Je, Mwanasiasa anayepatia Kiingereza cha Kuandikiwa tu ila Kuongea anaogopa na Yule anayekichapia ila haogopi Kukiongea nani ni Bora?

Je, Mwanasiasa anayepatia Kiingereza cha Kuandikiwa tu ila Kuongea anaogopa na Yule anayekichapia ila haogopi Kukiongea nani ni Bora?

wakuandikiwa bora maana anajitambua kuwa hajui lugha na kukubali kupewa mwongozo na kulinda image yake kwa public!
Nani amekuambia ukiongea lugha ya kigeni kwa kuikosea unaharibu image yako. Ni mjinga pekee anayeamini ubora wa mtu upo katika kuzungumza lugha ya kigeni kwa ufasaha.
 
Putin wala habongi kingereza akiwa anatoa matamko yake mubashara anaongea kirusi na anaeleweka na haohao waingereza na Americans na viingereza vyao
Ushawaona raia wake wanavipata shida wakiwa nnje ya Urusi??? Wewe toka hapo nenda Zimbabwe au South tu utaujuwa umuhimu wa Kingereza
 
Wenye elimu ndogo ndio wenye uthubutu wa kuongea kiingereza bila hofu ya kuchekwa
 
Majibu yenu Great Thinkers ni Muhimu.
Kiingereza kinasaidia nini?Mbona Japan,Uchina,Urusi,Korea ,Italy,Ufaransa,hawajui kiingereza na ni matajiri Sana.Sisi tunang'ang'ania kiingereza na ni masikini.Ukoloni umeacha Siri kubwa Sana hapa Africa.
 
Bora anaeongea vibaya anaboronga ili mradi anaeleweka!!! mara mia!!! kuliko anae andika sahihi saa ngapi mtu aka kusome weee atafute miwani ilipo ina huuu!! sababu asiye ongea vizuri watu watajua siyo lugha yake!!........

Mbona wahindi hawajui kuongea vizuri kiswahili na wamezliwa humu humu!!!...na wanauza!...asa uniandikie weee na mie nataka mbuzi wa supu faster...ntakuelewa kweli....lkn km ukiniuliza ...''ako taka puji nono papa??!!!...ndiyo! ''' hayaa rete mbesa ako dugu!

tunamaliza faster!!!
 
Jamani tusidanganyane.Watanzania wengi hatuko huru kuongea kingereza hasa hasa tuliofundishwa miaka saba kwa kiswahili na miaka minne kwa Kingereza
Julius Kambarage Nyerere hakuna alipokutana na Kiswahili katika soma soma yake.Hivyo alikuwa anaweza kujieleza vizuri Kwa Kingereza.Kitendo cha kubadilisha kiswahili kama rugha ya kufundishia imefanya wasomi wengi kuwa dhaifu kujieleza kwa kutumia kingereza
Kiswahili lugha yetu,hatukijui,watafuta kiingereza,umeandika RUGHA,ndio nini.Mimi na wewe hatuchekani kwenye kiswahili.Andika LUGHA sio RUGHA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnapima ubora wa rais kwa kuongea Kiingereza?
Mshamsikia Putin anaongea Kiingereza?
😊😊😊
 
Mbona wasomi wa zamani walikuwa wanajua kiigereza vizuri tu hata kama kaishia darasa la nne. Yule jamaa wa PhD yeye ilikuwaje mpaka level ile lakini hajui kiingereza wala kiswahili. Ndiyo maana watu wanamashaka na elimu yake pamoja na uraia wake. Alianza kudai yeye ni Muhaya ila huko hakutoboa akahamia kwa wasukuma.
Wasomi wazamani walifundishwa na wenye lugha yao, na pengine hata mtaani waliitumia ili kuwasiliana nao.
 
Back
Top Bottom