Je, nani anapokea mahari kwa binti aliyelelewa na mama pekee?

Je, nani anapokea mahari kwa binti aliyelelewa na mama pekee?

Kama baba mzazi hayupo lazima upande wa baba awape mtu yaan shangazi au baba mdogo na mkubwa. Haiwezekani ukoo mzima wa baba hakuna mtu wa kuwakilisha.
Mkuu, unaenda mbele halafu unarudi nyuma.. mwanzoni umesema kuwa kwa upanda wa Baba yake hakuna anayemfaham hata mmoja, halafu hapa unasema lazima wawepo, watakuwepoje wakati hawafahamiani!?? Au unataka sisi tukakusaidie kuwatafuta ndugu zake!??
Maana majibu tayari unayo.

Kama kuna uwezekano wa kuwatafuta hao ndugu zake, basi watafutwe, kama hakuna uwezekano basi mama yake na wajomba wapokee mahari
 
Tatizo unachukulia rahisi sana labda uelewa wako ni mdogo kuhusu jambo hili.
Hivi unadhani ni kwanini ukoo wa upande wa pili unapaswa kushiriki kwenye mahari?
Achana nao hao, hawajui mila, ulizia zaidi kwa wakubwa mahari sio jambo dogo la mzaha, usukumani inapotokea hivyo upande wa kiume hupokea mahari na hugawanywa kwa makaka wa dada
 
Huyu binti kalelewa na mama yake pekee yake. Baba yake yupo hajafa ila binti hajawahi kukutana ana kwa ana na baba yake wala katika upande wa baba yake hamjui ndugu yeyote.

Je, kwa scenario kama hiyo binti anafaa kutolewa mahari na kuolewa?

Na taratibu za mahari zipoje? Kwani navyojua mahari ni ya baba na kama baba hayupo mahari ipokelewe na yeyote upande wa baba yaani shangazi au baba mdogo au mkubwa.
Kwani waoaji wanataka kumpatia nani? Pia, waoaji watataka kumuona baba wa mtoto. Kwani huyo baba aliikataa hiyo mimba au huyo mtoto?

Kama kalelewa kwa mama na baba hakuwa na mchango wowote na kumkataa directly au indirectly, mjomba anapokea hiyo mahari, ingawaje sijui kwa makabila mengine.
 
Kwa waislamu (tukiacha posa maana sina ujuzi nayo) mahari anapewa muolewaji. Mahari ni zawadi ya bwana kumpa bibi na wala si thamani ya binti kwamba ananunuliwa kwayo!

Utofauti wa zawadi hii na zawadi nyingine ni kuwa muoaji haamui tu yeye mwenyewe bali lazima amuulize huyo mwanamke anayetaka kumuoa kwamba angependa zawadi gani.

Kwahiyo mahari atakayotaja bibi basi bwana ataileta na itapokelewa na walii wa muolewaji (walii ni baba wa muolewaji au mwanaume yeyote wa upande wa baba wa muolewaji aliyepewa jukumu la kumuozesha binti)

Akishapokea huyo walii atampa binti mahari yake yote iliyotolewa kisha ndoa inafungwa. Maamuzi ya mahari achukue au awaachie wazazi au atumieje yanabaki kwa binti mwenyewe.

Watu sasa (hasa watu wa mila za Kitanzania) kwa kuona sheria hiyo wakaingiza mambo kibao hapo ili wapate ulaji kupitia ndoa. Mara mkaja, mara blanketi, mara makosa, mara... Yaani unakuta unataka kuoa lakini unawalipa hela wana ukoo wote wa binti! Matokeo yake kukitokea jambo kidogo mtu anakimbilia kwenye mahari anaanza kuwianisha thamani ya ndoa au mtu na mahari.
 
Sidhani kama mleta mada kauliza kwa ubaya.

Kama mtu unafahamu taratibu, ni bora kumuelimisha kuliko kumzodoa na kumuona kwamba ni mzinguaji.

Hata kama upande wa kiume hautambuliki, lakini haiondoi ukweli kwamba mtoto lazima awe na baba mzazi. Na kuna sababu nyingi, zinazoweza kupelekea upande mmoja usiweze kutambulika.

Mzee wetu Mohamed Said njoo utupe elimu kidogo juu ya hili.
 
Hapa mnahangaika bure kuwa na mjadala mrefu. Upande wa baba hauhusiki kwa jambo lolote mahari inapokelewa na wajomba.

Huyo baba anayezungumzwa yeye mwenyewe hatambuliki na familia ya mama wa binti. Na hii inaonyesha wazi pia huyo baba wa binti hajawahi jitambulisha kama ndio mwenye mtoto wala kutoa mahari yoyote kwa mzazi mwenzie na hata malezi ya mtoto. Anakuja kuhusikaje kupokea mahari? Mtoto mpaka anafikia umri wa kuolewa baba yupo tu hafanyi jitihada zozote kuhusu mtoto wake. Uhalali wa kuwa mzazi unakuja na wajibu.
 
Ogopa mapel binti anaelelewa na mama tu hafai kuwa mke ,hamsikii tu kwa sasa ndoa ni utapeli wa hali ya juu?
Ni Kweli kabisa.
Mwanamke asiyelelewa na baba ni janga sana. Angalau Binti apate malezi ya baba ajue hekaheka za kufokewa mara nyingine na baba au ukali Wa baba japo Wa baba SIO wakali sana Kwa Binti zao lakini baba hawapeandi Kuona mabinti wanakua na uhuru Wa kuzurura mitaani au kusimama simama na wanaume mitaani.

Sasa ambaye ni single mother Hali ni Tofauti Inabidi umlelee kikekike na wanawake Wana ubinafsi Wa kutaka uhuru mkubwa Karne hili . Atataka uhuru aliokua anaiona Kwa mama yake aishi hivyo hivyo,yaani single maza Hata akiamua Kulala NJE hakuna Wa kumuuliza na haogopi chochote. Akiamua kubadili wanaume usiku na mchana hakuna Wa kumuuliza. Sasa Binti Aliyekulia kwenye mazingira yasiyo na utaratibu Wa kibaba na kimama ndani ya Ndoa ni Mungu tu ataweza kumfanya awe Mwanamke Bora.

Hata hivyo Kwa sana Ndoa kuvunjika ndani ya Miezi mitatu imeshakuwa ni jambo la Kawaida
 
Back
Top Bottom