Je! Mungu ni yule yule?

You are running away, you are not done.

You have not answered my questions.
Skia bro umetoa contradictions zako, nmejibu moja wapo kama mfano tu na umeridhika. Madai yalobaki ni ushupavu binafsi. Unasema logics, nmekuuliza unaujua upepo? hujataka kujibu straight sasa nikusaidieje? Huna logic, huna points. Achana na sources za ku-google zitakupoteza. Ukitaka kumjua Mungu soma vitabu vitakatifu. Sina muda wa kutosha kujadili haya, wapo wanasayansi wakubwa dunia wamekiri uwepo wa Mungu, wew ni nan?

Hatufanyi mzaha hapa ujue
 
Unaelewa kwamba hujajibu swali nililouliza na kama umejibu umejibu swali ambalo sijauliza?

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauna shetani, hauna dhambi, hauna mabaya yanawezekana mazuri tu na viumbe wake hawawezi kufanya mabaya, watachagua mazuri yoyote wataweza kufanya,lakinimabaya hata hayawezi kufikirika.

Alishindwa kuumba hivyo?
 
Hujaondoa contradiction ya Mungu wako wa "pembe tatu yenye pembe sita".
 
Jaribu tu kuelewa kuwa hizo unazoita contradictions ni kwa kuwa knowledge uliyonayo iko limited na logics ulizosoma hii miaka 20 au 30. Panua akili kidogo and imagine kuna knowledge ambayo hujaipata tu (which is a big possibility considering educational advancement now compared to those medieval ages) ambayo mwanadamu hajfunuliwa kuja kukufundisha. Huwezi kujenga logic hapo. Kwako itakuwa contradictions tu. Ungekuwa salama kama ungechukua position explanation ya kilichoko kwa Bible sijaielewa, not because there’s contradictions but because the true meaning has not been revealed to me.
 
Hii umesoma wapi?
Unapoandika "hii" una maana gani? Umeelewa hata nilichoandika?

Your God,is, by definition, a contradiction, just like "pembetatu yenye pembe sita".

Kamavile "pembe tatu yenye pembe sita" ambavyo haiwezi kuwepo, Mungu wako naye hivyo hivyo hawezi kuwepo.

Kwa sababu, katika dhana ya kuwepo Mungu wako,kuna vitu vinajipinga kama inavyojipinga dhana ya "pembe tatu yenye pembe sita"
 

hiyo ni hekima yako, ambayo kwangu mim naweza sema ni ujinga pia. Nasema ujinga sababu unaongea jambo usilolijua
 
Talking abt trinity sio?
 
Ukikubali logic, Mungu wako hayupo kwa sababu hana logic.

Ukikataa logic, huwezi kuthibitisha Mungu wako yupo (unahitaji logic). Arguments zote za kuwepo kwaMungu ambazo zinatumialogic nazo zinavunjika.

Ukikubali logic, ukikataa logic, Mungu wako hayupo.
 
 
Ahaaa now I get you. Kuwa mtu akikubali kuwa limited na logic basi Mungu ni contradiction. As for logic, it is a tiny subject that serves to complete small small matters. But for big things I go for God. Una akili sana wewe kiranga. Sasa kuwa msomi zaidi. STOP BEING LIMITED BY LOGICS. THEY ARE A SMALL TOPIC IN A BIG SUBJECT CALLED REALITY. I rest my case.
 
Ukienda nje ya logic, chochote kinawezekana.

Umekubali Mungu yupo.

Umekubali Mungu hayupo.

Umekubali Mungu yupo na hayupo hapo hapo.

Umekubali Mungu yupo na hayupo, halafu katikati ya kuwepo na kutokuwepo hayupo na yupo.

Umekubali hayupo lakini anaonekana kama yupo.

Umekubali yupo lakini anaonekana kama hayupo.

Umekubali hujakubali ulichokubali.

Hujakubali kukubali.

Hujui umesimama wapi.
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ alokufundisha hizo tautologies kakuweza kweli
 
Umeshindwa hata kuninukuu.

Mungu wako ana contradiction, kama contradiction iliyo katika dhana ya "pembe tatu yenye pembe sita".

Kama "pembe tatu yenye pembe sita" isivyoweza kuwepokiuhalisia, ndivyo Mungu wakoasivyoweza kuwepo kiuhalisia.
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ alokufundisha hizo tautologies kakuweza kweli
Ukikataa logic, tautology inakuwa sawa na contradiction na chochote kinawezekana.

Hata pembe tatu yenye pembe sita inawezekana kuwepo.

Na Mungu wenu mwenye contradiction anakuwa a tautological fiat.
 
Ukikataa logic, tautology inakuwa sawa na contradiction na chochote kinawezekana.

Hata pembe tatu yenye pembe sita inawezekana kuwepo.

Na Mungu wenu mwenye contradiction anakuwa a tautological fiat.
Toka eeewe pepo wa logic na umwachilie mtu huyu, yeye ni mtoto wa Mungu aliye hai. Huna mamlaka juu yake
 
Watu wanaosemaMungu yupo, ukiwabana kwakuonesha Mungu waoana contradiction,logically hawezi kuwepokama"pembe tatu yenye pembe sita", wanakimbia kumzungumza Mungu huyo logically.

Wanajihami kwa kusema Mungu huyu hapimwi kwa logic.

Utetezi huu unajulikana sikunyingi. Wayunani wa kale waliuita "Deus ex Machina".

Wayunani walikuwa na michezo yao ya kuigiza, basi ikiwa mchezo wa kuigiza umekuwa so complex hauwezi kuwa resolved, say star kabanwa hana pakutokea, ili kumaliza mchezo, walikuwa wanamshusha Mungu wa mbaokutoka juu anakuja kumaliza mchezo.

Katikawatu wanaojua habari za "creative writing", story ikiwa na "deus ex machina" ni weakness, muandishi anaonekana mvivu na mzembe. Hakuwezakutunga story inayokuwa na resolution natural, ame force resolution.

Wanaosema Mungu yupo nje ya logic wameshindwa kumuelezea Mungu wao, wanatupa suluhishola "deus ex machina"

Deus ex machina - Wikipedia
 
Tetezi nyingi za Mungu huyu wa contradiction zinaangukia humu.

1. Deus ex machina
2. Logical Non sequitur
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…