. Kama huwezi kuwaelewa hao huwexi kuyaelewa utakayoambiwa humu. Aquinas unayemtaja aliamini.
 

Wewe ni Genius
 
Mkuu, mimi nimenukuu tu na kuona ni hekima kuitumia hiyo nukuu.

Vv
acha kupenda kutumia hizo concipirace theory hao wajanja wajanja tu "" wametupiga brain wash ..wewe unaamini maneno ya kutungwa na watu hayo "" jiulize wew tangu upate ufahamu umeshawahi kuongopa Mara ngapi ..mpaka wao washindwe kukuongopea
 
hahaaa umekuja !!? umeona wameshamkimbia kianga !?? tatizo watu waliokuja kujibu hoja zake niwepesi mnooo "" hii hoja nibora ungeianzisha kule kwenye jukwaa letu LA watu wenye akili nyingi
Nimesoma comment yake moja moja na za wanaojibu hoja nimeona hawana hoja za kumshawishi mtu aamini zaidi kukazia "Yupo yupo amini ".

Hoja za Kiranga ni za msingi na mtu yeyote anayeweza kufikiria akiamua kukaa chini na kuanza kufikiria lazima aje na maswali ya Kiranga.
 
Alisema huwezi kudhibitisha kitu ambacho hakipo!!! Yeye amesema Mungu hayupo sasa hapo unataka adhibitishe nini?

Wanasema yupo ndio wadhibitishe uwepo wa huyo Mungu

HAYO NDIO MAJIBU YA KIRANGA
nashangaa mtu anauliza maswali ambayo yameshajibiwa
 
kuna watu wengine wanaelewa tu ila kwakuwa wamejikuta wameshakulia ktika hiyo mifumo basiii tu wanashindwa kujitoa ktika hiyo minyorolo ..."""
wanahofu ya kutengwa na ndugu na Jamaa zao ..lakini sio kwamba hawaelewi mkuu"" hapa wapo kubishana tu lakini akili zao zinapingana na maneno yao
 
Me pale kwenye bustani ya Eden ndio huwa sipaelewi kabisa.Tunaambiwa Mungu ndio mueza wa yote na alitujua kabla hata hajatuumba (Yohana) na anatujua mpaka mwisho wetu (yesu msalabani alivyomjibu yule aliyekuwa msalabani) ila sasa tunaambiwa Adamu alikatazwa asile tunda la kati(si mungu asingeuweka huo mti kabisa kwenye bustani) na wakila watakufa.

Kwa kuwa tunaambiwa Mungu anatujua kabla hajatuumba na mwisho wetu pia anaujua hivyo ule mti aliuweka makusudi pale kati wakina Adamu wale(Alijua kama watakula kabla hata hajawaumba).

Walipokula wakaadhibiwa!

Life is not fair
 
Deadbody, Biblia inasema kuwa "mpumbavu amesema moyoni mwake kuwa hakuna Mungu.".

Sasa unataka huyo mtu athibitishiwe vipi kuwa kuna Mungu wakati Biblia inamwita mtu wa namna hiyo kuwa ni mpumbavu? Unathubutu vipi kubishana na 'mpumbavu '?

Vv
Kiranga anasema mtumie hoja sio matusi. Hiyo biblia kiranga haiamini kwahiyo hata kilichoandikwa humo hakuamini
 
Nukuu ya Adolf Hitler..."It is easy to fight knowledge than to fight faith"
Na nnachoona hapa huyo jamaa ana knowledge ndo maana anatumia facts,lkn wanaomjibu wana Imani tu bila knowledge,hvyo wanakosa facts na kuishia kutukana tu.

Anyway...mambo ya kiroho ctakag kubishana..Nbak tu na Mungu wangu,kathibitika kwangu wala c kwa mwngne.
 
Inawezekana wewe ndio umeshindwa kulielewa swali kwa utashi japo swali lineulizwa kiufasaha

Nimekwambia nguvu zaidi ya hilo jua, sijui hujaelewa nini

Halafu mtu kushindwa kuthibitisha jambo flani lipo haimaanishi halipo. Mfano miaka ya nyuma, kabla ya kuthibitisha, hakuna aliyethibitisha kwamba kuna sayari nyingine zinazolizunguka jua.

Jambo lingine, huwezi kuthibitisha uwepo wa roho kwa kutumia mbinu za kimwili (ambazo wewe ndio unaziamini kama mbinu pekee za kuthibitisha jambo). Mshana alitangulia kusema hapo awali.
Yeye mwenyewe pia ameshindwa kuthibitisha kama aidha yupo au hayupo!
 
 
daaaahh nasikitika kuona hoja zako nzito kama hzi huwa zinajibiwa na watu wenye hoja nyepesi mnooo ""
Kuna mwanafaksafa anajulikana kama "God's Philosipher". Anaitwa Alvin Plantinga.

Katika dunia ya falsafa ya magharibi/ Ukristo, huyu ndiye mwamba katika kupangua hoja za wapinga kuwepo Mungu.

Na huyu mwamba kashindwa kujibu hili swali.

Papa wa Wakatoliki aliulizwa na kisichana huko Ufilipino, kwa nini Mungu kaachia ulimwengu wenye maovu kiasi kuna visichana vidogo vingi vinaishi kwa kujiuza miili yao? Mungu kashindwa kuzuia haya?

Papa akajiumauma tu, alishindwa kujibu swali.

Sasa hapa watu wengi ninaojibizana nao sio tu hawajamsoma Alvin Plantinga, hawajawahi hata kumsikia.

Sasa hapo majibizano lazima yawe magumu.
 
Nguvu zaidi ya hilo jua ndiyo ipi?

Ya Black Hole?

Zaidi ya hilo jua kwa kipimo gani?

Nikikwambia pembetatu yenye pembe sita ipo, ila huwezi kuithibitisha kimwili, utakubali ipo?
 
nashangaa mtu anauliza maswali ambayo yameshajibiwa
Nilijiunga na JF mwezi January mwaka 2014... ni hoja za kiranga ndizo zilizonifanya nijiunge humu. Waliojiunga 2017 hawatuelewi kabisa tunaposema Kiranga ni noma. Sasa kiranga akiamua kuandika kiingereza na usitoke hata na neno moja ndio utamkubali... nakumbuka walifanyaga debate ya kiingereza ilikuwa ni mtafutano humu.
 
haaahhaa kweli waliojiunga miaka ya hivi sasa hawawezi kuelewa ..kiranga ni hatari mnoo
 
naaam nikweli kabisaaa lazima majibizano yawe magumu !!?
ngoja na mimi ni tafute debate za huyo platinga nipate kujiongezea kitu ""
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…