Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

🤣🤣🤣 hesabu za Present value na future value lazma zihusike. ROI, ROCE na wenzake
Sawa mkuu, huyu ana kiwanja na nyumba yake ya 150m na mwingine ana 498m.

Yes hawa after 29 year wapo hapo je nani mjanja?
 
Waheshimiwa

Kuna jambo moja ambalo watu wengi wamekua wanalikosea bila kujua. Kwa maoni yangu:
Ni muhimu kuelewa tofauti kati ya business na investments
Ni muhimu kuzingatia suala la return on investment au Retun on Asset wakati wowote unapofanya investment au biashara. Usipozingatia haya utasema huna bahati au unalogwa. Utakua frasturated na kuchukia biashara. Mfano

Mimi na wewe tunaweza kuchukua mkopo wa million 100, tukafungua biashara tofauti. Wewe ukawa unapata faida kubwa kwa haraka kuliko mimi. Au Wewe unaweza kuanzisha biashara ambayo ni capital intensive mimi nikaanzisha biashara ambayo sio capital intensive (haihitaji mtaji mkubwa). Au wewe unaweza ukafungua biashara yenye matumizi mengi / higher expenses kama daladala/ malori kuliko mimi. Au wewe unaweza ukafungua biashara yenye risk kubwa kuliko mimi kama vile daladala zinazopata ajali kila mara nk. Au wewe unaweza kufungua bishara yenye mzunguko mkubwa wa mauzo kuliko mimi. Yote haya yataamua nani atafanikiwa kuliko mwengine baina yetu

Wakati mwengine hata structure ya biashara inaweza kuamua nani anafanikiwa kuliko mwengine. mimi na wewe wote tunaweza kuanzisha biashara inayofanana lakini tukatofautiana katika structure ya management au operations na hapo mmoja akafanikiwa kuliko mwengine. Kwamfano wote tunaweza tukanunua bajaji kwa million 6 wewe ukaingia mkataba na dereva awe anakuletea kiasi fulani mpaka itakapofika million 10 then bajaji itakua yake. Mimi nikaweka dereva tu akawa analeta hesabu na hapo mmoja wetu akafanikiwa kuliko mwengine.

Wakati mwengine usimamizi tu unaweza kuleta tofauti kubwa sana. Wewe unaweza ukawa na Lori lako liko kijijini kwenu huko kaka zako wanasimamia na mimi nna Lori langu liko hapa Dar nasimamia mwenyewe au wote tunaweza kua na Fuso ziko dar lakini wewe ukapata dereva mwenye nidhamu mimi nikapata dereva asie mwaminifu na hapo tukapata matokeo tofauti kabisa

Tofauti hizi nyingi ndogo ndogo za kiufundi hua zinaleta matokeo tofautisana katika biashara na ni mambo ya kuzingatia kama unataka ufanikiwe kibiashara. ndio maana wewe unaweza ukawa na Daladala likakushinda ukauza mwenzako akanunua hioihilo akaa nalo miaka 10 ukabaki unashangaa

Kingine ni uvumilivu na kujifunza. Ukiwa na biashara na haiendi vizuri jitahidi kuvumilia na kujifunza na kurekebisha mapungufu yako katika biashara. Uyarekebishe na kuendelea. usiruke ruke na kuanzisha biashara mpya kila mwaka

Kingine Muhimu ni kuandika mapato na matumizi yote katika biashara yako ili baada ya mwaka au miaka 2 uweze kufanya tathimini na kuamua kama uendelee au la.

