Je, ni aibu, kwa familia ambayo wazazi walikuwa watumishi wa serikali lakini hakuna mtoto aliye serikalini?

Je, ni aibu, kwa familia ambayo wazazi walikuwa watumishi wa serikali lakini hakuna mtoto aliye serikalini?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Nauliza hili swali niweze kupata viewpoint yenu maana kuna baadhi ya watu nawashangaa wanasema watoto wameaibisha wazazi wao ila mimi naona hawapo sawa kwasababu kazi hazirithishwi, Nyie mnaona vp?

baba alikuwa ni engineer shirika kubwa tu, Mama alikuwa ni Muhasibu taasisi flani ya mambo ya mapato, Wazazi wote wameshastaafu. Wazazi walikuwa poa kiuchumi maana kila mtoto alipomaliza form 6 alipewa gari kasoro moja tu ambae shule ilimshinda.

Watoto wapo wanne.

Mtoto wa kwanza wa kasoma engineering ila kazi ni changamoto zimemfanya afungue kibanda umiza.

Mtoto wa pili kasomea procurement ila kazi kakosa kaolewa, ni mama wa nyumbani

Mtoto wa tatu shule ilimshinda kaamua awe fundi matairi ya scania, biashara iko poa hakosi laki kwa siku.

Mtoto wa mwisho wa mwisho kasomea uhasibu lakini kafungua mgahawa wake mtaani ni mama ntilie.
 
Una matatizo makubwa Sana ya akili
 
Tueleze, ulitegemea waingie vipi?
 
Sijaelewa point Yako. Kwani ulitaka wazazi waajiri watoto kwenye mashirika ya umma kwani wao ni maafisa utumushi?
 
Ungejua wafanyakazi wa serikalini wanalipwa RAMBI RAMBI na sio MISHAHARA usingeandika ulichoandika hapa
 
baba alikuwa ni engineer shirika kubwa tu, Mama alikuwa ni Muhasibu Tra, Wazazi wote wameshastaafu.

Watoto wapo wanne.

Mtoto wa kwanza wa kasoma engineering ila kazi ni changamoto zimemfanya afungue kibanda umiza.

Mtoto wa pili wa kike kasomea procurement ila kazi kakosa kaolewa, ni mama wa nyumbani

Mtoto wa tatu wa kiume shule ilimshinda kaamua awe fundi matairi ya scania, biashara iko poa hakosi laki kwa siku.

Mtoto wa mwisho wa kike wa mwisho kasomea uhasibu lakini kafungua mgahawa wake mtaani ni mama ntilie.
Kwanini unasema ni aibu? Ulitaka watumie nafasi zao serikalini kuwaingiza watoto wao hata kama hawana sifa?

Kwanini usione kuwa mfumo wa ajira serikalini kupitia Sekretariati ya Ajira uko fair and transparent?

Mimi ni dreva wa Benki binafsi hapa Dar lakini binti yangu Ali graduate mwaka jana na akaomba kazi za TRA zilizotangazwa Oktoba. Alipata bila kutoa rushwa wala kusaidiwa.

Tuipongeze Serikali inapofanya vizuri
 
Ilikuwa ni system nzuri enzi hizo, kwa sasa mambo yamebadilika, Raisi katoa ruksa ajira ziweze kusimamiwa na mashirika badala ya sekretarieti

Mfano ni hizi ajira mpya za TRA wanasimamia wenyewe, tunarudi kule kule kwenye kujuana

Back
Top Bottom