Je, nani anatoa taarifa binafsi za wananchi kwenda makampuni ya Mitandao ya Simu?

greater than

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
1,764
Reaction score
3,230
Jumatatu ya leo ya tarehe 13/04 ni kumbukizi ya siku ya kuzaliwa.

Asubuhi nilipokea pongezi kutoka kwa marafiki na jamaa kupitia jumbe za meseji za kawaida na WhatsApp.

Ilipofika mida ya saa 4 Asubuhi, nikapokea meseji kutoka Airtel, ikintakia heri ya siku ya kuzaliwa.Nilifurahi lakini baada ya kama dakika 5 hivi;nikaanza kujiuliza maswali

1. Wamejuaje kama leo ni siku yangu ya kuzaliwa

2. Kama ni kupitia NIDA ,je, wamepewaje bila ridhaa yangu

3. Makampuni binafsi mangapi mengine wana taarifa zangu binafsi?

4. Kama zinatumika kibiashara,mimi nafaidikaje

5. Narindwaje kwa uwepo wa taarifa hizi katika makampuni binafsi...?

Nikaona hili suala lafaa kulileta jukwaani ili kuona maoni ya wengine.
 
Hizo taarifa uliwapa wewe mwenyewe, ukiwa na akili Timamu wakati wa kusajili Raini ya Simu.

Tena wakasema weka saini apa ukaweka huku unachekelea, Kuna kikaratasi hua kina kuja na simcard kinaeleza bayana A - Z na jinsi watakavyo tumia data hzo kwa ajiri ya biashara, lkn wewe hukusoma..
 
Nilijaza namba ya NIDA ili waweze kuona kama namba ipo kwenye Database ya serikali...

Taarifa binafsi zinatakiwa kuhifadhiwa na serikali.
 
Jumatatu ya leo ya tarehe 13/04 ni kumbukizi ya siku ya kuzaliwa.

Asubuhi nilipokea pongezi kutoka kwa marafiki na jamaa kupitia jumbe za meseji za kawaida na WhatsApp.

Ilipofika mida ya saa 4 Asubuhi, nikapokea meseji kutoka Airtel, ikintakia heri ya siku ya kuzaliwa.Nilifurahi lakini baada ya kama dakika 5 hivi;nikaanza kujiuliza maswali

1. Wamejuaje kama leo ni siku yangu ya kuzaliwa

2. Kama ni kupitia NIDA ,je, wamepewaje bila ridhaa yangu

3. Makampuni binafsi mangapi mengine wana taarifa zangu binafsi?

4. Kama zinatumika kibiashara,mimi nafaidikaje

5. Narindwaje kwa uwepo wa taarifa hizi katika makampuni binafsi...?

Nikaona hili suala lafaa kulileta jukwaani ili kuona maoni ya wengine.
Happy birthday mkuu,ishi sana 🙏..faida ni lile gawio wanatumaga usiku wa manane😀😀😀au hujawai pata?
 
Hizo ni kumbukumbu zako ulizo zitoa mwenyewe wakati wa kusajili laini, kinacho kushangaza hapo ni kipi?

Unapoenda kusajili laini kwa kutumia kitambulisho cha NIDA au kingine, taarifa zako zinabaki kwenye data base yao kuanzia siku hiyo.
 
nilienda dodoma, Yas wakaniambia, karibu kwenye duka letu ambalo lipo sehemu x,( ndani ya dodoma ) pia nikaenda Manyara wakaniambia karibu kwenye duka letu lililopo Galapo ( ndani ya manyara )
Mkuu, hujawahi kuligundua hili unapohama ukanda mmoja kwenda mwingine hata vifurushi vya mitandao vinakuonesha?

Ukishaanza kutumia simu tayari umejianika.
 
Back
Top Bottom