Mwisho nimalizie na mfano ulioko kwenye kichwa cha habari ya bandiko hili - case study. Nimekutana na rafiki zangu kama 4 ambao wanajilaumu kwa uamuzi wao wa kujenga nyumba na kuanza kukusanya kodi. Wamekuja kugundua baadae kua faida hua ni ndogo na inachukua muda mrefu sana kupata - inachukua zaidi ya miaka 20 kubreak even na kuanza kupata real profit. Yuko mmoja ameachiwa nyumba ya urithi na anasema anatamani angeweza kuuza na hizo fedha akaingiza kwenye biashara nyingine yenye high and quick return - familia haiwezi kumruhusu. Nyumba haimpi faida yoyote ya maana tena ni kubwa mno na wapangaji hamna. Yuko mwengine yeye alichukua mortgage kama million 200 pamoja na wife wakajenga nyumba. Wamekaa wamepiga hesabu na kugundua watakapomaliza kulipa baada ya miaka kama 15 watakua wamelipa kama million 400 kwa mbinde maana malipo ya mwezi ni zaid ya million 1 ambayo inawatesa sana kwasasa. Wanajilaumu. Kwamfano: ukijenga nyumba kwa million 150 na kuanza kukusanya kodi ya 600,00 kwa mwezi itachukua miaka 21 kuweza kukusanya kodi ya million 150. Kama unajenga nyumba ya kuishi ni sahihi lakini nyumba kama biashara it might be a challenge. Furthermore, kama una million 150 wapo wanaodhani unaweza kuiingiza kwenye biashara kisha ukatumia faida ya hiyo biashara kujenga nyumba polepole

Tupe maoni yako, tujadiliane, tubadilishane mawazo, tufundishane
Kaka wengi wetu si wavumilivu pia hatujifunzi wakati wa changamoto za biashara zetu mtu akipata changamoto kidogo anabadilisha biashara huko nako anakutana na zingine tena kali zaidi ya zile za kwanza.

Ni kweli pia kwamba kingine kikubwa kinachokwamisha ni kumbukimbu ya mahesabu yaani mapato na matumizi ya biashara...mara nyingi hakuna kumbukumbu mtu anafanya project kwa uzoefu tu.

Good analysis; wengi tutajifunza hapa.
 
Huoni wewe pia itahitaji miaka 10 kubreak even
Bado ndani ya hiyo miaka 10 kuna marekebisho mengi na pia nyumba nzuri na mpya zitajengwa hivyo itakubidi upunguze bei
nadhani ujui ht bei ya cement kaka angu,, yaan baada ya miaka kumi kodi itashuka, kwaiyo unavyohisi kwa kodi iyo mtu atashindwa kurekebisha Nyumba kwa miaka iyo, kingine ukiwa na nyumba ya kupangisha si kwamba huna shuhuri zingine, unafikiri miaka kumi ijayo maitaji ya watu kupanga nyumba yatashuka kwakuwa idadi ya watu daresalaam itapungua au?
kama hujui miaka kumi ijayo kodi ya chumba tu kimoja itafika laki mbili, maana sasaivi chumba kimoja tu chenye masta ni laki moja bei kuanzia maeneo ya mbezi, bunju, tegeta, ununio, etc
 
Mimi huwa naamini nyumba hazipandi thamani bali hela yetu inashuka thamani na kusababisha vitu kuwa ghali hivyo nyumba nayo inapanda bei. Ibadili kwa dollar ndio utajua huwa haipandi bei
Kwa uelewa wangu mdogo, kadiri miaka inavyosonga mbele nyumba inachakaa na kutoka kwenye fashion na muonekano wa kisasa hivyo thamani yake inapungua.
Kuna mijengo ya miaka ya 2000 ilikuwa tishio lakini sasa hivi yamekuwa magofu. Mtu akinunua anaipiga chini yote na kuanza kujenga nyumba mpya.
Kwahiyo kinachopanda thamani ni kipande cha ardhi husika na sio nyumba.
 
Safi kabisa nenda Magomeni, Sinza utakuta mjengo style Msimbiji type 1980's kwa sasa utaipeleka wapi hiyo... sana sana uvunje ujenge mpya. Hata ukijenga yako swafii majirani je??

