Watu wengi hasa vijana waliofiksha muda wa kuoa au kuolewa wengi wanatamani sana maisha ya kuwa na wenza wa maisha yao. Harusi nyingi huandaliwa kwa gharama kubwa kiasi ambacho kwa mtu ambaye huna kitu unaweza kuogopa kutangazia umma kuwa unampango wa kuoa.
Mara kadhaa nimesikia viongozi wa dini wakilalama kuwa wale waliowafungisha ndoa siku chache zilizopita wamefika ofisini kutaka ndoa yao ivunjwe au zimeshavunjika. Unaweza kujiuliza na kukosoa watu hawa ukizingatia gharama zilizotumika kuziandaa ndoa hizo kwa maana ya sherehe n.k. Suala la kuoa au kuolewa linahitaji uangalifu mkubwa mpaka Kufikia hatua ya kumteua na kumtangaza kuwa huyu ndiyo mtarajiwa wakweli. Kwa mwanamme ambaye anataka kuoa mke ni lazima ajiridhishe kuwa anapendwa kwa dhanti na mchumba wake huyo. Vijana wengi wamekuwa wakilazimisha wapendwe na wasichana kwa kuwapa ofa na zawadi mbalimbali hadi kuwalainisha na kutimiza haja zao, wengi wanaofanya hivyo hawana muda wa kujiuliza swali hili kuwa wasichana hao wanawapenda kwa dhati ya moyo wao? Au wamekubali tu kwa zawadi alizotoa? Athari za mwanaume kulazimisha mahusiano hadi kufikia hatua ya ndoa huwagharimu wengi kwani ndoa za aina hiyo haziishi misukosuko na kusalitiana.
Wanaume wengi nimewasikia mitaani wanasema yule binti ananipenda kweli lakini sinampango naye kwangu mimi hawa wanachezea bahati maana ni nadra na ni bahati ya kipekee unapojikuta msichana ndiye anayekupenda, wasichana/wanawake wengi hulazimishwa kupenda maana wengi hawana uwezo au niseme sio utamaduni kumtamkia kijana wa kiume kuwa anampenda. Hivyo basi ili kijana ufikie hatua ya kutamka kuwa unataka kuoa lazima ujiridhishe kuwa huyo unayemuoa anakupenda kwa upendo wa dhati pengine zaidi yaw ewe unavyompenda. Kinyume chake usije ukashangaa usaliti ukiinuka maana aliyemuyoni mwake sio wewe!!! hivyo usijaribu kuoa binti ambaye hakupendi kwa maana ya kuwa wewe ndiye uliyemlazimisha kwa vishawishi kadha wakadha. (ushauri huu unawahusu vijana wa kiume wanaotaka kuoa)