Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Sina tatizo na mtu anayeamini kitu kilicho logically consistent na chenye overwhelming supporting evidence.Una maana gani kusema kuamini kuwe njia ya kujua?
Hebu fafanua mkuu maana kushindwa kuelewana huku ndiyo sababu za hii mijadala kutokuisha.
Kwa mfano. Leo mtu akiniambia anaamini jua litachomoza kesho. Hiyo ni imani. Sina tatizo na imani hiyo.
Kwa sababu, ina overwhelming supporting evidence. Katika miaka yote tunayojua ya kuwepo kwa watu hakuna siku jua liliposhindwa kuchomoza. Tumesoma fizikia ya anga na kujua jua linavyofanya kazi. Pia habari ya jua kuchoniza kesho haina contradiction yoyote.
Hivyo mtu akiniambia anaamini jua litachomiza kesho, sitamshangaa. In fact anayeniambia haamini jua litachomiza kesho ndiye nitamshangaa.
Lakini mtu anayeamini Mungu ambaye hathibitishiki na wala hana logical consistency, tena ana contradiction, huyu atapata maswali yote yenye mshangao na hija kwamba anaamini hadithi ya Mungu ambaye hayupo.
Tatizo si imani. Imani hata unapokanyaga sakafu kutika kitandani asubuhi, uneshaamini sakafu itaku support na haitaoasuka na kukumeza.
Tatizo, imani ipo logical au illogical?