Je! Mungu ni yule yule?

Una maana gani kusema kuamini kuwe njia ya kujua?

Hebu fafanua mkuu maana kushindwa kuelewana huku ndiyo sababu za hii mijadala kutokuisha.
Sina tatizo na mtu anayeamini kitu kilicho logically consistent na chenye overwhelming supporting evidence.

Kwa mfano. Leo mtu akiniambia anaamini jua litachomoza kesho. Hiyo ni imani. Sina tatizo na imani hiyo.

Kwa sababu, ina overwhelming supporting evidence. Katika miaka yote tunayojua ya kuwepo kwa watu hakuna siku jua liliposhindwa kuchomoza. Tumesoma fizikia ya anga na kujua jua linavyofanya kazi. Pia habari ya jua kuchoniza kesho haina contradiction yoyote.

Hivyo mtu akiniambia anaamini jua litachomiza kesho, sitamshangaa. In fact anayeniambia haamini jua litachomiza kesho ndiye nitamshangaa.

Lakini mtu anayeamini Mungu ambaye hathibitishiki na wala hana logical consistency, tena ana contradiction, huyu atapata maswali yote yenye mshangao na hija kwamba anaamini hadithi ya Mungu ambaye hayupo.

Tatizo si imani. Imani hata unapokanyaga sakafu kutika kitandani asubuhi, uneshaamini sakafu itaku support na haitaoasuka na kukumeza.

Tatizo, imani ipo logical au illogical?
 
Sikukujibu hulo swali nikakaa kimya?

Unaelewa kukaa kimya ni nini?

Sijakujibu kirefu kwa mfano wa square root ya 2 kwamba inawezekana nisijue jibu la swali lakini nikajua jibu la Mungu ni la uongo kama ninavyoweza kutokujua square root ya 2 ni nini lakini nikajua jibu la 10 ni la uongo?
 
Nadhani hujui kinachoongelewa hapa.Nani aliyesema kuwa hayo maumbile yametoakana na nature!!?

Kiranga ameshasema hajui.Na kutokujua kwake usimlazimishe aamini kuwa tumembwa na fulani wakati hata hata kwa akili ndogo tu inagoma.
Unamwambia mtu hujui jibu. Tunahitaji uchunguzi zaidi. Inawezekana chanzo si Mungu wala nature kuna dubwana jingine huko tofauti kabisa hata kulitaja hatujaanza kuelewa kulitaja.

Mtu anakupa jibu kwa kukisia tu unamaanisha nini.
 
Species ya samaki kubadili jinsia kutoka jike kuwa dume au vice versa kuna contradict vipi nature wakati kubadilika huko ndiyo nature yenyewe?

Unajua kuna sexual reproduction na asexual reproduction isiyohitaji species kuwa hata na sex ya dume au jike?

Unafahamu contradiction ni nini?

Wapi nature iliwahi kusema ni lazima kuwa na jike au dume tu na jike haliwezi kubadilika kuwa dume na dume haliwezi kubadilika kuwa jike?
 
Kiranga
Unaweza kumuoa dada yako au mkakubaliana kuwa wapenzi?

Au mama yako let's say she have raised you as a single mother, Je ukikua unaweza kumuomba muwe wapenzi??

Na kama hauwezi ni kwa nini? Kwani hii nayo inaingia katika katika maana zako za kutambua uovu?
 
meaning
 
Ukishapost kitu JF, tayari ushajitoa katika kanuni ya "kila mtu awe na lake".

Kwa sababu kitendo cha wewe ku post bandiko JF tu, umeshataka kumpa lakomwingine asome.

Kama kweli unataka kila mtu awena lake, kuhusu sualahili, usibandike kitu JF kuhusu hili.

Kuna watu wengi wanaamini hivyo, na hawachangii mijadala hii.

Ukichangia tu, umeshavunja kanuni ya "kila mtu awena lake", kwa sababu wewe mwenyewe hujakaa na lako umelileta JF.
 
meaning?
 
Nyie mnaompinga Kiranga ni wagumu sana wa kuelewa.Kutokujua jibu sahihi la swali fulani hakukufanyi uamini jibu unalopewa moja kwa moja.Lazima kwanza ulitazame kama linakubaliana na logic ama kanuni za msingi!


Mfano ni huu,

Tuashumu wewe hapo ulipo una umri wa miaka 40.Bahati mbaya toka uzaliwe hukuwahi kumuona baba yako mzazi na hivyo humjui.Nami siku moja nikakuuliza swali la unamfahamu baba yako mzazi!? Ukanijibu humjui.Kwa kuwa humjui nikakuonesha ka bwana mdogo kenye umri wa miaka 25 kuwa ndiye haswa baba yako mzazi.Je,utanikubalia kwa sababu tu toka uzaliwe hujawahi kumuona baba yako mzazi?.

Hapo lazima unikatalie tu maana kwa umri wako wa miaka 40 haiwezekani baba mzazi wako awe na umri wa miaka 25.

Hata kama humjui baba yako mzazi lakini kuna kanuni muhimu tayari unayo kichwani,nayo ni kuwa baba yako mzazi sharti kwanza awe na umri mkubwa kuzidi wewe.
Kwa hiyo si kweli kwamba kutokujua kwangu jibu sahihi la swali lako ndiyo kunifanye niamini jibu unalonipa.Ninaweza nikalikubali ama kulikataa na jibu langu likaendeea kubaki lile lile kuwa sijui jibu sahihi.
 
