Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

🤣🤣🤣 hesabu za Present value na future value lazma zihusike. ROI, ROCE na wenzake
Sawa mkuu, huyu ana kiwanja na nyumba yake ya 150m na mwingine ana 498m.

Yes hawa after 29 year wapo hapo je nani mjanja?
 
Kaka wengi wetu si wavumilivu pia hatujifunzi wakati wa changamoto za biashara zetu mtu akipata changamoto kidogo anabadilisha biashara huko nako anakutana na zingine tena kali zaidi ya zile za kwanza.

Ni kweli pia kwamba kingine kikubwa kinachokwamisha ni kumbukimbu ya mahesabu yaani mapato na matumizi ya biashara...mara nyingi hakuna kumbukumbu mtu anafanya project kwa uzoefu tu.

Good analysis; wengi tutajifunza hapa.
 
Huoni wewe pia itahitaji miaka 10 kubreak even
Bado ndani ya hiyo miaka 10 kuna marekebisho mengi na pia nyumba nzuri na mpya zitajengwa hivyo itakubidi upunguze bei
nadhani ujui ht bei ya cement kaka angu,, yaan baada ya miaka kumi kodi itashuka, kwaiyo unavyohisi kwa kodi iyo mtu atashindwa kurekebisha Nyumba kwa miaka iyo, kingine ukiwa na nyumba ya kupangisha si kwamba huna shuhuri zingine, unafikiri miaka kumi ijayo maitaji ya watu kupanga nyumba yatashuka kwakuwa idadi ya watu daresalaam itapungua au?
kama hujui miaka kumi ijayo kodi ya chumba tu kimoja itafika laki mbili, maana sasaivi chumba kimoja tu chenye masta ni laki moja bei kuanzia maeneo ya mbezi, bunju, tegeta, ununio, etc
 
Mimi huwa naamini nyumba hazipandi thamani bali hela yetu inashuka thamani na kusababisha vitu kuwa ghali hivyo nyumba nayo inapanda bei. Ibadili kwa dollar ndio utajua huwa haipandi bei
Kwa uelewa wangu mdogo, kadiri miaka inavyosonga mbele nyumba inachakaa na kutoka kwenye fashion na muonekano wa kisasa hivyo thamani yake inapungua.
Kuna mijengo ya miaka ya 2000 ilikuwa tishio lakini sasa hivi yamekuwa magofu. Mtu akinunua anaipiga chini yote na kuanza kujenga nyumba mpya.
Kwahiyo kinachopanda thamani ni kipande cha ardhi husika na sio nyumba.
 
Safi kabisa nenda Magomeni, Sinza utakuta mjengo style Msimbiji type 1980's kwa sasa utaipeleka wapi hiyo... sana sana uvunje ujenge mpya. Hata ukijenga yako swafii majirani je??

Kuna jamaa yangu ana watoto 3 wana 9, 5 na 3 sasa anawajengea kila mwanae nyumba moja...sasa swali by the time wanafika 30 utu uzima watazipenda hizo?

Ama angewekeza pesa hizo sehemu nyingine ili wakafika 30 wakutane nazo?
 
Uko sahihi kabisa

Hata mimi naamini kujenga ni uoga wa maisha nani mawazo yakizamani. Business models are changing we also must change
Sema hili kundi LA wajengaji kwa asilimia kubwa in Wafanyakazi ambao no wengi, na wengi wao huwa wanakuja kuikurupukia biashara wakiwa wameshastaafu. Kila MTU afanye kipaumbele chake ila kwangu Mimi swala LA kuzika Pesa Hapana kabisa
 
pokea phd ya heshima madam
 
Umetumia mfano usio na uhalisia sana wa mazingira yetu ya kitanzania.
 
Hii jf ya dizaini hii ilipotea sana. Great contribution...
 
Mie nilijenga Nyumba ya kupangisha kipindi cha nyuma kusema ukweli imenisaidia kusomesha watoto shule za kueleweka na hasa kwa kipindi hiki ambacho biashara zimeshuka sana.
 

Ni kweli

Ijapokua rais Mwinyi alifungua milango mwaka 1985 na sasa ni miaka zaidi ya 30 imepita nadhani athari hizo zinatakiwa ziwe zimefifia bynow
 

Wooow Very Nice

Umejenga eneo/ mitaa gani mkuu na kiwanja ulinunua au kilikuwepo tayari?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…