Hakuna mungu, huyo unayemsoma ni hadithi tu zimetungwa na watu.
Ukijua hili swali lako halitakutatiza.
Kwa hiyo Mkuu Kiranga huwezi kuamini kuwa Mungu yupo hadi umuone? Tutaaminije kuwa kuna mtu aliitwa Vasco da Gama ilihali hatumuoni. Kama historia iliyo ktk vitabu vya dini ni maneno ya watu tu unatushauri tusiamini historia kwa sababu ni hadithi tu zilizotungwa na watu?
Unataka kutuaminisha kuwa hata wajerumani hawakuitawala Tanganyika kwa sababu kina Gen. Smutts hatuwaoni?
Lakini nyinyi kina Kiranga msioamini uwepo wa supreme being, kama wengine wanavyoita, mna ushahidi gani wa coincidence ya namna hii, kuwa eneo moja watokee viumbe hai wa aina tofauti, wenye uwezo tofauti bila kuwa na mpangaji? Tizama tu ulivyo, macho mawili, Masikio mawili, siyo moja nk. Angalia hizo sense zinavyofanya kazi. Mfumo wa mwili na ubongo, kwamba vitu hivi vijitengeze vyenyewe kwa mpango mkuu kiasi hiki cha kustaajabisha. Hakuna ushahidi wa kisayansi hadi muda huu wa kuthibitisha hayo mnayoyasema. Hakuna pori lolote, mahali popote, ktk Dunia hii, ambapo imegundulika kuwapo na aina yoyote ya kiumbe kinachoanza kujiumba chenye mwelekeo wa baadaye kuja kuwa binadamu au ht Simba. Mfumo wa kujiumba ungekuwepo mfumo huo usingehangaika kutengeneza dume na jike ambao ni very sophisticated. Mfumo ungeendelea kuproduce viumbe kwa njia hiyo hiyo iliyoanza nayo. Kwa vyovyote, mfumo tulio nao wa reproduction ni planned very carefully. Tatizo lenu ni huyo, the great planner, hamumuoni, na nyinyi mnataka ushahidi wa 5 senses, kuona, kusikia, kugusa, kunusa na kuonja. Nyinyi ni sawa na watu waliokuta hoteli kubwa porini, wakaingia ndani, wakakuta kila kitu, wakala, wakaoga na kulala bila kumuona mwenye hoteli. Kesho wakaondoka na kuamua kuwa hoteli ilijijenga yenyewe kwa sababu hawakumuona mjenzi wa Hoteli.
Mpango wa Mungu unatisha, the universe inavyofanya kazi. Mwendo wa kasi wa Dunia ya speed zaidi ya 105,000 kwa saa, haijapungua wala kuongezeka. Na hii ni kuwahi majira ya siku na mwezi. All these are the plans of the Great Being.
Jamani, wakati fulani tunatakiwa kuamini ukuu na uwepo wa huyu Muumbaji na mpangaji Mkuu kwa kuona na kushuhudia uumbaji na ubunifu huu wa ajabu.
Sio lazima Mungu awaeleze kila kitu kuhusu yeye. Sio lazima Baba au Mama yako akueleze kila kitu kuhusu kupatikana kwako. Siyo lazima akuambie mimba yako ilipatikana muda gani, kwa staili gn ya kujamiana.