Zanaki
..Joseph Kizurira Burito Nyerere aliwahi kuwa Naibu Waziri, enzi hizo wakiita Waziri Mdogo, katika serikali ya Mwalimu Nyerere. nadhani ilikuwa miaka ya 60/70.
..sasa kwasababu Mwalimu alifanya mabadiliko ktk uongozi, na hakumrudisha Joseph ktk nafasi yake, ndiyo maana Kuhani anadai Joseph alikuwa "fired."
Daaaaah, huwa akitokea mtu mmoja akanielewa huwa nafurahi sana. Ha haa haaaa
Ni hivi: Katika mabadiliko yaliyopita ya baraza la Mawaziri la Kikwete, wakina Mramba, Juma Mwapachu, Juma Ngasongwa, Margaret Sitta, Zakia Meghji, Diallo, wote hawa walikuwa fired!!!
Ambao hawakuwa fired japo hawakurudishwa ni wawili tu, Kingunge Mwiru na Joseph Mungai, ambao Rais alisema wameomba kupumzika. Kwa nini unadhani Rais ali take the trouble kueleza kwa nini kuna watu wawili hakuwarudisha ? Maana yake ni kwamba alitaka ijulikane ni hawa wawili tu ndio hawakuwa fired!!!
Ndio maana nimesema Nyerere alim fire mdogo wake kwenye baraza la Mawaziri. Na mimi sijawahi kuuliza ni kwa nini alim fire kwa sababu alikuja kuwa wino mmoja ( mlevi wa kuokotwa okotwa) wa matapu tapu Mwananyamala Komakoma alikoishi miaka yake ya post-government life. Joka Kuu, ahsante kwa kunielewa.
Zanaki,
Unanishangaza kujiweka kama hujui maana ya Waziri kuwa fired. Halafu unasema Butiku ndio alisoma Tanzia ya Joseph Nyerere kwa hiyo historia yangu ni mbovu. Lakini kumbuka mwanzo umesema hivi: "Mwalimu hakuhusika na haya maendeleo na yeye mwenyewe alikiri yote haya siku ya mazishi ya marehemu mdogo wake."
Kwa maana hiyo unatuambia Julius aliongea siku ya msiba wa Joseph, akamsifia mdogo wake kwa kuleta hayo maendeleo. Ndio hiyo nasema "tanzia," yani kutoa wasifu wa marehemu! Hata kama Butiku alisoma Tanzia, hata Nyerere nae anaweza kusemwa alitoa tanzia hata kama hakuwa ana kikaratasi mkononi.
Nyerere alim fire Joseph Nyerere kwenye Uwaziri.