Je, Mwalimu alihodhi maendeleo na kupeleka Butiama??

Je, Mwalimu alihodhi maendeleo na kupeleka Butiama??

Jasusi,

..now, how about kati yako wewe na Bibi Ntilie? kwasababu to some extent she is agreeing with what Manyerere is saying about Butiama.

Bibi Ntilie,

..asante kwa kutuhabarisha kuhusu mchango wa Joseph Nyerere.

..je, kati ya aliyoyaeleza Manyerere ni yapi ya kweli na yapi ya uongo?

..je, unaweza kutueleza mara ya kwanza kufika Butiama ilikuwa lini? vilevile umetembelea mara ngapi Butiama?

..Jasusi alikuwa huko 2004, na Magabe alikuwa huko in the 90s.

Magabe Kibiti,

..wewe uliona magofu ya kitu gani huko Butiama?

..it is you against Manyerere na Bibi Ntilie
.

Fafanua swali lako hapa mzee

Kumbuka mimi niliandika hiki hapa:

Kwamba,

hakukuwa na magofu ya viwanda vya nguo, benki mbili, matrekta na malori yasiyo idadi, nk nk

Unataka niseme magofu yapi tena?
 
Jasusi,

..now, how about kati yako wewe na Bibi Ntilie? kwasababu to some extent she is agreeing with what Manyerere is saying about Butiama.

Bibi Ntilie,

..asante kwa kutuhabarisha kuhusu mchango wa Joseph Nyerere.

..je, kati ya aliyoyaeleza Manyerere ni yapi ya kweli na yapi ya uongo?

..je, unaweza kutueleza mara ya kwanza kufika Butiama ilikuwa lini? vilevile umetembelea mara ngapi Butiama?

..Jasusi alikuwa huko 2004, na Magabe alikuwa huko in the 90s.

Magabe Kibiti,

..wewe uliona magofu ya kitu gani huko Butiama?

..it is you against Manyerere na Bibi Ntilie.

jokaKuu,
Between me and Bibi Ntilie, I think Bibi Ntilie is more credible.
Mimi pale Butiama nimepita kama mgeni. Bibi Ntilie has spent much time
there and she knows the place much better than I do. Hapana, siwezi kusema aliyoandika Manyerere yote ni ya uongo labda tu kuwa wana malori mengi pale Butiama. Mimi sikuyaona, unless waliyaficha kwenye mazizi ya ng'ombe.
Mara ya kwanza kufika Butiama was 1973, just a few hours visit. Sikurudi tena mpaka mazishi ya Mwalimu 1999. Halafu I was there last time 2004. Kwa sababu ya ugeni I was not looking for magofu or anything. Hope that helps. But my offer still stands. There is no better proof than eyewitnessing.
 
Nakushauri mwenyewe utembelee Butiama ujionee. Sijui Jackton anazungumzia Butiama ipi. Maendeleo pekee niliyoona pale wakati wa mazishi ya Mwalimu yaliuwa kuwepo umeme na viosk vya Vodacom na Tritel. Na urithi pekee ambao Mwalimu aliwaachia nje tu ya Butiama(kuelekea Kiarano) ni bwawa kubwa la maji kwa sababu hawa walikuwa wakihangaika kutafuta maji siku nzima. Kama kuna benki na posta basi zimefunguliwa baada ya 2004( last time I visited) Na sina hakika kweli kama huyo mwandishi amekulia Butiama. Anaweza kuwa ana asili ya hapo lakini sidhani anaijua Butiama.

Wakati wa Uongozi wa Mwalimu Nyerere na wakati hasa ambao alisisitiza vijiji vya ujamaa, Butiama ilikuwa ni kijiji cha mfano. Kwanza ni kweli kwamba ofisi ya posta imekuwapo Butiama tangu Julius Kambarage Nyerere akiwa Rais wa Tanzania na mpaka leo posta ipo, Butiama imekuwa na hospitali ambayo ina hadhi ya hospitali ya wilaya wakati akiwa Raisi na hadi leo, Butiama pale kulikuwa na Irrigation Farm ikiendeshwa na Wakorea bahati mbaya "is no more", kulikuwa pia na mashine za kusaga, ni kweli pia Butiama ilikuwa kijiji cha kwanza kupatiwa umeme Mkoani mara baada ya umeme wa gridi kufika mkoani mara, Kulikuwa pia na shamba la mifugo la kisasa na kituo cha uzalishaji ng'ome (Artificial Insemination Centre) kilichokuwa kinaendeshwa na Wa-Cuba. Pia kulikuwa na tawi moja la NBC kabla haijabinafsishwa. Kwa hiyo, kama ni maendeleo Butima ilikuwa na maendeleo kuzidi miji mingi tu ya Tanzania.

