Prakatatumba abaabaabaa
JF-Expert Member
- Aug 2, 2022
- 1,842
- 6,087
Ni jioni Sasa napanda Kitandani kupumzisha fuvu langu nikitafakari mambo yaliyotokea leo.
Mpaka muda huu nimepokea simu 3 kutoka kwa washikaji zangu tuliosoma nao chuo wanafunga ndoa simu za usumbufu ni Kila siku, jirani yangu hapa mtoto wake anapata kipaimara kesho anaomba mchango, napigiwa simu na baba yangu mdogo nitume mchango wa harusi ya dada angu, mjomba ananipigia simu nim-support kwenye ndoa anayofunga. Mimi sikufanya sherehe ya ndoa kwa sababu ya kuepuka gharama na kusumbuana na watu, nilienda na wife kwa mchungaji tukamaliza ofisini.
Marafiki zangu wanaomba pesa kidogo tu hata ya vocha 5000-10,000 (Hawa ni washikaji zangu haswa ambao siwezi kuwatupa).
Bado mdogo wako anakutafuta umpe Hela ya graduation ya form four, Hapo sijarudi kwenye familia yangu hapa mambo ni mengi mnoo Bado wazazi wa pande zote mbili, Kodi ya nyumba n.k kipato chenyewe 400,000/= kwa Mwezi.
Nimeona Ili kuepuka lawama kutoka kwa watu nawaza kubadilishana Laini ya simu kabisaaa, Kuna kitu nimekigundua mtu Ukiwa na roho nzuri basi sahau kuishi Maisha unayoyawaza utajikuta nusu au robo tatu ya kipato Chako wanatumia wengine.