Je, Musa hakuandika kitabu cha Mwanzo??

Embu weka hiyo mistari
 
Nimemsikiliza ila anachozungumza kinakinzana na imani anayosimamia haimaanishi kua yupo neutral

Hujamsikiliza mpaka mwisho kwani time ya hiyo clip ni nusu saa na wewe umerukia kuandika hata dakika kumi haijafika
 

"Yehovah atapaka watu mavi naam mavi ya vyakula vyao" Malaki 2:3

Yaani huyu yehovah hatarii
 
Mkuu cjui umeelewa concern yangu kwamba mtu anayesema WALA HAJAINUKA ni mtu mwingine.... Ikimaamisha Musa mwenyewe asingeweza kutoa hii kauli ya "majigambo" ilihali alishakuwa amekufa hivyo ni moja ya sababu kwamba tunaamini hakuandika kitabu cha mwanzo.

Kingine kuhusu hii sentensi ni kwamba ipo kwa wakati uliopita kimaandiko yaani mtu anasimulia experience ya jambo fulani na sio wakati uliopo sababu Musa amemaliza safari na amemkabidhi joshua alafu kauli itolewe kwamba WALA HAJAINUKA..... Haileti maana unless mwandishi alishaona manabii kama musa,joshua,obadiah n.k ndio akafikia hitimisho kuwa WALA HAJAINUKA.....

Mfano siku nyerere anamuachia mwinyi alafu mtu aseme HAJATOKEA Rais kama Nyerere ilihali hata mwinyi hajaanza kuongoza ita make sense kweli??
 
Nakubaliana na wewe kwamba musa alipewa maagizo akawaambie kwa sababu alikuwa nao karibu lakini kulikuwa na muweka kumbukumbu wake alieitwa yoshua
Lakini mpaka joshua anakufa hakukuwa ma kabila la wakaldayo sasa iliwezekanaje Joshua akarefer kabila ambalo halipo duniani yaani mtu aandike kwenye gazeti kuwa kabila la WAAMALEKI linaishi moshi ilihali hilo kabila bado hatujawahi liona moshi unafkiri message itaeleweka kweli?? Huoni alieandika hapa aliishi miaka mingi baada ya joshua baada ya kabila hili kuwepo duniani
 
We unavionaje hivo Vitabu?
Vinahekima?
Kina hekima sana tu mkuu ila mie nina shida na uandishi tu.... Je kwanini waseme kimeandikwa na Musa na wasiseme aliyekicompile alikuwa ni nani na kama anaaminika isije ikawa compiled na wapagani wachache wakaingiza maoni yao kwenye Biblia hasa mwanzo 6 na 10 ambazo zimezaa utata mkubwa sana kwenye kitabu cha mwanzo.
 
Embu weka hiyo mistari
Siwezi copy sura zote 14 mkuu ila kapandisha mlimani kwenye kutoka 24 sasa kama aliandika pentateuch huko je sura ya 27 na kuendelea iliandikwa lini na wapi ilihali inaeleza maisha ya baada Musa kushuka toka mlimani

Yaani kama pentateuch yote iliandikwa kwenye zile siku 40 zile sura zilizofuata baada ya tukio la kutoka mlimani zimeandikwa na nani na lini ilihali Musa alishakuwa ameshuka??
 
kukuelewesha itakuwa ngumu sana.
tatizo hutaki kuelwa Ila unataka kubishana na kufanya hoja & mawazo yako ndiyo yawe huru.
kama upo na utayri wa kutaka kuelewa kubali kuwa humble
 
kukuelewesha itakuwa ngumu sana.
tatizo hutaki kuelwa Ila unataka kubishana na kufanya hoja & mawazo yako ndiyo yawe huru.
kama upo na utayri wa kutaka kuelewa kubali kuwa humble
Unataka kunielewesha kwa fact au kwa imani?
 
Ndio maana nikasema hawakuandika kwa akili zao wenyewe Bali walisaidiwa kutoka juu
Ndio maana nikasema ukisoma kwa makini kitabu cha mwanzo ambacho huonyesha asili ya vitu vilipotokea utagundua aliyekuwa anatusimulia ni Mungu mwenyewe ambaye yeye anajua linalokuja mbele kuliko sisi binadamu
 
Hapa tunatofautiana jambo moja! Musa hakua akiandika maneno yake mwenyewe bali maagizo aliyopewa ma Mungu kupitia roho takatifu. Kwahiyo hilo neno HAJAINUKA au HAJATOKEA halimishi ni Musa aliandika kwa kujigamba bali ni Mungu alimwambia aandike vile kwa sababu ya imani Mungu aliyoiona kwa Musa. Kumbuka hili sio jambo pekee Musa alikoandika linalomuhusu yeye binasfi. Kuna wakati alimkosea Mungu na akapewa adhabu ya kutoingia nchi ya ahadi na bado aliandika mambo hayo. Hizo ndizo sababu zinasomfanya Musa kuwa mmoja wa watumishi waadilifu kabisa wa Yehova

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Lakini mkuu neno hili WALA HAJAINUKA limeandikwa baada ya Musa kufa je kama ni Mungu ndio alimuambia aandike ni muda gani ilihali limetamkwa baada ya kifo cha Musa ikimaanisha kulikuwa na mtu wa tatu aliyeripoti hii habari..... Na ndio naibua swali hapo kuwa alikuwa nani?? Na kama alikuwa mtu mwingine je kwanini tuambiwe muandishi wa kitabu cha mwanzo hadi kumb. Ni Musa

Hapo ndio nataka kuelewa mkuu
 
Hivi vitabu vinaitwa vitabu vya musa sio vitabu alivyondika musa

sababu ya kuviita vitabu vya musa ni kwa sababu matukio ya musa toka misri mpaka mlima sinai yaliacha maandiko ambayo kwa hayo watu waliweza kuandika story kamili kama mungu alivyokusudia

mfano
unaweza kusoma kitabu kinaitwa kitabu cha mkwawa
haimaanishi mkwawa ndie aliyeandika lakini matukio ya mkwawa ndio yamesababisha tupate story nzima
 
Mkuu kwenye machapisho yooote ya kiimani wanasema AUTHOR wa VITABU VYA MUSA ni Moses..... Ndio maana ikaleta maswali. Ila hiki unachosema ndio sahihi kwamba kuna WATU waliandika na wakatumia Musa kama chanzo cha taarifa zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…