Kuna jamaa yangu ana watoto 3 wana 9, 5 na 3 sasa anawajengea kila mwanae nyumba moja...sasa swali by the time wanafika 30 utu uzima watazipenda hizo?

Ama angewekeza pesa hizo sehemu nyingine ili wakafika 30 wakutane nazo?
 
Uko sahihi kabisa

Hata mimi naamini kujenga ni uoga wa maisha nani mawazo yakizamani. Business models are changing we also must change
Sema hili kundi LA wajengaji kwa asilimia kubwa in Wafanyakazi ambao no wengi, na wengi wao huwa wanakuja kuikurupukia biashara wakiwa wameshastaafu. Kila MTU afanye kipaumbele chake ila kwangu Mimi swala LA kuzika Pesa Hapana kabisa
 
Waheshimiwa

Kuna jambo moja ambalo watu wengi wamekua wanalikosea bila kujua. Kwa maoni yangu:
Ni muhimu kuelewa tofauti kati ya business na investments
Ni muhimu kuzingatia suala la return on investment au Retun on Asset wakati wowote unapofanya investment au biashara. Usipozingatia haya utasema huna bahati au unalogwa. Utakua frasturated na kuchukia biashara. Mfano

Mimi na wewe tunaweza kuchukua mkopo wa million 100, tukafungua biashara tofauti. Wewe ukawa unapata faida kubwa kwa haraka kuliko mimi. Au Wewe unaweza kuanzisha biashara ambayo ni capital intensive mimi nikaanzisha biashara ambayo sio capital intensive (haihitaji mtaji mkubwa). Au wewe unaweza ukafungua biashara yenye matumizi mengi / higher expenses kama daladala/ malori kuliko mimi. Au wewe unaweza ukafungua biashara yenye risk kubwa kuliko mimi kama vile daladala zinazopata ajali kila mara nk. Au wewe unaweza kufungua bishara yenye mzunguko mkubwa wa mauzo kuliko mimi. Yote haya yataamua nani atafanikiwa kuliko mwengine baina yetu

Wakati mwengine hata structure ya biashara inaweza kuamua nani anafanikiwa kuliko mwengine. mimi na wewe wote tunaweza kuanzisha biashara inayofanana lakini tukatofautiana katika structure ya management au operations na hapo mmoja akafanikiwa kuliko mwengine. Kwamfano wote tunaweza tukanunua bajaji kwa million 6 wewe ukaingia mkataba na dereva awe anakuletea kiasi fulani mpaka itakapofika million 10 then bajaji itakua yake. Mimi nikaweka dereva tu akawa analeta hesabu na hapo mmoja wetu akafanikiwa kuliko mwengine.

Wakati mwengine usimamizi tu unaweza kuleta tofauti kubwa sana. Wewe unaweza ukawa na Lori lako liko kijijini kwenu huko kaka zako wanasimamia na mimi nna Lori langu liko hapa Dar nasimamia mwenyewe au wote tunaweza kua na Fuso ziko dar lakini wewe ukapata dereva mwenye nidhamu mimi nikapata dereva asie mwaminifu na hapo tukapata matokeo tofauti kabisa

Tofauti hizi nyingi ndogo ndogo za kiufundi hua zinaleta matokeo tofautisana katika biashara na ni mambo ya kuzingatia kama unataka ufanikiwe kibiashara. ndio maana wewe unaweza ukawa na Daladala likakushinda ukauza mwenzako akanunua hioihilo akaa nalo miaka 10 ukabaki unashangaa

Kingine ni uvumilivu na kujifunza. Ukiwa na biashara na haiendi vizuri jitahidi kuvumilia na kujifunza na kurekebisha mapungufu yako katika biashara. Uyarekebishe na kuendelea. usiruke ruke na kuanzisha biashara mpya kila mwaka

Kingine Muhimu ni kuandika mapato na matumizi yote katika biashara yako ili baada ya mwaka au miaka 2 uweze kufanya tathimini na kuamua kama uendelee au la.

