Je, mwanaume anaweza kumbaka mke wake wa ndoa?

Je, mwanaume anaweza kumbaka mke wake wa ndoa?

Sheria inayotumika ni hii hii ya kawaida ya kubakana ila tatizo kwetu sisi ni mwanamke gani yupo tayari kwenda kusimama kizimbani kumshitaki mumewe kambaka?

Ila watafiti wanasema wanawake waliomo kwenye ndoa wengi wanabakwa na waume zao!!

Kwa mfano mwanaume katoka huko na mipombe yake saa saba za usiku kakuta mkewe kalala then kamkurupua usingizini bila hata ya kumuandaa anaanza kulazimisha tendo........huo ndiyo ubakaji ndani ya ndoa brooo!!! Kwa sababu tendo la ndoa ni maandalizi ndugu yangu!!

Ukimfanyia hivyo mkeo, akaenda polisi kutoa maelezo akapewa PF3 na kwenda hospital na daktari akaconfirm kwamba kweli anamichubuko inayotokana na kulazimishwa tendo la ndoa na akakusimamisha kizimbani umembaka!!! Loh!! Unakwenda jela miaka yako kadhaa kama wabakaji wa kawaida tu!!
 
Tunabakwa kila siku na hatusemi (naomba mungu my huby asisome hapa BE)

Inaelekea jamaa yako huwa anakubaka! "Ee Mungu lisikie ombi la dena Amsi kuwa jamaa yake asome hii thread ili aache kumbaka'' usijali nimekuombea na hatakubaka tenaaaa!
 
Ipo mme kumbaka mke hasa pale anapoforce (ite illocutive/perlocutive/loctive)
ila kwa bongo sidhani kama inafanya kazi niliwahì kusikia wakiijadili redio 1 mwaka jana ndipo nilipofahamu kuna mume kumbaka mke.
 
mhh! kwa tanzania bwana hii haipo. Kama tutachukulia wikipedia kama source ya information, Tanzania inatambua marital rape pale mume na mke wanapokuwa wametengana.<br />
<a href="Marital rape - Wikipedia" target="_blank">Marital rape - Wikipedia, the free encyclopedia</a><br />
next time Dena mpe tu kwa raha zenu....
Chapakazi acha uchokozi basi bana
 
Hii ya mume kumbaka mkewe ipo ndugu zangu, wala msimshangae mtoa mada. Japokuwa hajajieleza vizuri. Ila mambo haya yapo. HERI WENYE NDOA SAFI.
 
Nafikiri mume kubaka ni pale anapolazimisha tendo wakati mke hayupo tayari
 
  • Thanks
Reactions: rom
Nafikiri mume kubaka ni pale anapolazimisha tendo wakati mke hayupo tayari

Mke anaweza kumbaka mume? Hapo inakuwaje? Mke anawezaje kumlazimisha mume tendo wakati nanihii lazima isimame kwa tendo kutendeka? au rape inatokea kwa jinsia moja tu?
 
Hakuna cha kubakwa ukishakubali kuolewa wewe timiza yanayokupasa basi. Sasa mimi nimekuoa kwa utaratibu
mzuri kwanini mambo fulani ujifanye unajua kubania
 
Wachangiaji wengi wameonyesha kwa ubakwaji kwa akina mama ktk ndoa upo. Lakini hakuna aliyenifafanulia iwapo na mume anaweza kubakwa na mke katika ndoa au la! Na vipi sheria inasema nini kuhusu hili? Au inawapendelea akina mama peke yao? Je mwanaume akibakwa na yeye niende polisi kupata PF3 aende kwa daktari?
 
Wachangiaji wengi wameonyesha kwa ubakwaji kwa akina mama ktk ndoa upo. Lakini hakuna aliyenifafanulia iwapo na mume anaweza kubakwa na mke katika ndoa au la! Na vipi sheria inasema nini kuhusu hili? Au inawapendelea akina mama peke yao? Je mwanaume akibakwa na yeye niende polisi kupata PF3 aende kwa daktari?

