Je naweza kupandikiziwa korodani (P"mbu) mpya

Je naweza kupandikiziwa korodani (P"mbu) mpya

Adolph Jr

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2016
Posts
5,950
Reaction score
9,511
Baada ya kuzaliwa mdogo wangu alionekana ana tatizo la korodani kuto kushuka katika eneo lake (scrotam) na kubakia kwa juu tumboni yaani hazishikiki...,
Tulichelewa kufanya maamuzi ya kumuwahisha kufanya operation (upasuaji) , lakini pindi tulipoamua kwenda hospital madaktari walituambia tumechelewa kumpeleka kwani ilifaa kabla hajafikisha mwaka mmoja hivi sasa anayo 20 ...
Na hivyo wakasema anahitaji upasuaji wa kuziondoa kabisa maana zinaweza develop Cancer ...
Please wataalam mnaweza msaidiaje huyu kijana maana watoto ni muhimu jaman ....kwani wakiisha zitoa ndo hapati kabisa...au kama vipi ziondolewe hizo awekewe mpya.....msaada wajuvi wa mambo haya....
 
Msaada wa mawazo na tiba pia kwa tatizo hilo.....
 
Pole sana, nadhani uwezekano upo ila kwa hapa kwetu ni ngumu. Je, penis yake ina erect?
 
Kwani madaktari wake wamesemaje? hamkuwauliza hilo?
 
ungewauliza zaidi mafaktari waliomhudumia toka mwanzo nafikiri watakupa majibu yote ya mwaswal unayojiuliza.
 
Kama ana miaka 20 si ampige demu mimba ndio azing'oe awe na mtoto hata mmoja
 
sidhani kama hizo korodan kama zinafanya kazi mpaka sasa.angejaribu kufanya uzalishaji mwingine tofauti na watoto kwani hata wakina kaoge,James delicios,raybayb na akina dan mtoto wa mama walizariwa na watu wenye korodani zinazofunction.huenda angekuwa na korodan nzima angezaa wasiohitajika kama watajwa hapo juu kwa hiyo kumshukuru mungu kunamuhusu
 
Pole sana kwake, sasa kwa nijuacho korodani haitakiwi kukaa juu kwa sababu ya jotoridi lililoko huko juu kwa sababu ya joto zinaharibika.
Labda apate ushauri kutoka experts wa masuala hayo ya urology etc ili wampe technical concepts

Poleni sana sana
 
Kuhusu kupandikiza mpya, hilo hakuna duniani kote, hata wanaofikia hatua ya kuziondoa au kufanyiwa matibabu ya mionzi na mengine kama hayo kwenye testicles ambayo yanamadhara kwa ubora wa sperms, huwa wanashauriwa kutunza sperms zao hospitali (sperm banks) kwa matumizi ya baadaye.

Sasa huyo mdogo wetu, maelezo yanaoneshi status ya testicles kwa sasa, huenda hata ziliishakufa na hazina kitu ndani, kama zingekuwa nzima huko juu bado kuzishusha inawezekana na zikaendelea kupiga kazi. Uhakika wa kukuta nzima ni asilimia sifuri point something.
 
Nachoweza kusema ni poleni. Kuweni karibu na huyo mtu maana kwa tatizo lake anaweza akaja kujidhuru. Mungu huyu kuna watu anajua kuwapa mitihani
 
Baada ya kuzaliwa mdogo wangu alionekana ana tatizo la korodani kuto kushuka katika eneo lake (scrotam) na kubakia kwa juu tumboni yaani hazishikiki...,
Tulichelewa kufanya maamuzi ya kumuwahisha kufanya operation (upasuaji) , lakini pindi tulipoamua kwenda hospital madaktari walituambia tumechelewa kumpeleka kwani ilifaa kabla hajafikisha mwaka mmoja hivi sasa anayo 20 ...
Na hivyo wakasema anahitaji upasuaji wa kuziondoa kabisa maana zinaweza develop Cancer ...
Please wataalam mnaweza msaidiaje huyu kijana maana watoto ni muhimu jaman ....kwani wakiisha zitoa ndo hapati kabisa...au kama vipi ziondolewe hizo awekewe mpya.....msaada wajuvi wa mambo haya....
Ulimpeleka hospital gani
 
Back
Top Bottom