Je, Mwenyekiti mpya BAVICHA, Wakili Deogratius Mahinyila ni nani?

Je, Mwenyekiti mpya BAVICHA, Wakili Deogratius Mahinyila ni nani?

Katika umri mdogo huyU wakili msomi ameshapitishwa katika tanuru la moto la siasa za kiuonevu zinazoendeshwa na ccm kwa kutumia dola. Natumaini amekomaa vya kutosha kushinda vishawishi na kuiongoza vyema BAVICHA katika kipindi hiki kigumu cha kiuongozi CHADEMA
InshaAllah
 
Wengine tulishauri na kuonya, mwamba pumzika kulinda legacy...
Lakini wapambe maslahi waliziba masikio!

1736880325859.png
1736881395334.png

Sasa tusubiri 21/1/2025!​
 
14 Januari 2024

Wakili wa Mahakama Kuu achaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa BAVICHA Chadema leo 14.01.25.​

Je Wakili msomi Deogratius Mahinyila ni nani ?​

View attachment 3201927
Picha maktaba : Deogratius Mahinyila

Wakili wa mahakama kuu ya Tanganyika Deogratius Mahinyila leo ametangazwa kuwa mwenyekiti mpya wa taifa wa Baraza la Vijana wa CHADEMA yaani BAVICHA kufuatia uchaguzi mkuu wa baraza la vijana wa CHADEMA uliofanyika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam


Wakili Deogratius Mahinyila ni mhitimu wa chuo kikuu University of Dar es Salaam (UDSM) degree LLB na amepita shule ya Sheria na kusajiliwa pia kuthibitishwa kutumika na wateja wa huduma za kisheria na utetezi kama wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania

Wakili Deogratius Mahinyila anarithi mikoba ya mwalimu John Pambalu ambao muda wake wa uongozi kama mwenyekiti wa BAVICHA taifa umekwisha

Wakili Deogratius Mahinyila amepitia mengi ambayo wanasiasa wa upinzani hutegemea kuyapitia katika siasa za Tanzania ambazo zimetawali kwa wivu uliopitiliza na chama dola kongwe CCM kinachofanya kila kiwezekanavyo kubaki madarakani hata kwa mbinu zisizo za kidemokrasia, utawala bora na mikakati mingine haramu ambayo kisheria haikubaliki kwa kufuatana na katiba ya nchi tuliyo nayo..


TOKA MAKTABA PIA MAPITO YA KIONGOZI MPYA WA BAVICHA

09 May 2021

Wakili Deogratious Mahinyila Toka kugombea udiwani mpaka kesi ya uhujumu uchumi


View: https://m.youtube.com/watch?v=w8DGtcdh9qc

Toka kugombea udiwani mpaka kesi ya uhujumu uchumi


The Chanzo imefanya mahojiano na mwanasheria Deogratias Mahinyila, aliyekuwa mgombea udiwani kupitia CHADEMA kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 katika kata ya Berege iliyopo wilaya ya Mpwapwa mkoa wa Dodoma nchini Tanzania.

Wakili Deogratius Mahinyila ambaye ni kijana aliyehitimu masomo yake mwaka 2019 Chuo kikuu cha Dar es salaam UDSM na kuamua kwenda kugombea udiwani kipindi cha uchaguzi mkuu wa 2020, ameongea mengi kuhusiana na dosari zilizojitokeza wakati wa uchaguzi pamoja na mashitaka yanayo mkabili hivi sasa kutokana na mchakato mzima wa uchaguzi.

Pia ameeleza kuhusiana na mwenendo mzima wa mfumo wa utoaji haki nchini Tanzania hususani mfumo wa haki jinai unavyoumiza watu kupitia sheria zinazozuia dhamana kwa baadhi ya makosa na namna watu wanavyotumikia adhabu kinyume cha sheria kwa mtindo ambao umekuwa maarufu kama 'kifungo kidogo...


27 March 2023 kijijini Berege Mpwapwa Tanzania, wakili Deo Mahinyila akihutubia

View: https://m.youtube.com/watch?v=NialNYvMdGY


15 November 2024

UCHAGUZI WA TAMISEMI 2024

Wakili Wakili Deogratius Mahinyila siyo mgeni katika shughuli za kisiasa kuanzia kuwania nafasi ya ngazi ya uenyekiti wa kijiji ...