Mwisho nimalizie na mfano ulioko kwenye kichwa cha habari ya bandiko hili - case study. Nimekutana na rafiki zangu kama 4 ambao wanajilaumu kwa uamuzi wao wa kujenga nyumba na kuanza kukusanya kodi. Wamekuja kugundua baadae kua faida hua ni ndogo na inachukua muda mrefu sana kupata - inachukua zaidi ya miaka 20 kubreak even na kuanza kupata real profit. Yuko mmoja ameachiwa nyumba ya urithi na anasema anatamani angeweza kuuza na hizo fedha akaingiza kwenye biashara nyingine yenye high and quick return - familia haiwezi kumruhusu. Nyumba haimpi faida yoyote ya maana tena ni kubwa mno na wapangaji hamna. Yuko mwengine yeye alichukua mortgage kama million 200 pamoja na wife wakajenga nyumba. Wamekaa wamepiga hesabu na kugundua watakapomaliza kulipa baada ya miaka kama 15 watakua wamelipa kama million 400 kwa mbinde maana malipo ya mwezi ni zaid ya million 1 ambayo inawatesa sana kwasasa. Wanajilaumu. Kwamfano: ukijenga nyumba kwa million 150 na kuanza kukusanya kodi ya 600,00 kwa mwezi itachukua miaka 21 kuweza kukusanya kodi ya million 150. Kama unajenga nyumba ya kuishi ni sahihi lakini nyumba kama biashara it might be a challenge. Furthermore, kama una million 150 wapo wanaodhani unaweza kuiingiza kwenye biashara kisha ukatumia faida ya hiyo biashara kujenga nyumba polepole

Tupe maoni yako, tujadiliane, tubadilishane mawazo, tufundishane
pokea phd ya heshima madam
 
Ni kweli watu wengi Afrika wana mtazamo huu lakini nadhani times are changing nadhani kuna haja yakubadili mitazamo yetu na kufanya mambo kimkakati zaidi. Yuko bwana alinitumia bandiko hili linaloongelea kwamba wafanyabishara wengi wanalalamika biashara zinakua ngumu lakini wasichofahamu ni kua biashara zinabadilika na wao wanatakiwa wabadili business models. Nalinukuu bandiko lile la whatsapp hapa chini kwafaida ya wengi

Economy is not struggling...the business models are changing.

Below is a very interesting insight :

Often heard nowadays that " Kenyan Economy is struggling_ ".

Sit back & dispassionately think "is the economy really struggling or" are business models struggling ?

Some food for thought:

1) Car sales are going down... but Ola / Uber are rising.

2) Restaurants are going empty... but home delivery is rising

3) Tuition classes are not getting students but online studying is rising

4) Traders are struggling but online market sites and reference based direct selling are breaking all records in sales.

5) Old commission based businesses are snivelling... but online services, at low cost, are finding takers.

6) Cell phone bills have reduced & internet penetration is increasing.

7) Stable (read "Govt Jobs") are dwindling but "Start up" jobs offering equity & Flexi work time are expanding.

😎 Jobs seekers are reducing but job creaters are on the rise. Working 40 hrs a week for 40 years is trend of past. Working for few years and spending quality time in contributing to society is the trend.

If truth be told what we are experiencing is a transition phase.

& Any transition is painful for the "well set"...... "the masters of the past".

_It's challenging for those who's business models are based on ancient data...._

It's a mystery for those who have never looked beyond traditional methods or have assiduously resisted change of any kind.

Economy is not struggling...the business models are changing.
Umetumia mfano usio na uhalisia sana wa mazingira yetu ya kitanzania.
 