Completely irrelevant example.
 
si kila bada linaletwa na mungu, hata siku moja mungu asingependa wanadamu wafe au wapotee but kama unakumbuka lile neno linalosema ole wao wakaao katika nchi kwa kuwa mshitaki wenu ameshushwa duniani Basi unamjua mshitaki wako ni nani, jibu ni Shetani ambaye ni mungu wa dunia. Jiepushe na roho zidanganyazo maana shetani alipotupwa duniani alishuka na baadhi ya malaika waliokuwa wakimkubari pia na ndio hao wanaotoa vishawishi vya mtu kutomuamini kama mungu hayupo
 
Sasa kama mungu mwenyewe hapendi mabaya inakueje kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana na kwanini amshushe duniani huyo shetani kwani wakati anamuumba hakulijua hilo vipi uwezo wake wakujua mwanzo na mwisho wa kila kitu kabla hajakiumba?
 
Una maana gani kusema kuamini kuwe njia ya kujua?

Bado hujatoa ufafanuzi katika hilo,umeeleza sana jinsi unavyochukulia imani ila kauli ya kwamba kuamini kuwe njia ya kujua bado haujatoa ufafanuzi.
 
Una maana gani kusema kuamini kuwe njia ya kujua?

Bado hujatoa ufafanuzi katika hilo,umeeleza sana jinsi unavyochukulia imani ila kauli ya kwamba kuamini kuwe njia ya kujua bado haujatoa ufafanuzi.
Nina maana kwamba , kuamini kusiwe mwisho, kuwe kunatumika kupata kujua, in a converging, verifiable, logically consistent mannar.

Ukifanya kuamini ndiyokuwe mwisho wa habari, nitakuambia mimi ndiye Mungu niliyeumba kila kitu,as long as kuaminindiyo mwisho wa ulimwengu wako, hapo unaamini au huamini, bila maswali.

Hii ni njia mbovu sana ya kuishi, kwa sababu utaaminiuongo mwingisana na hutaamini ukweli mwingi sana.

Ndiyo maana nasema, imani iwe njia ya kuufikia ukweli.

Nikikwambiamimi ndiye Mungu niliyeumba kila kitu, whether unaamini auhuamini si muhimu sana, muhimu sana ni maswali utakayojiuliza baada ya kuamini au kutoamini kuhakikihabari hii na kuijua kama ni ya ukweli au si ya ukweli.
 
Sasa baada ya maelezo hayo je,hauoni kuwa kauli yako ya kusema hautaki kuamini ila unataka kujua huwa si sahihi?

Hadi leo watu huamini kuchomoza kwa kujua na huna tatizo na hilo,sasa iweje kwenye kuhusu mungu ndiyo useme hautaki kuamini bali unataka kujua? Au kuna ukweli gani uliyopatikana toka watu waanze
kuamini kuchomoza kwa jua?
 
Muktadha, muktadha, muktadha,unaelewa maana ya hilo neno?

Imani ya kwamba kesho jua litachomoza hainipi tatizo, kwa sababu.

1. Haina contradiction. Hakuna popote unapoweza kunipa habari ya kueleweka inayosema kwamba habari ya kesho jua kuchomoza ina contradiction .Sina tatizo nayo.

Habari ya Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kuwepo na kuumba ulimwengu huu wenye mabaya mengi ina contradiction. Nina tatizo nayo.

2. Ina ushahidi. Habari ya jua kuchomoza kila siku kwa miaka nenda rudi, maelfu kwa maelfu ni ushahidi uliowekwa na kupimwa. Jua linaonekana, limesomwa, linajulikana linavyofanya kazi, watu wamelipigia hesabu mpaka litazimika lini. Sina tatizo na vitu vyenye ushahidi.

Mungu wenu hana ushahidi walauthibitisho wowote kwamba yupo. Nina tatizo na habari ambazohazina ushahidi wala uthibitisho.

3.Habari za jua kuwepo hazina tatizo la logical consistency. Watu wameelezea jualinavyofanya kazikwa ufanisi tangu Laplace. Hilisina tatizo nalo.

Mungu wenu ana tatizo la logical consistency. Hakuna anayeweza kumuelezea akaeleweka. Hilinina tatizo nalo.

Mungu wenu hana ushahidi, hajulikani, hasemekani, hapimikani, haelezeki, ni dubwana lililowekwa kuficha tusiyoyajua tu bila ya hilodubwana kuwepo. Hili ni jambo ambalo nina tatizo nalo.

Kwa sababu hizi mbili tu za haraka haraka, imani ya jua kuchomoza kesho hainipi tatizo, kwa sababu ina ushahidi uliokusanywa miaka mingi, pia haina contradiction
 
Mkuu sijafika huko kwenye kuichambua imani iwe ina contradictions au haina.

Bado nipo kwenye neno imani au kuamini,ulivyosema hautaki kuamini bali unataka kujua haukusema hautaki kuamini imani zenye contradictions tu.

Wewe mwenyewe umesema imani iwe njia ya kuufikia ukweli/kujua tusibaki kuamini tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…