Kitu ambacho hakikuwepo Butima wakati wa Nyerere ni kwamba hapakuwa na Barabara ya lami hadi anastaafu. Barabara pekee ya lami kwenda Butiama ni ile inayotokea barabara ya Mwanza-Musoma kutokea Kiabakari, nayo ilijengwa wakati wa utawala wa Mkapa.

Ni kweli pia hadi anastaafu mwalimu hakuwa amejenga nyumba yenye hadhi yake kama Rais, nyumba pekee aliyokuwa nayo ni ile iliyojengwa Mwitongo, na alijengewa na Samora Machel. Baadaye ndo JKT walimjengea nyumba ambayo leo hii ni Maktaba yake hapo Butiama.

Mambo mengi aliyoongelea Manyerere Jackston ni ya kweli.

Mimi nilifika Butiama mara kadhaa wakati Nyerere akiwa Rais na Baada ya kustaafu. Naweza kusema kwamba Butima ya leo haina maendeleo ukilinganisha na Butiama ya wakati wa Mwalimu.

Tuendelee kupeana habari
 
Ngereja,
Asante kwa masahihisho. Alishasema vivyo hivyo Bibi Ntilie. Lakini kitu ambacho kimenikuna ni what happened kwa vijiji vya ujamaa? Mama Ntilie amezungumzia kijiji kingine kule Iringa, je hivi vijiji mbona havikuendelezwa? Kama hiki cha Butiama kingekuwa mfano mzuri na kingesaidia sana uzalishaji na ajira. Je, vimekufa kwa sababu ya uongozi mbovu au tangu Tanzania iachane na ujamaa serikali za Mwinyi na Mkapa kwa makusudi ziliamua kuviachia hivyo vijiji, hasa vile vilivyokuwa vimefanikiwa vife kimya kimya?
 
Jokakuu,
Aliyoandika Manyerere ni kweli kabisa.Ukweli huo umeungwa mkono wa wachangiaji wanaoijua Butiama barabara kama Ngereja na bibi Ntilie.Ngereje ameandika ya kweli zaidi na mimi nampa credit zaidi.Huyu MAGABE KIBITI ni wale wanakurupuka ili kuonyesha wanajua vitu kiasi gani wakati hawajui lolote.Huku kutoroka shule kwa bwn Magabe kwenda Butiama mimi naweza kusema alikuwa anaishia kwenda kushangaa nyumba anayoishi Nyerere tu na kurudi.kimsingi haijui butiama inayoongelewa na manyerere,bali anajua vipande vya ka-butiama tena ya miaka ya 90 tena naweza `kupinga kuwa hata huko kwenda butiama ilikuwa labda ni mara moja baada ya miaka 2 tena wanaenda kama darasa kutembelea nyumba ya Nyerere.

Usiogope mtu kuzaliwa Tarime na kusoma Mara sec ukafikiri anaijua butiama.La hasha.Sisi tulizaliwa Makutano lakini kuna kaka yangu hajawahi kufika Butiama.

