Je, Mwalimu alihodhi maendeleo na kupeleka Butiama??


Naona mada yako inazidi kupanuka sana, kinachoongelewa sasa hapa ni zaidi ya ulichoweka kwenye heading ya hii thread. Je uko tayari kusema kwa wazi zaidi unachotaka kiwe main issue ya huu mjadala?
 
Huyu Manyerere Jacton kesha toka Mtanzania alipokuwa mhariri?Mwenye nyeti atupe.Maana kama kaandika makala Raia mwema inawezekana kesha mwaga manyanga.Huyu jamaa alitumika sana kuwasaidia Rostam na Edward.Habari kama vile Lowasa apokelewa na magari zaidi ya mia 300 monduli.Watu wa Raia mwema wakimuacha ataanza kuandika makala za kuwasifia watu wake.Toeni nyeti huyu mtu bado yuko Habari Corp?
 
Magabe Kibiti said:
Naona mada yako inazidi kupanuka sana, kinachoongelewa sasa hapa ni zaidi ya ulichoweka kwenye heading ya hii thread. Je uko tayari kusema kwa wazi zaidi unachotaka kiwe main issue ya huu mjadala?

Magabe,

..haiwezekani kuthibiti na kulazimisha mwelekeo wa mjadala ktk mazingira kama ya jamii forums.

..mchangiaji wa kwanza kuleta jina la Joseph Kizurira Nyerere ni Bibi Ntilie. Kuhani na Zanaki wameongezea tu.

..lakini sidhani kama kuna ubaya wowote ule wa kumjua zaidi Joseph Nyerere. huyu ni kati ya waasisi wa Umoja wa Vijana wa Tanu.

..binafsi naiamini sana jamii forums. hili ni jungu kuu kwelikweli. at the end of the day ukweli hujulikana.
 

Daaaaah, huwa akitokea mtu mmoja akanielewa huwa nafurahi sana. Ha haa haaaa

Ni hivi: Katika mabadiliko yaliyopita ya baraza la Mawaziri la Kikwete, wakina Mramba, Juma Mwapachu, Juma Ngasongwa, Margaret Sitta, Zakia Meghji, Diallo, wote hawa walikuwa fired!!!

Ambao hawakuwa fired japo hawakurudishwa ni wawili tu, Kingunge Mwiru na Joseph Mungai, ambao Rais alisema wameomba kupumzika. Kwa nini unadhani Rais ali take the trouble kueleza kwa nini kuna watu wawili hakuwarudisha ? Maana yake ni kwamba alitaka ijulikane ni hawa wawili tu ndio hawakuwa fired!!!

Ndio maana nimesema Nyerere alim fire mdogo wake kwenye baraza la Mawaziri. Na mimi sijawahi kuuliza ni kwa nini alim fire kwa sababu alikuja kuwa wino mmoja ( mlevi wa kuokotwa okotwa) wa matapu tapu Mwananyamala Komakoma alikoishi miaka yake ya post-government life. Joka Kuu, ahsante kwa kunielewa.

Zanaki,

Unanishangaza kujiweka kama hujui maana ya Waziri kuwa fired. Halafu unasema Butiku ndio alisoma Tanzia ya Joseph Nyerere kwa hiyo historia yangu ni mbovu. Lakini kumbuka mwanzo umesema hivi: "Mwalimu hakuhusika na haya maendeleo na yeye mwenyewe alikiri yote haya siku ya mazishi ya marehemu mdogo wake."

Kwa maana hiyo unatuambia Julius aliongea siku ya msiba wa Joseph, akamsifia mdogo wake kwa kuleta hayo maendeleo. Ndio hiyo nasema "tanzia," yani kutoa wasifu wa marehemu! Hata kama Butiku alisoma Tanzia, hata Nyerere nae anaweza kusemwa alitoa tanzia hata kama hakuwa ana kikaratasi mkononi.

Nyerere alim fire Joseph Nyerere kwenye Uwaziri.
 
Kuhani,
Sawa kama unavyosema, Nyerere alim"fire" mdogo wake kwenye uwaziri. Sababu hata mimi sizijui kama vile mpaka leo sielewi ni kwa nini alim"fire" Babu kwenye uwaziri kama tulivyojadilia kule kwenye thread ya Babu. If you have any inside information it would be nice to hear it. Mimi hapa naapa sijui na hata wakati huo I was too young to ask. But if you have any info please share it with us.
 

Haya ni maneno ya wanaotaka kumchafua Marehemu badala ya kumuacha apumzike katika pumziko lake la milele kwa amani. Nimefika seheni nyingi sana Tanzania wakati Mwalimu akiwa madarakani na Butiama ikiwa ni mojawapo. Kuna sehemu nyingine nyingi tu zilikuwa na maendeleo makubwa ukilinganisha na Butiama.

Nyerere kama tunamvyomfahamu Watanzania wengi hakuwa na ubaguzi au upendeleo wa namna hiyo i.e kuhakikisha maendeleo yote yanapelekwa Butiama kwanza kabla ya mahali pengine popote pale Tanzania. Kama ingekuwa hivyo basi Butiama ingekuwa inafanana na ile miji mikali sana katika nchi za Ulaya au Amerika.
 

Bubu Ataka Kusema,

"Muache apumzike" maana yake nini, tusimseme vibaya, au tusimjadili kabisa, au tuongelee mazuri yake ?
 
i agree with you. maendeleo gani butiama? no running water ( kulikuwa na mradi wa mkono kwa mkono kupeleka maji butiama, shule ya msingi butiama hoi kama zingine, kituo cha afya taabani kama vingine, hali ya umasikini kama vijiji vingine tanzania! indeed there was nothing exeptional about butiama. hata makumbusho ya mwalimu nyerere yalikuwa yanasikitisha. poorly maintained! poorly marketed! only last week nilikuwa arkansas kutembelea clinton presidential library...now thats a way to be remembered!

bottomline: butiama was no Gbadolite!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…