Definition ya kubaka ni nini? Kwa kawaidi ni non-consensual sex! Sasa mwanaume ukidinda ijapokuwa ni involuntary, mara nyingi huwezi sema hapana. Ndio maana ni rahisi kwa mwanamke kupata ngono zaidi ya mwanaume. Na ndio maana biashara ya uchangudoa inashamiri na the oldest profession.

Katika cases nyingi za ubakaji wa mwanaume by mwanamke huwa ni kwa watoto. Kwa mfano mwalimu mwanamke na mwanafunzi mdogo mwanaume!
 
hakuna cha kubakwa ukishakubali kuolewa we timiza yanayokupasa basi. sasa mimi nimekuoa kwa utaribu
mzuri kwanini mambo fulani ujifanye unajua kubania

???
Mtu anapokubali kuoa/olewa, anakubali kuishi na mke/mume wake na kuwa mpenzi wake mpaka kifo kiwatenganishe. Hakubali kuwa sex object wake tu na kutimiza tamaa yake kila atakapo.
 
Wachangiaji wengi wameonyesha kwa ubakwaji kwa akina mama ktk ndoa upo. Lakini hakuna aliyenifafanulia iwapo na mume anaweza kubakwa na mke katika ndoa au la! Na vipi sheria inasema nini kuhusu hili? Au inawapendelea akina mama peke yao? Je mwanaume akibakwa na yeye niende polisi kupata PF3 aende kwa daktari?

Kulingana na sheria ya Tanzania, mwanaume hawezi kubakwa kamwe (whether married or not). Nilifanya utafiti nikapata taarifa hii:

'(1) It is an offence for a male person to rape a girl or a woman.

A male person commits the offence of rape if he has sexual intercourse with a girl or a woman under circumstances falling under any of the following descriptions:
not being his wife, or being his wife who is separated from him without her consenting to it at the time of the sexual intercourse.
with her consent when the consent has been obtained by the use of force, threats or intimidation or by putting her in fear of death or of hurt or while she is in unlawful detention.


Mume anaruhusiwa kumbaka mke wake unless she's separated from him also.
 
Kama hamko tayari ku-do bnafsi nawashauri msiolewe... hizi sheria zinaletwa na maradical feminists ambao kwao ndoa ni kama biashara, kuna mambo ya xploitation,n.k

Sasa haya mambo yanaletwa kwetu na sie kama kasuku maana kila kinacholetwa kwetu ni kizuri,cha ajabu sie hatuko tayari kuwakosoa kwa ya kwao ili nao wayachukie ya kwao na waige ya kwetu(utumwa wa kimtazamo)

Mwaka juzi niliwahi kusikia TAWLA wakiongea juu ya hii mada na wakaulizwa kama inatokea mme anafanya hvyo wao wanapendekeza nn?wakasema mme afungwe,kwa mda gani?hata miaka5,nilijiuliza maswali yafuatayo:

Je,ni kweli hajawahi kukubaka mpaka leo mna miaka10 kwenye ndoa?Je,unahisi nini mme akifungwa na akarudi kweli mtaweza kuishi kama zamani?Je,utakuwa ukiwaambiaje wanao juu ya kufungwa kwa baba yao?Je,siku moja wakijua wewe ndo umemfunga baba yao unahisi watakaa wakupende wewe?Je,mme akirudi si ndo mzungu wa nne,na si ndo kuruhusu ndoa nyingne nje ya ndoa?

Unajua wanasheria hawasomi saikolojia na sosiolojia na ndio maana hawawezi kujua uhusiano wa sheria hizi kwenye jamii za kiafrika na tofauti ya mazingira na tamaduni kati ya Ulaya Vs Afrika.