Ni kweli butiama ilikuwa na maendeleo kama hayo yaliyosemwa na Manyerere.Mimi binafsi huwa namlaumu Nyerere kwa kupendelea Butiama na kusahau baadhi ya sehemu za mkoa wa Mara ususani majita na Kibara.Kama hoja ni vijiji vya ujamaa haikuwa Butiama pekee.Nenda Mugango,murangi,Bukima au Namhula kijiji cha ujamaa kule Iramba-kibara utaona ni jinsi gani maendeleo ya mkoa huo yalielekezwa huku juu zaidi ya sehemu zingine.
mimi nimezaliwa makutano nimekulia Buhare nimefanya kazi Majita A,Mwibagi,Mwigundu,Kutanu,Butiama,Utegi na sehemu zingine nyingi tuu.So naweza kusema kuwa Mwl alihodhi maendeleo na kupeleka Butiama tabia inayoendelezwa na mbunge mkono.Dawa ya kuondoa hii mentality ya kupendelewa huko juu kwa mkoa wa mara (hasa majita) ni kutengwa kwa jimbo la musoma vijijini ili sisi wajita tujitawale wenyewe na hawa wa huku juu nao waendelee na uchifu wao.
 
Ngereja,
Asante kwa masahihisho. Alishasema vivyo hivyo Bibi Ntilie. Lakini kitu ambacho kimenikuna ni what happened kwa vijiji vya ujamaa? Mama Ntilie amezungumzia kijiji kingine kule Iringa, je hivi vijiji mbona havikuendelezwa? Kama hiki cha Butiama kingekuwa mfano mzuri na kingesaidia sana uzalishaji na ajira. Je, vimekufa kwa sababu ya uongozi mbovu au tangu Tanzania iachane na ujamaa serikali za Mwinyi na Mkapa kwa makusudi ziliamua kuviachia hivyo vijiji, hasa vile vilivyokuwa vimefanikiwa vife kimya kimya?

Wasu,heshima mbele.
Hii ya vijiji vya ujamaa bora ilivyokufa na kama ingewezekana hata visingewahi kuwepo.
Historia ni ndefu ya ujamaa hasa wa Nyerere tofauti kidogo na wa Karl Marx et al.Mimi siyo mjamaa na sijawahi kuupenda wala kuufikiria ila niwewahi ku-experience machungu yake.Hii ya kuanzisha vijiji vya ujamaa na kupunguza kasi ya maendeleo ya vijiji jirani ilinipa shida SANA.Hebu angalia maendeleo ya sasa ya vijijini collectively ukilinganisha na ya vijiji vya ujamaa.
 
Vijiji vya Ujamaa enzi hizo vingi tu vilimiliki malori, mabasi, matrekta, vinu vya kusaga nafaka, mashamba makubwa ya mazao, ng'ombe wa maziwa wa kisasa, maduka ya vijiji,....
Baada ya kuingia vitani na Idd Amin mwishoni mwa 1978, na hasa baada ya vita hiyo, tulianza kushuhudia uporomokaji wa KASI sana wa maendeleo haya kwa vijiji hivi pamoja na mashirika ya UMMA kufilisika kwa kasi ya ajabu.Hata hivyo uanzishwaji wa vijiji hivi umetusaidia wengi. Utanzania huu tunaojivunia sasa umechangiwa sana na vijiji hivi ikisaidiwa na mambo mengine kama JKT, lugha yetu ya Kiswahili, Uongozi wa Mwalimu na TANU/CCM ya enzi zake,...
Sio Butiama peke yake iliyokuwa imeendelea kiasi hicho. Na wala sio Butiama pekee ilyofilisika hivyo. UFISADI ulianzia VIJIJINI.
 
Jamani ukweli kausema Bibi Ntilie na Jasusi pia to some extent,ingawaje Jasusi the only correction i can make ni kuwa Joseph Nyerere alifariki 1994.
Wakati wa kifo chake alikuwa hana madaraka yeyote Butiama,na ilikuwa hivyo kwa miaka kadhaa.

Huyu Nyerere mdogo,alikwenda Butiama 1970 kwa maagizo ya kaka yake kukiendeleza kijiji.Ukiwauliza wanakijiji wa zamani pale,hata huyo baba yake Manyerere,watakwambia Joseph Nyerere wakati anakabidhiwa kijiji alikuta shs 100 tu.
He started from scratch.By early 80's,kile kijiji kilikuwa ni bora Tanzania nzima.Walikuwa na combine harvesters,hospitali kubwa tu,shule na vinginevyo kama ilivyotajwa na wengine huko nyuma.
Advantage aliyokuwa nayo Joseph,wakati huo pia alikuwa ni Member wa East African Legislative Council na pia kuna wakati alikuwa ni Mbunge wa Taifa.Kwa hio,ilikuwa ni rahisi kwake yeye kupeleka maendeleo kwao.Ikumbukwe kuwa alishawahi kuwa waziri mdogo wa utalii na pia mkuu wa mkoa wa Mwanza in the 60's.

