Je! Mungu ni yule yule?

Sasa si tutakuwa vichaa kuamini kitu ambacho hakipo?
Sasa kama kweli hicho kitu kipo kwanini ushindwe kukithibitisha? Unashindwa kwasababu hakipo
Itakuwa ni ajabu pia kung'ang'ania kusema kuwa kitu hakipo lakini huna uhakika kuwa hicho kitu hakipo,maana ungekuwa na uhakika kuwa hicho kitu hakipo basi ungeyaeleza yale yenye kukufanya hadi ukawa na uhakika kuwa hicho kitu hakipo. Ukiona mtu anasema kitu hakipo halafu hawezi kuthibitisha kutokuwepo kwa hicho kitu basi ujue huyo mtu hicho kitu hakijui na ndiyo maana ana kosa sababu za kuthibitisha kuwa hicho kitu hakipo kwa sababu hata hakijui.
 
sasa sisi ni kina nani na ilikuwaje tukawepo hapa duniani
Katika kutafuta majibu, kuna njia nyingi.

Moja wapo ni "elimination process". Unaelewa theory, unaichambua, unaikubali au kuikataa kutokana na merits au demerits same.

Mimi siwezi kujifanya unajua sisi ni nani na tumetokeaje.Point ya kuntenganisha Homo Sapien Sapien tu na wengine si rahisi hata kwa watu waliosomea hili maisha yao yote.

Ila ninachosema kutuambia kwa uhakika ni kwamba hatujaumbwa na Huyo mungu wa vitabuni. Kwa sababu anafeli basic and simple checks.

Checks kama logical consistency. Which is a very elementary test.

Ni kama umuulize mtu square root ya 2 ni nini, halafu mtu akakwambia siijui, lakini unajua hawezi kuwa 10. Kwa sababu 10 ni kubwa kuliko 2 na square root ya 2 ni ndogo kuliko 2.

Hapo kuna a logical consistency test ndogo tu inayokuonyesha kwamba, hata kama hujui square root ya 2 ni ipi (an irrational number by the way), haiwezi kuwa 10.

Sasa hawa wanaotuambia kuna mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu unaowezekana kuwa na mabaya kama huu ni kama mtu anayekuambia square root ya 2 ni 10.

Haiwezekani, hatabila ya kujua tulipotokea ni wapi, kwa sababu jibu la 10/mungu huyu halina logical consistency.
 
Kwa nini unafikiri kuna kitu kama "mwanadamu wa kwanza" in the first place?

Kipimo chako cha kusema "huyu ni mwanadamu" ni kipi?
Haujajibu swali lake kwa jinsi aelewavyo wala haujaweza kuonesha hivyo anavyofikiri si sahihi.
Mueleze sasa kipi ni sahihi kama unaona hivyo anavyofikiri pengine si sahihi.
 
Ni utumwa mbaya sana kuamini kuna mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo, aliyeko kila mahali, nk. Huo ni upunguani na ni upumbavu kukubali hayo.

Tujikomboe na huu utumwa [emoji16]
Unaweza kunithibitishia kuwa kuamini kuwa hakuna mungu ni uhuru na si utumwa?
 
Haujajibu swali lake kwa jinsi aelewavyo wala haujaweza kuonesha hivyo anavyofikiri si sahihi.
Mueleze sasa kipi ni sahihi kama unaona hivyo anavyofikiri pengine si sahihi.
Unajuaje kwamba sijaweza kuonyesha afikiriavyo si sahihi?

Umeingia kichwani mwake?

Mtu akiuliza kuhusu mwanadamu wa kwanza, ni lazima atupe kipimo cha uanadamu.

Kipimo cha uanadamu ni nini?
 
Unaweza kunithibitishia kuwa kuamini kuwa hakuna mungu ni uhuru na si utumwa?
Utakuwaje mtumwa wa kitu ambacho hakipo?

To the contrary, unakuwa mtumwa wa kile ambacho kipo.
 
Wakuthibitisha ni wewe unaesema yupo.
Mungu wao angekuwapo, kusingekuwa na mabaya.

Kuwepo kwa mabaya ni ushahidi kwamba mungu huyo hayupo.

Ama sivyo, kwa nini mungu mwenye ujuzi wote, upendo wote na uwezo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana?
 
Unajuaje kwamba sijaweza kuonyesha afikiriavyo si sahihi?

Umeingia kichwani mwake?

Mtu akiuliza kuhusu mwanadamu wa kwanza, ni lazima atupe kipimo cha uanadamu.

Kipimo cha uanadamu ni nini?
Sijaona maana ya swali lako pengine labda ungeliweka vizuri.
 
Mungu wao angekuwapo, kusingekuwa na mabaya.

Kuwepo kwa mabaya ni ushahidi kwamba mungu Huyo hayupo.

Ama sivyo, kwa nini mungu mwenye ujuzi wote, upendo wote na uwezo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana?
Nimechoka kurudia maneno mkuu. Hawa watu wana akili lakini wanaziweka pembeni kwenye maswala yanayomhusu huyu mungu wao.
 
Kwanini nini mie? Ina maana wewe hutaki watu wapate uhakika na usemayo?
Haiwezekani kuwepo na Mungu mwenye uwezo wote, upendo, muumbaji wa vyote na aliyeko kila mahali huku tushuhudie mapungufu mengi kiasi hiki kwenye ulimwengu huu mnaosema kwamba kauumba yeye.
 
Sasa si tutakuwa vichaa kuamini kitu ambacho hakipo?
Sasa kama kweli hicho kitu kipo kwanini ushindwe kukithibitisha? Unashindwa kwasababu hakipo
Hii mmetoa wapi kama mtu akishindwa kukuthibitishia kitu kwa njia unayoitaka basi hakipo...?!

ndio maana nakwambia "logic" inakwambia tutakuwa vichaa, akili bana...

Imani ipo juu ya mantiki...

Hivi kwa mfano nikishindwa kukuthibitisha hapa nilipo navuta hewa, basi itakuwa sivuti ama...?!
 
Kina nani wamemtunga...?!
 
Mpaka hapo bado hujathibitisha kuwa Mungu yupo, naona unatoka nje ya mada tu

Kwani mada inataka kuthibitisha Mungu yupo...?! Ila wewe unayetaka uthibitisho ndio upo ndani ya mada...?!

Bado sijathibitisha kiaje, nimekwambia kama unataka nikuthibitishie maabara kwa kweli siwezi kuthibitisha kwa njia unayoipenda wewe...

Hebu labda nikuulize wewe ulijuaje kwamba hayupo...?!
 
Najua kwasababu hayupo na hajawahi kuwepo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…