View: https://m.youtube.com/watch?v=lNFmK3fqPCU&pp=ygUYV2FraWxpIE1haGlueWlsYSBtcHdhcHdh

Uongozi Chadema Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wameonyesha kutoridhishwa na majibu ya rufaa za wagombea wao kutoka kamati ya rufaa,juu ya wagombea walioenguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa.Hayo yamejiri leo Novemba 15, 2024 wakati Wakili Deogratius Mahinyila ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) Mkoa wa Dodoma alipokuwa akieleza kusikitishwa kwake na maamuzi hayo mbele ya ofisi ya mKuu wa wilaya.

13 Januari 2025

Wakili Deogratias Mahinyila mgombea BAVICHA alivyojinadi na kubanwa Maswali na Wajumbe



View: https://m.youtube.com/watch?v=6K2_wOxbIgs


Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA BAVICHA wakati wa Mkutano Mkuu ambao katika mkutano huu ndiyo walipata nafasi ya kuwauliza maswali kuelekea uchaguzi wa viongozi wakuu wa baraza hilo BAVICHA ambao umefanyika jiji Dar es Salaam katika ukumbi wa Ubungo Plaza.

Tunahitaji vijana wengi kama hawa.
 
Chama changu CCM kwa nini mnatelekeza vijana potential kama hawa wanaenda kuangukia mikononi mwa maadui zetu?

Huyu wakili ni ngumu sana, amepitia mengi lakini hakukengeuka.
1736884756669.jpeg

Picha maktaba: Wakili Deo Mahinyila akiwa na Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu


Inaonesha sasa hamahama imeishia kwa mjomba mchungaji Peter Msigwa.
 
Ulivyotaja tu mahakama kuu ya Tanganyika nimeacha kusoma,

Wapo wengi waliopata kibali cha Jaji Mkuu kuhudumu kisheria katika Mahakama Kuu ya Tanganyika


Prof. P.L.O. Lumumba​


Prof. PLO Lumumba is a Professor of Public Law, a holder of an LL.D (Doctor of Laws) on the Law of the Sea from the University of Ghent, Belgium, Master of Laws degree and Bachelor of Laws degree from the University of Nairobi.

Prof PLO Lumumba holds an honorary Degree of Doctor of Letters (D.Litt.) (Honoris Causa) from the University of Cape Coast in Ghana. He is also a holder of the Degree of Doctor of Science (DSc) (Honoris Causa) from Bells University of Technology in Nigeria. He has been trained on Humans Rights at the Institute of Advanced Legal Studies University of London in England, Humanitarian Law at the Raoul Wallenberg Institute of the University of Lund in Sweden and on International Humanitarian Law in Geneva, Switzerland.

He is an Advocate of the High Courts of Kenya and Tanganyika and a Certified Mediator
 
Wapo wengi waliopata kibali cha Jaji Mkuu kuhudumu kisheria katika Mahakama Kuu ya Tanganyika


Prof. P.L.O. Lumumba​


Prof. PLO Lumumba is a Professor of Public Law, a holder of an LL.D (Doctor of Laws) on the Law of the Sea from the University of Ghent, Belgium, Master of Laws degree and Bachelor of Laws degree from the University of Nairobi.

Prof PLO Lumumba holds an honorary Degree of Doctor of Letters (D.Litt.) (Honoris Causa) from the University of Cape Coast in Ghana. He is also a holder of the Degree of Doctor of Science (DSc) (Honoris Causa) from Bells University of Technology in Nigeria. He has been trained on Humans Rights at the Institute of Advanced Legal Studies University of London in England, Humanitarian Law at the Raoul Wallenberg Institute of the University of Lund in Sweden and on International Humanitarian Law in Geneva, Switzerland.

He is an Advocate of the High Courts of Kenya and Tanganyika and a Certified Mediator
Mpe elimu huyo Mbumbumbu
 
UDSM hakuwai toa viraza , kama ujapitia Udsm jua hu kilaza
Ukioana mtu anaandika viRaza kisha kiLaza basi jua nae ni mmojawao.

Yani hujui hapo utumie R au L means shuleni ulienda kukukua, sio kusoma.
 
Back
Top Bottom