Je naweza kuwa na tatizo la kisaikoloji.Msaada tafadhari

Je naweza kuwa na tatizo la kisaikoloji.Msaada tafadhari

Pure_sapiens

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2016
Posts
2,228
Reaction score
2,064
Habari zenu wana jf.Niende kwenye mada ni hivi sina uwezo wa kukumbuka watu wangu wa karibu
Mimi nimesoma shule ya msingi makumbusho(2006)nimehitim lakini hakuna hata rafiki yangu mmoja ninayemkumbuka japo kuwa wao wananikumbuka na kuni call Mara kwa Mara.Elimu ya secondary nimemaliza mwaka(2010) Jamhuri dar sec school lakini hakuna ninayemkumbuka Kati ya wanafunzi niliomaliza nao.Advance nimesoma Benjamin sec school lakini nako tatizo ni hilo hilo linajirudia.
Nimemaliza elimu ya chuo hapo udsm lakini hakuna mtu wangu wa karibu ninayemkumbuka.Yaani hata mtaani wale niliocheza nao utotoni siwakumbuki kabisa mi nahisi naweza nikawa na tatizo lakini silijuwi.
Kibaya zaidi hata viongozi wangu wa nchi siwajuwi kwa majina na wadhifa wao katika nchi.
Je kwa maelezo hayo naweza kuwa na matatizo,kama ninayo ni yapi na yanatibika.Naomba ushauri wenu Matusi na kebehi havina nafasi
 
😱😱
waisheni msaada atasahau na huu uzi
 
aaaahh punguza puchuu......inasababisha kusahau sahau
 
Basi utakuwa na roho mbaya na ubinafsi uliopitiliza ndio maana
 
Duh inaweza kuwa utani au ni kweli. Pole mkuu
 
Sawa tumeshaipata biography yako isipokuwa tuu picha na majina kamili!
 
jaman nimecheka eti hata viongoz wako wa taifa huwakumbuki hahahhah bora aiseee
 
Viongozi hauwakumbuki kwan waliopita au hauwajuhi waliopo? Maana mimi najua kukumbuka ni kutaka kurejesha mawazo yako nyuma kukumbuka yaliyopita, sasa viongozi wepi?
 
Viongozi hauwakumbuki kwan waliopita au hauwajuhi waliopo? Maana mimi najua kukumbuka ni kutaka kurejesha mawazo yako nyuma kukumbuka yaliyopita, sasa viongozi wepi?
waccm aanmaanisha
 
Mimi huwa sina tabia ya kipiga puli
Mimi ni mlinzi wa baa ya peace iko pale round about ya Makumbusho karibu na shule yenu.

Mwaka jana kama jumapili mbili nimeona wenzako wakikutana wa shule hiyo na waliomaliza mwaka huo.

Wakija jumapili hizi nitamuomba mmoja namba ili akuunganishe na wenzao.
 
Tukirudi darasani kuna kitu kinaitwa prosopagnosia au face blindness, ingawa kwa ninavyojua hii hua inafikia mpaka kwa ndugu zako hivyo nashindwa kupin point kama ndiyo kinachokusumbua.

Kwa kawaida hii hali ni ya kurithi.

Ulizia kama katika ukoo wenu kuna mtu aliwahi kupitia hii hali kisha Nenda hospitali.
 
Bhangi too much nayo some time inaweza kurusha network dizaini hiyo
 
Habari zenu wana jf.Niende kwenye mada ni hivi sina uwezo wa kukumbuka watu wangu wa karibu
Mimi nimesoma shule ya msingi makumbusho(2006)nimehitim lakini hakuna hata rafiki yangu mmoja ninayemkumbuka japo kuwa wao wananikumbuka na kuni call Mara kwa Mara.Elimu ya secondary nimemaliza mwaka(2010) Jamhuri dar sec school lakini hakuna ninayemkumbuka Kati ya wanafunzi niliomaliza nao.Advance nimesoma Benjamin sec school lakini nako tatizo ni hilo hilo linajirudia.
Nimemaliza elimu ya chuo hapo udsm lakini hakuna mtu wangu wa karibu ninayemkumbuka.Yaani hata mtaani wale niliocheza nao utotoni siwakumbuki kabisa mi nahisi naweza nikawa na tatizo lakini silijuwi.
Kibaya zaidi hata viongozi wangu wa nchi siwajuwi kwa majina na wadhifa wao katika nchi.
Je kwa maelezo hayo naweza kuwa na matatizo,kama ninayo ni yapi na yanatibika.Naomba ushauri wenu Matusi na kebehi havina nafasi

Hilo si tatizo kwani jibu tumeshalijuwa tayari. Hizo shule zote ulizozitaja hujasoma kweli na ndiyo maana hukumbuki kitu wala mtu. Je, majengo yake unayakumbuka? Sasa hao marafiki zako wanakupigia simu unawakumbukaje kama si uwongo? Je, unavuta bangi au kubugia yale madudu ya Chidi Benz? Nakuuliza hivi kwa sababu hizi ni dalili zake.
 
Back
Top Bottom