Je naweza kumjua mtu anaetumia arv

Je naweza kumjua mtu anaetumia arv

SWEET GIRL

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2011
Posts
520
Reaction score
377
Wadau habari hapa jamvini
Mimi nauliza swali je mtu anaetumia ARV anaweza kugundulika kwa dalili zipi??
 
No sign unless huyo mtu alishawahi kuugua sana,kwani akianza kuzitumia kwa uliyemzoea pale mwanzoni utamuona ana utofauti flani sasa sijui ni kwa wote na au la lakini baada ya muda fulani anarudi kwenye hali yake ya kawaida yaani hakuna dalili yoyote ya kuonyesha anatumia,hivi nionavyo mimi kwa experience nilioipitia na kwa watu nilio karibu nao ambao nafahamu wanatumia hizo dawa.
 
Wadau habari hapa jamvini
Mimi nauliza swali je mtu anaetumia ARV anaweza kugundulika kwa dalili zipi??

mnataka muanze kunyanyapaa watu? Jamani, wameacha kuslim bado mnawafuata na huku? Dawa ni kupima kabla ya kufanya uzinzi.
 
Sioni utofauti wa wewe na wale madaktari na manesi wanaobeba habari za wagonjwa hospital na kuzipeleka vijiweni.!
 
Wadau habari hapa jamvini
Mimi nauliza swali je mtu anaetumia ARV anaweza kugundulika kwa dalili zipi??
Kuna baadhi wanaweza kuwa na "Buffalo syndrome" (aina fulani ya kibiongo) nayo ni mojawapo ya dalili za wanaotumi ARVa
 
Hahhaahahahaa bufallo syndrome..ddnt knw

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Wadau habari hapa jamvini
Mimi nauliza swali je mtu anaetumia ARV anaweza kugundulika kwa dalili zipi??

Si rahisi kujua mtu fulani anatumia dawa za ARV, ...dawa za ARV zina madhara fulani (Side effects), hizi hutegemeana na dawa fulani. Lakini pia baadhi ya madhara haya yanaweza kuwa kama dalili za ugonjwa mwingine.

Hivyo basi pasipokujua mtu fulani ameatjirika kwa VVU si rahisi kutambua, ingawa inawezekana.
 
Kuna baadhi wanaweza kuwa na "Buffalo syndrome" (aina fulani ya kibiongo) nayo ni mojawapo ya dalili za wanaotumi ARVa

Kuna watu wanaweza kuwa na Cushing syndrome na hivyo kuwa na kibiongo (Buffalo torso), hivyo si sababu tosha ya kusema mtu anatumia dawa za ARV.
 
Kuna watu wanaweza kuwa na Cushing syndrome na hivyo kuwa na kibiongo (Buffalo torso), hivyo si sababu tosha ya kusema mtu anatumia dawa za ARV.

mkuu hawa ni wanyanyapaa, shida yao nini,? Kama wana tamaa ya ngono wawe wanapima kwanza. We unataka kujua dalili za patients on art ili iweje? Uwe unatangaza njiani? Jf doctor is not kwa ajili ya kupoint watu mitaani.
 
Huyu inaelekea ameharibu mahali, sasa anatafuta namna ya kujipoza!
 
Dawa ni Yesu bwana. Mbona unambania mwenzio wewe?

Aah King'asti upo sawa kabisa!
Mithali 26:5 inasema hivi: "Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake;
Asije akawa mwenye hekima machoni pake."
Ndivyo nilivyo fanya kwa mtoa mada!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom