Je!naweza kuunganisha floot swith 3 kwenye pump moja?

Je!naweza kuunganisha floot swith 3 kwenye pump moja?

Nitafafanua kwa kutumia block diagram hii hapa chini

View attachment 3453995
1. Una float swict nne, kila tenki ina moja.

2. Float switch zinazoweza kuwasha pump ni FL2, FL3 na FL4. na hizo float switch wakati zinawasha pump, vilevile kila moja itafungua valve inayoingiza maji kwenye tenki lake.

3. Float switch namba 1 (FL1) kazi yake ni kuhakikisha maji yapo kwenye underground tank na ndipo iruhusu pump kuwaka endapo itawashwa na float switch yoyote kati ya FL2, FL3 na FL4 au, mbili au zote. Yoyote kati ya hizo tenki laki likijaa, itafunga tenki husika kupitia solenoid valve na kuondoa signal yake ya kuwasha pump. Hivyo kama kutakuwa na float switc nyingine imeruhusu pump kutembea, basi itabaki hiyo.

4. Endapo maji kwenye underground tenk yatakuwa yameisha, float switch number 1 (FL1) haitaruhusu pump kutembea, maana kutembeza pump wakati hakuna yaji ya kuya-pump utauwa pump (CAVITATION)

5. Huo mstari mweusi unawakilisha bomba za maji, na hiyo mishale inaonyesha uelekeo wa maji
Kwa iyo ina maanisha baada ya floot swith kuna vitu vingine vinahitajika hapo ili kazi yangu ifanyike ninavyotaka?
 
Ni kwangu kaka
Underground tank inalishwa na dawasa unataka uwekee float switch ya kazi gani.!? Waka ball valve inatosha

Na tank za juu hata ziwe kumi float switch moja tu inatosha wakiziunga pamoja

Huyo fundi wako wa mwanzo pia kakupiga
 
Back
Top Bottom