Naona mahesabu yenu wengi hayako sawa. Mnaweka rejesho katika hela ya mkopo na sio hela ambayo wewe mwenyewe umewekeza. Unaponunua au kujenga nyumba kuna 'down payment' ambayo ni asilimia flani ya bei ya nyumba unatoa mwanzo.
Kama hela yote ya kujenga au kununua unakopeshwa basi kiwango hiki ni sifuri. Hivyo sasa kama umejenga na rejesho la kila mwezi ukijumuisha rejesho kwa benki, gharama za utunzaji wa nyumba na matumizi yote yanayohusiana na nyumba ukapata 500,000 halafu kodi ikawa 600,000 basi hapo faida yako ni 100,000 kila mwezi ambayo ni 1,200,000 kwa mwaka. Kama hukutoa hela yoyote katika ujenzi au ununuzi hii ni 1.2 million ya faida kamili kutoka mtaji wa sifuri.
Hii ni pesa unaipata kila mwaka kwa muda wote unamiliki nyumba. Kama ulitoa hela yako mwenyewe katika ujenzi au ununuzi mfano milioni 12 basi unachukua 1.2 m gawa kwa 12 m unapata 10% rejesho kwa hela yako kila mwaka. Mtu yeyote ataefanya maamuzi mazuri katika kuchagua sehemu inayopangishika basi atafanikisha hili.
Ila uzuri wa real estate unakuja katika uwezo wa kufanyisha kazi mtaji (leverage). Kila ukilipa rejesho unajenga umiliki katika nyumba. Hivyo kama una umiliki wa asilimia 20 katika nyumba (yani umelipa rejesho kufikia umiliki huo) basi unaweza kutumia ule umiliki (equity) kupata mkopo mwingine.
Kumbuka kwa kuwa kodi ndio inalipa rejesho basi hii inakuwa hela ya bure kwa kuwa wewe binafsi pesa yako mfukoni haitoki. Mkopo huu unaweza kutumia katika ujenzi mwingine au biashara nyingine. Ni wachache wanajua kuhusu hili.
Jambo lingine ni kadri muda unavyoenda thamani ya nyumba inabadilika. Na muda wowote unaweza kwenda bank na kuwataka wafanye tathmini ya thamani.
Kama thamani imepanda basi unaweza kukopa tena kwa kuweka dhamana ya nyumba hiyohiyo ambayo inalipiwa na wapangaji. Mfano umejenga kwa milioni 100 na ndio thamani benki imekubaliana mwanzoni. Baada ya miaka 3 umeshalipa milioni 30 katika 100 hivyo kiharakaharaka una umiliki (equity) ya asilimia 30.
Ila kama unadhani nyumba imeongezeka unaweza kwenda benki na kuwataka wafanyie tathmini nyumba yako upya. Kama wakija na tathmini ya milioni 120 basi ina maana unaweza kukopesheka milioni 20 zaidi, hela ambayo unaweza kutumia kulipia mkopo au kufanyia mengine kama kujenga nyumba mpya. Hili ni advanced kidogo na inahitaji ujue hayo mawili ya kwanza kabla ya kuja huku.
Na hivi ndivyo unaweza kuwa tajiri kwa real estate. Kodi peke yake haitoshi ila kucheza na thamani ya nyumba yako ni muhimu pia.