Binafsi nishaandaa andiko la kuanza ufugaji wa nguruwe kwa kiwango kikubwa ili kwa siku za baadae nije kufungua kiwanda cha nyama ya nguruwe. Kwa sasa watanzania wengi tunakula nyama za nguruwe zisizo na ubora licha ya kuwa zinathibitishwa na madaktari wa mifugo. Pia soko kubwa lipo hata kwa nje ya nchi.