mbu wa dengue
JF-Expert Member
- Jun 2, 2014
- 8,860
- 11,554
Au akikupiga ngumi ya jicho wewe unampiga ngumi ya sikio,akikuuliza unajionaje wewe unamuuliza anajisikiaje?Ukiniuzia cheni ya bandia nakupa pesa bandia pia.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Au akikupiga ngumi ya jicho wewe unampiga ngumi ya sikio,akikuuliza unajionaje wewe unamuuliza anajisikiaje?Ukiniuzia cheni ya bandia nakupa pesa bandia pia.
Nilimaanisha Mkwere MweusiMufuruki, Mosha, Mayo na wengineo ni Watanzania wekundu? Au unamaanisha kwenye ukoo wenu mkuu? Wapo Watanzania weusi wenye apartments mpaka nje ya Tanzania hata kama hatuwajui.
Ukitaka kufaidi biashara ya guest nenda ikwiriri tengeeza guest za kawaida za 10000Mkuu guest house si mpaka upate kiwanja maeneo ya mjini kitu ambacho si rahisi kihivyo. Guest nje ya mji kupata TZS 30,000 kwa kitanda bado ngumu'; labda Dodoma ambako mahitaji yanazidi idadi ya guest zilizopo kwa vipindi vya vikao vya Bunge
Duuh hii ni fursa kabisa.Ukitaka kufaidi biashara ya guest nenda ikwiriri tengeeza guest za kawaida za 10000
Nimekuwa nasafiri sana kwenda ikwiriri sijawahi pata guest bila kuweka oda. Ikifika satatu waweza kuzurura mji mzima mwisho ukalala stendi
Katika wote walioongea Point kuhusu kujenga Nyumba za Kupangishaa wewe ndo umenena Mkuu...tena jenga karibu na stand aiseee...[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]Utapiga pesa balaaaa hiyo mil 150 itarudi ndani ya mwaka tu mamaee..M naona kama unataka pesa wekeza kweny Lodge au nyumba za wageni ali maarufu kama gest House hii naamini haiangushani sana kama hizo za mwezi
wahindi hela zao za majini, usiwaige
M naona kama unataka pesa wekeza kweny Lodge au nyumba za wageni ali maarufu kama gest House hii naamini haiangushani sana kama hizo za mwezi
umeongea pointi sana..Nahisi kuna mambo kadhaa yanaachwa kwenye huu mjadala.
1: Nyumba ya kuishi Vs Nyumba ya Kupangisha.
Nyumba ya kuishi : Hapa watu tumetofautiana malengo kwenye maisha.., ukielewa hili wala hutopata tabu., mimi nimekua na ndoto zangu kua nyumba ntakayoishi lazma iwe na swimming pool..lazma iwe na uwanja mkubwa..garden..parking ya maana n.k, hivyo nimekua mkubwa nimejenga hivi lakini nje ya mji kidogo...kwangu mimi ..nimetimiza ndoto..na kila nikilala nikiamka...naona fahari., sasa ukiniambia nikakae sinza mfano..kwenye kijumba kama kiota cha ndege kisa tu nakaa mjini ...siwezi kukuelewa..sana sana ntakuona una shida na umaskini.., huu ni upande mmoja wa kuangalia hili suala..., watu wanajenga kwa sababu mbalimbali...wengine wana ndoto za kuishi maisha flani hivi..wengine wana familia kubwa hawawezi kupangisha chumba na sebule . n.k
Nyumba ya kupangisha: Pia kwenye hili ....inabidi tuwaze zaidi.., Wapo wanaoona hii ndo biashara salama ..hawataki stress za biashara...., ukijenga nyumba kwa mil 100, ukiwa unapokea kodi laki 5 kila mwezi...ukiwa unaila hii pesa..., tatizo liko wapi.,? kuna tofauti gani kama ungekua na hii 100mil na wewe uwe una withdraw kidogo kidogo kwenye account?
Pili: kwa wale wenye watoto., kuna njia gani safe zaidi ya kumpa kianzio mwanao zaidi ya real estate? ..mimi ninae jenga..unajuaje kama nimewajengea wanangu...baada ya hio miaka 20, wao watakua vijana na ndo wataanza ku enjoy? cha kuelewa hapa ...sio kila investment mtu anayofanya ni kwa ajili yake....
Swali la kizushi : Nyie mnaoona fahari kua mnapanga tu...hao wenye nyumba wenu wangekua na mawazo kama yenu ..mngekua mnaishi wapi?
Hitimisho: Tusijazane upepo wala kutiana ujinga... mwisho wa siku Nyumba/Kiwanja (kwa ajili ya biashara) ndo best way ya kuhifadhi pesa .., ila kwa anaetaka biashara yenye kurudisha faida haraka haraka..hio sio investment sahihi kwake.
Ni vizuri mtu ujenge mahala pakuishi kwanza then uje na ujenzi wa nyumba za kupangisha...na tena nyumba za kupangisha iwe ni unajega ghorofa hata floor mbili tu ili uanze kukusanya haraka kodi, pia nyumba za kupangisha kama upo eneo ni zuri usitumie gharama kubwaa kujenga maana itakuchukua muda kurejesha,
Wahindi wengi nchini hawamiliki nyumba ila wamefikia utajiri wa kutisha. Sisi wabantu tunakimbilia kujenga Mapinga, sijui Mkuranga watoto tunawapeleka st.kayumba bado utegemee maajabu maishani
Mkuu kuna kitu haujui kwenye real estate business.., nayo ni Other Peoples Money.., pia kitu kinaitwa Property Ladder..
Moja hakuna mtu wala sio busara kujenga nyumba kwa cash au pesa yako.. (it takes long kwa return on investment)
Hivyo basi katika hii real estate.., mtu anakopa benki anajenga nyumba hata ikichukua miaka 20 kurudisha ile pesa, hajengi moja..., hio aliyoshajenga anaiombea mkopo benki anajenga nyingine na nyingine na nyingine hii miaka 20 inakuwa sio ya kupata pesa ya kula bali wapangaji ndio wanaomnunulia hizo nyumba.., after the end of 20 years anakuwa amejenga nyumba bila kutumia senti yake hata moja.. (thus other peoples money)... na property ladder unaanza na nyumba moja unakopa unajenga ya pili, tatu, nne n.k.
Cha maana ni Location, Location, Location na sio muda wa kumaliza hio investment.., Walijisemea wachina wote tungetaka kupata kivuli cha miti tunayopanda hakuna mtu angepanda mti..., 20 years in nothing if someone else is paying..
nakuacha na msemo mwingine "As Safe as a House..."