Historia ya Mzee Joseph Nyerere ni ndefu sana ambayo inahitaji thread yake yenyewe.
Mwalimu hakuhusika na haya maendeleo na yeye mwenyewe alikiri yote haya siku ya mazishi ya marehemu mdogo wake.
Mwalimu alichangia sana kuwepo kwa kanisa kubwa pale kijijini na pia alimuomba Ghadafi kuwajengea msikiti waislamu wa Butiama,ambao idadi yao ilikuwa inaongezeka,pia wakajenga na guest house nzuri tu.
Leo hii Butiama kuna lami mpaka katikati.
 
Alivyosema Manyerere na Zanaki ni sahihi kabisa. Vitu hivyo vilikuwepo enzi za Mwalimu wakati akiwa Rais. Vilianza kulegalega baada ya Mwalimu kustaafu. Vingine vikafa kabisa kama karakana ya kijiji, matrekta, magari shamba la mifugo n.k. Lakini vile ambavyo vilipelekwa na instutions za serikali bado vipo mpaka leo na vinafanya kazi kama posta, hospitali, benki n.k.
Kwangu mimi sio rahisi kutamka kuhusu Mwalimu kuhodhi maendeleo lakini ninachokiona ni kuwa viongozi wa taasisi hizo za serikali kama posta, benki walikuwa wanapeleka huduma hizo ama kwa kujipendekeza au uamuzi wao kwa kuwa kile kiji kilikuwa ni eneo alilozaliwa Mkuu wa nchi wakati huo, na ambako alikuwa anaenda likizo mara kwa mara.
Tusisahau ule mradi mkubwa wa bomba la maji kutoka Mugango mpaka Butiama (Haukuwa na tofauti sana na ule wa sasa wa Wami mpaka Chalinze ingawa huu umetawanyika sana, kwa maana ya kupelekwa vijiji vingi).
Huduma hizi zilizopelekwa zilikuwa na hadhi ya Tarafa. Ingawa ukienda makao makuu ya Tarafa ya Nyanja yaliyoko kilometa 5 kutoka hapo Butiama hakuna huduma hata moja isipokuwa mahakama. Makao makuu ya tarafa yako kijiji cha Muriaza. Butiama ni sehemu ya Tarafa ya Nyanja.
 
Huyu Nyerere mdogo,alikwenda Butiama 1970...
He started from scratch...

Historia ya Mzee Joseph Nyerere ni ndefu sana ambayo inahitaji thread yake yenyewe.
Mwalimu hakuhusika na haya maendeleo na yeye mwenyewe alikiri yote haya siku ya mazishi ya marehemu mdogo wake.

Kwa hiyo hoja kwamba Mwalimu alihodhi maendeleo na kupeleka Butiama si kweli?
 
Kwa hiyo hoja kwamba Mwalimu alihodhi maendeleo na kupeleka Butiama si kweli?

Sio kweli. Vipo vijiji Nchi hii vilikuwa vinakizidi kijiji hiki kwa MAENDELEO. Mashindano yalikuwa yakifanyika kitaifa enzi hizo na sikumbuki Butiama kushika nafasi ya kwanza.
 
Nadhani turudi tusome vizuri hii makala, na pia tumwombe mwandishi aichapishe upya "with specific reference of the timeframe" wakati Butiama ilipo kuwa pepo ndogo...

Mwaka 1975-76 Mzazi wangu alikuwa vet office pale Musoma na we used to visit Butiama wakati akienda kuangalia mifungo ya Mwl, despite kwamba ni muda mrefu umepita hakuna kitu nilichokiona pale butihama kipo tofauti na VIJIJI vya wakati huo...
 