Nadhani tunapokosea sana ni kutojua faida inakuja baada ya muda gani? Eneo ninalojenga je linalipa? Mfano jirani yangu mjeda kachukua mkopo sijui ni kiasi gani kanunua viwanja vitatu mtaani. Kajenga nyumba tatu, mbili hazijamalizika. Alipopata mkopo kwanza kamnunulia wife Ist ya kuwapeleka watoto shule.nyumba ya kwanza imeisha ni two in one kuna mpangaji mmoja tu. Hizo mbili keshapaua lkn finishing bado naona pesa zimekata, naona wife hatumii tena IST, watoto wanasimamishwa shule pesa hakuna. Imefikia wife wake anauza mpaka bites na mboga mboga mtaani. Huyu kafanya bad investment, kwanza maeneo aliyojenga kodi haizidi laki 3. Pili katumia pesa yote kujengea bila kuwa na savings huku marejesho yanamsubiri. Hapa utaona mkopo mbaya wala haufai. Lazima kuwe na projections ya mradi mzima. Nachukua pesa kiasi gani, mradi wangu una cost kiasi gani, mida wa mradi mpaka kukamilika, eneo husika la mradi lina thamani gani, mvuto wa eneo kwa wateja, umbali na barabara kuu, pia urahisi wa kufikika, uwepo wa maji, umeme. Baada ya mradi kukamilika tozo kwa chumba itakuwa kiasi gani? Je ntaweza pata rejesho kupitia tozo hizi? Atleast sasa waweza kopa mamilioni ukijua fika mradi utalipa
Hii jf ya dizaini hii ilipotea sana. Great contribution...
 
Mie nilijenga Nyumba ya kupangisha kipindi cha nyuma kusema ukweli imenisaidia kusomesha watoto shule za kueleweka na hasa kwa kipindi hiki ambacho biashara zimeshuka sana.
 
Sekta ya real estate KWA Tz NA Afrika yote haijaendelea sana, kwanza ndio imeanza miaka ya hivi karibuni.
KWA Tz sekta hii imeathirika zaidi na zaidi kwa miaka mingi kutokana NA sera mbaya kabisa ya Ujamaa, Azimio LA Arusha NA Operesheni Vijiji ambayo IPO tangu enzi za Mwl. Nyerere.

Watu waliojaribu kujenga nyumba au majengo ya biashara walionekana kuwa ni maadui ktk nchi, NA walibatizwa majina mbalimbali NA mabaya yasiyofaa kama vile, kupe, wanyonyaji, makabaila, mabwanyenye, n.k. Nyumba zao ziltaifishwa NA Serikali, Leo hii nyingi zinamilikiwa NA NHC.

Ni kweli

Ijapokua rais Mwinyi alifungua milango mwaka 1985 na sasa ni miaka zaidi ya 30 imepita nadhani athari hizo zinatakiwa ziwe zimefifia bynow
 
mnajidanganyaaa, Nyumba ya kupangisha inalipa sana, inategemea na eneo tu, mi nna Chumba sebule jiko, napangisha laki na nusu, na upande mwingine Ivyo Ivyo,

Yaan Nyumba moja ila ina pande mbili, kwaiyo nakusanya laki tatu kwa mwezi, na ya kawaida tu nje, ila ndani finishing nzuri,

Imenigharimu milioni 30,kujenga,
nimepaulia miti badala ya mbao za 4by 2..ila kwa upande wa 2by2 nimetumia mbao za Dawa, pia fishabodi mbao za dawa, mabati nimenunua ya gage 32 kwa Bei ya 16,000. Nimetumia bati sabini na tano tu, nyumba inalipa sana, ila usijenge kitajiri kama ni yakupangisha, na ikibidi mpaka mchanga nenda kanunue mwenyewe usimtume mtu, na misumari pia kanunue mwenyewe,

Yaan iyo million 150 mi najenga nyumba nne hapo za kodi ya laki tatu kwa mwezi,, ela Ya urithi niliifanyia jambo la maana nashukuru kwakweli

Wooow Very Nice

Umejenga eneo/ mitaa gani mkuu na kiwanja ulinunua au kilikuwepo tayari?
 
Back
Top Bottom