Tusipokuwa makini na UKIMWI wetu huu tutaleta maafa badala ya kuondoa matatizo
 
  • Thanks
Reactions: rom
Kama hamko tayari ku-do bnafsi nawashauri msiolewe...hizi sheria zinaletwa na maradical feminists ambao kwao ndoa ni kama biashara,kuna mambo ya xploitation,n.k

sasa haya mambo yanaletwa kwetu na sie kama kasuku maana kila kinacholetwa kwetu ni kizuri,cha ajabu sie hatuko tayari kuwakosoa kwa ya kwao ili nao wayachukie ya kwao na waige ya kwetu(utumwa wa kimtazamo)

mwaka juzi niliwahi kusikia TAWLA wakiongea juu ya hii mada na wakaulizwa kama inatokea mme anafanya hvyo wao wanapendekeza nn?wakasema mme afungwe,kwa mda gani?hata miaka5,nilijiuliza maswali yafuatayo:

Je,ni kweli hajawahi kukubaka mpaka leo mna miaka10 kwenye ndoa?Je,unahisi nini mme akifungwa na akarudi kweli mtaweza kuishi kama zamani?Je,utakuwa ukiwaambiaje wanao juu ya kufungwa kwa baba yao?Je,siku moja wakijua wewe ndo umemfunga baba yao unahisi watakaa wakupende wewe?Je,mme akirudi si ndo mzungu wa nne,na si ndo kuruhusu ndoa nyingne nje ya ndoa?

Unajua wanasheria hawasomi saikolojia na sosiolojia na ndo maana hawawezi kujua uhusiano wa sheria hizi kwenye jamii za kiafrika na tofauti ya mazingira na tamaduni kati ya ulayaVsafrika.

Tusipokuwa makini na UKIMWI wetu huu tutaleta maafa badala ya kuondoa matatizo

Hapo kwenye bold: would you truly find this hard to believe? Sheria hii hailetwi na (radical) feminists tu, inaletwa na wanawake watakao kuwa na umiliki wote juu ya mwili wao. Binafsi partner yangu angenibaka kwa mara kadhaa, singetaka kuishi naye tena. Ubakaji repetitive wa mke wake ni ishara ya ubinafsi kubwa na mume kuwa na ukosefu wa empathy for his wife. Ungetaka kuwa na partner asiyekuheshimu na kupuuza maoni/mahitaji yake ili atimize matakwa yake tu?

Pale ambapo watoto wangegundua kuwa mimi ndimi aliyemfungisha baba wake, ningewaeleza tu kwa nini niliamua kufanya nilichofanya. Kama nimewapatia malezi bora na kuwafunza maadili mema wangeelewa kuwa aliyofanya baba yao ni tendo baya sana.

Hakuna haja ya kusoma saikolojia kujua kuwa kuhalilisha kwa ubakaji kwenye ndoa nayo yaweza kuharibu uhusiano kati ya mke na mume na kuwafanya wanawake wengi walazimishwe kuvumilia ukiukaji wa intimacy yao bila kuwa na uwezo wa kufanya chochote. Rapists are criminals in the eyes of the law, so why is it suddenly different when the rapist happens to be married to his victim?

Naelewa kwamba wanawake wote hawakubali nami, wapo wanawake ambao wangesamehe mume wao kila mara, wanawake wasiohisi kama ubakaji is a big deal, au wanawake ambao wangebaki na mume wake kwa ajili ya watoto. Lakini, at least, ubakaji ungeharamishwa, wanawake hao bado wangekuwa na choice ya kuwalaani mume wao kwa kosa aliyotenda au la.
 
Nimesoma gazeti la nipashe la tar9.7.2011,...

Kwamba utafiti ulio fanyika unaonesha "wanawake wengi hubakwa na waume zao",....

Hii imenistua kidogo, wanabakwa vipi na waume zao?
Kubaka ni nini,... yaani ni ipi definition ya kubaka?

Kama inatokea mme anambaka mke wake... inawezekana pia mke akambaka mme wake?

So, kisheria mtu anaweza kufungwa ile miaka mingapi sijui kwa
kumbaka mke wake?

Nini solution ya tatizo hilo?

Mimi bado mdogo, nifumbueni macho hayo yote hayajaelezewa kwenye gazeti hili.
 
Tulishaliongelea hili...fukunyua post za nyuma utapata majibu yako!!
 
Tulishaliongelea hili...fukunyua post za nyuma utapata majibu yako!!

Ingekua hivo basi hata UKIMWI usingekua unaongelewa leo,...
Au hili gazeti lisingetoa habari hii leo
Nimejitahidi kutafuta kabla ya kuanzisha hii,... nipe link
 
Back
Top Bottom