Mimi siijui Butiama wala sijawahi kuitembelea, ila inaelekewa watu hapa mnanunua maneno just because yanamchafua mwalimu.
watanzania siku hizi tuna ugonjwa huo sana, yani habari si habari hadi imchafue mtu fulani, na waandishi wanatuweza kwelikweli! si ndio kula yao?!
yani mtu unabishana na mtu anayesema amesoma tarime na anaifahamu butiama unaamua kukubaliana na article ambayo ukiichunguza haina logic ya kutosha just because kuna mtu kachafuliwa.
Inasikitisha!
 
Hilo sio tatizo, hapa JF hakiharibiki kitu. Ukweli husimama mwishoni.

.
 
Alivyosema Manyerere na Zanaki ni sahihi kabisa. Vitu hivyo ... Vilianza kulegalega baada ya Mwalimu kustaafu.

Zanaki kasema hivi: "Mwalimu hakuhusika na haya maendeleo na yeye mwenyewe alikiri yote haya siku ya mazishi ya marehemu mdogo wake."

Kwa hiyo, Congo, huwezi kusema unakubaliana na Zanaki halafu hapo hapo ukaanza kumpambapamba Nyerere kwa vitu ambavyo umeshakubali kwamba hakusika navyo! Tuache kuendelea kuji-brainwash kuhusu legacy ya Mwalimu!!!

Zanaki,

Inawezekana Nyerere siku ile alikuwa anasoma tanzia ya mdogo wake tu, ndio maana alimpambapamba huyu Joseph. Sijui Joseph Nyerere aliwezaje kufanya yote hayo wakati most of his post-govermnent life alikuwa mlevi machafuchafu mmoja pale Mwananyama A, Komakoma. Jiulize kwa nini Nyerere alim fire!!!
 
Jokakuu,
Aliyoandika Manyerere ni kweli kabisa.Ukweli huo umeungwa mkono wa wachangiaji wanaoijua Butiama barabara kama Ngereja na bibi Ntilie.Ngereje ameandika ya kweli zaidi na mimi nampa credit zaidi.Huyu MAGABE KIBITI ni wale wanakurupuka ili kuonyesha wanajua vitu kiasi gani wakati hawajui lolote.

Waoo poti mwenzangu naona umekuja na accusations za nguvu....

tuendelee...

Huku kutoroka shule kwa bwn Magabe kwenda Butiama mimi naweza kusema alikuwa anaishia kwenda kushangaa nyumba anayoishi Nyerere tu na kurudi.

Ramli zimeanza sasa kiasi kwamba sasa unajua nilichokuwa nakifanya huko butiama

kimsingi haijui butiama inayoongelewa na manyerere,bali anajua vipande vya ka-butiama tena ya miaka ya 90 tena naweza `kupinga kuwa hata huko kwenda butiama ilikuwa labda ni mara moja baada ya miaka 2 tena wanaenda kama darasa kutembelea nyumba ya Nyerere.

Ukipata sehemu yoyote hapa nimeandika kuwa naijua butiama ya Manyerere, naomba uionyeshe hapa poti

Usiogope mtu kuzaliwa Tarime na kusoma Mara sec ukafikiri anaijua butiama.La hasha.Sisi tulizaliwa Makutano lakini kuna kaka yangu hajawahi kufika Butiama.

Sidhani kama kuna aliyetisha watu hapa kwa sababu tu kazaliwa Tarime na kusomea Mara Sec (hey it is Mara boyz kwi kwi kwi). Nilikuwa najibu swali la Jokakuu aliyetaka kujua ninaijua butiama kwa capacity gani.

Ni kweli butiama ilikuwa na maendeleo kama hayo yaliyosemwa na Manyerere.Mimi binafsi huwa namlaumu Nyerere kwa kupendelea Butiama na kusahau baadhi ya sehemu za mkoa wa Mara ususani majita na Kibara.Kama hoja ni vijiji vya ujamaa haikuwa Butiama pekee.Nenda Mugango,murangi,Bukima au Namhula kijiji cha ujamaa kule Iramba-kibara utaona ni jinsi gani maendeleo ya mkoa huo yalielekezwa huku juu zaidi ya sehemu zingine.

