Kuna mwanafaksafa anajulikana kama "God's Philosipher". Anaitwa Alvin Plantinga.
Katika dunia ya falsafa ya magharibi/ Ukristo, huyu ndiye mwamba katika kupangua hoja za wapinga kuwepo Mungu.
Na huyu mwamba kashindwa kujibu hili swali.
Papa wa Wakatoliki aliulizwa na kisichana huko Ufilipino, kwa nini Mungu kaachia ulimwengu wenye maovu kiasi kuna visichana vidogo vingi vinaishi kwa kujiuza miili yao? Mungu kashindwa kuzuia haya?
Papa akajiumauma tu, alishindwa kujibu swali.
Sasa hapa watu wengi ninaojibizana nao sio tu hawajamsoma Alvin Plantinga, hawajawahi hata kumsikia.
Sasa hapo majibizano lazima yawe magumu.