Naona poti unataka kusahau kitu ambacho mimi nimekiuliza kwenye hii mada kuanzia mwanzo. Kama umesahau, swali langu la kwanza baada ya post ya jokakuu lilikuwa hili:

hii ni butiama ipi anayoongelea huyu?

Na kisha baada ya hapo, Jokakuu akafahamisha kuwa manyerere anaongelea Butiama ya wakati wa Mwalimu (miaka ya 70) huku akaniuliza mimi naongelea Butiama ipi na mimi nikajibu:

Ninaongelea Butiama ya miaka ya 90 ambayo sio tu haikuwa na vyote hivyo anavyosema Manyerere, haikuwa na magofu ya hivyo vyote anavyosema.

Kitu ambacho sasa kinatolewa sababu nyingi tu.

mimi nimezaliwa makutano nimekulia Buhare nimefanya kazi Majita A,Mwibagi,Mwigundu,Kutanu,Butiama,Utegi na sehemu zingine nyingi tuu.So naweza kusema kuwa Mwl alihodhi maendeleo na kupeleka Butiama tabia inayoendelezwa na mbunge mkono.Dawa ya kuondoa hii mentality ya kupendelewa huko juu kwa mkoa wa mara (hasa majita) ni kutengwa kwa jimbo la musoma vijijini ili sisi wajita tujitawale wenyewe na hawa wa huku juu nao waendelee na uchifu wao.

Huu ushauri wako wa kujitenga pia ni mzuri hasa ukichukulia kuwa umekaa sehemu zote hizo ulizotaja hapo juu lakini kumbuka kuwa umoja wa watu wa mara ni nguvu na utasaidia mkoa wetu zaidi ya utengano.
 
Mimi siijui Butiama wala sijawahi kuitembelea, ila inaelekewa watu hapa mnanunua maneno just because yanamchafua mwalimu.
watanzania siku hizi tuna ugonjwa huo sana, yani habari si habari hadi imchafue mtu fulani, na waandishi wanatuweza kwelikweli! si ndio kula yao?!
yani mtu unabishana na mtu anayesema amesoma tarime na anaifahamu butiama unaamua kukubaliana na article ambayo ukiichunguza haina logic ya kutosha just because kuna mtu kachafuliwa.
Inasikitisha!

Na wewe unaweza kuweka mawazo tofauti kwenye hoja inayojadiliwa badala ya kuweka vilio vingi kuwa watu hawakufanya kile ulichotaka wakifanye hapa. Au sio hivyo?
 
Zanaki,

Inawezekana Nyerere siku ile alikuwa anasoma tanzia ya mdogo wake tu, ndio maana alimpambapamba huyu Joseph. Sijui Joseph Nyerere aliwezaje kufanya yote hayo wakati most of his post-govermnent life alikuwa mlevi machafuchafu mmoja pale Mwananyama A, Komakoma. Jiulize kwa nini Nyerere alim fire!!!

Alimfire kutoka wapi? Hebu tuelimishe....siku hio ya mazishi hakusoma tanzia yake,aliyesoma ni Butiku,kwa hio unataka kusema alikuwa anawadanganya wazanaki palepale? Wewe unaijua historia hii inayoongelewa hapa?Nimeelezea hapo aliwezaje kuyafanya yote hayo.Hata kama alikuwa mlevi,lakini maendeleo ya Butiama ni juhudi zake binafsi.Hata leo wewe mwenyewe unaweza kwenda Butiama na utaambiwa maneno hayahaya.

Haabari ndio hio
 
Zanaki,

..Joseph Kizurira Burito Nyerere aliwahi kuwa Naibu Waziri, enzi hizo wakiita Waziri Mdogo, katika serikali ya Mwalimu Nyerere. nadhani ilikuwa miaka ya 60/70.

..sasa kwasababu Mwalimu alifanya mabadiliko ktk uongozi, na hakumrudisha Joseph ktk nafasi yake, ndiyo maana Kuhani anadai Joseph alikuwa "fired."

..labda kuna wachangiaji wanaoweza kutueleza sababu zilizomfanya Mwalimu Nyerere, amuondoe Joseph Nyerere ktk serikali yake.
 
Back
Top Bottom