Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Mufuruki, Mosha, Mayo na wengineo ni Watanzania wekundu? Au unamaanisha kwenye ukoo wenu mkuu? Wapo Watanzania weusi wenye apartments mpaka nje ya Tanzania hata kama hatuwajui.
Nilimaanisha Mkwere Mweusi
 
Changamoto kubwa ni kuwa uamuzi wa uwekezaji unafanywa holela na si systematic.mko bar mnakunywa castle unapewa wazo la biashara na maneno hayo yanakuwa msingi wa uamuzi. Maswali ya kuwa : Mosi , Uwekezaji unarudi lini?.Pili, Nia ya kuwekeza ni nini i.e Cashflow au hutaki pesa zipotee? Wala hayawi sehemu ya uamuzi.

Jambo lingine la kujua hakuna shughuli ya uchumi isiyo na hatari .hata kuweka fedha bank nayo ni hatari ukibisha waulize watu walioweka pesa Twiga Bancorp na Meridian Biao. Ukisema ununue hati fungani pia serikali zina default ukibisha waulize watu waliokuwa na hati fungani za ugiriki.

Ukisema ardhi haiushuki thamani pia siyo kweli Magu alivyoingia thamani ya ardhi ilishuka sana na hata nyumba zilianguka bei.

Dhana ya kuwa kuna risk free asset or investment ni nothing more than a mirage.ukiamua kufanya biashara ni lazima uwe na roho ngomo na mvumulivu .
 
Mkuu guest house si mpaka upate kiwanja maeneo ya mjini kitu ambacho si rahisi kihivyo. Guest nje ya mji kupata TZS 30,000 kwa kitanda bado ngumu'; labda Dodoma ambako mahitaji yanazidi idadi ya guest zilizopo kwa vipindi vya vikao vya Bunge
Ukitaka kufaidi biashara ya guest nenda ikwiriri tengeeza guest za kawaida za 10000
Nimekuwa nasafiri sana kwenda ikwiriri sijawahi pata guest bila kuweka oda. Ikifika satatu waweza kuzurura mji mzima mwisho ukalala stendi
 
Ukitaka kufaidi biashara ya guest nenda ikwiriri tengeeza guest za kawaida za 10000
Nimekuwa nasafiri sana kwenda ikwiriri sijawahi pata guest bila kuweka oda. Ikifika satatu waweza kuzurura mji mzima mwisho ukalala stendi
Duuh hii ni fursa kabisa.
Na uzuri wa wa maeneo Kama yale wateja wake hawana mbwembwe kudai AC au vitanda vikubwa.
Unajenga nyumba ya kawaida tu na unapata wateja.
 
M naona kama unataka pesa wekeza kweny Lodge au nyumba za wageni ali maarufu kama gest House hii naamini haiangushani sana kama hizo za mwezi
Katika wote walioongea Point kuhusu kujenga Nyumba za Kupangishaa wewe ndo umenena Mkuu...tena jenga karibu na stand aiseee...[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]Utapiga pesa balaaaa hiyo mil 150 itarudi ndani ya mwaka tu mamaee..
 
N16,

Asante sana kwa angalizo muhimu. Hilo ni tatizo kubwa sana kwetu waafrika. Kabla ya kufanya biashara hua hatufanyi feasibility study. Hata wakati biashara inaendelea hatufanyi quarterly reviews. Mambo haya haya tunafanya kazini lakini kwenye biashara zetu wenyewe hatufanyi.

Karibu kil amtu nnaemfahamu alieenda kufanya kilimo mororgoro na iringa alipata hasara - almost wote. Sababu ni kwakua uamuzi wa uwekezaji walifanya holela wakiwa bbar wanakunywa wanasimuliwa theories wana inject mitaji
 
bonna,
umeongea pointi sana..
hasa hapo kwenye nyumba za kuishi mawazo yetu yamefanana
 
Nahisi kuna mambo kadhaa yanaachwa kwenye huu mjadala.

1: Nyumba ya kuishi Vs Nyumba ya Kupangisha.

Nyumba ya kuishi : Hapa watu tumetofautiana malengo kwenye maisha.., ukielewa hili wala hutopata tabu., mimi nimekua na ndoto zangu kua nyumba ntakayoishi lazma iwe na swimming pool..lazma iwe na uwanja mkubwa..garden..parking ya maana n.k, hivyo nimekua mkubwa nimejenga hivi lakini nje ya mji kidogo...kwangu mimi ..nimetimiza ndoto..na kila nikilala nikiamka...naona fahari., sasa ukiniambia nikakae sinza mfano..kwenye kijumba kama kiota cha ndege kisa tu nakaa mjini ...siwezi kukuelewa..sana sana ntakuona una shida na umaskini.., huu ni upande mmoja wa kuangalia hili suala..., watu wanajenga kwa sababu mbalimbali...wengine wana ndoto za kuishi maisha flani hivi..wengine wana familia kubwa hawawezi kupangisha chumba na sebule . n.k

Nyumba ya kupangisha: Pia kwenye hili ....inabidi tuwaze zaidi.., Wapo wanaoona hii ndo biashara salama ..hawataki stress za biashara...., ukijenga nyumba kwa mil 100, ukiwa unapokea kodi laki 5 kila mwezi...ukiwa unaila hii pesa..., tatizo liko wapi.,? kuna tofauti gani kama ungekua na hii 100mil na wewe uwe una withdraw kidogo kidogo kwenye account?

Pili: kwa wale wenye watoto., kuna njia gani safe zaidi ya kumpa kianzio mwanao zaidi ya real estate? ..mimi ninae jenga..unajuaje kama nimewajengea wanangu...baada ya hio miaka 20, wao watakua vijana na ndo wataanza ku enjoy? cha kuelewa hapa ...sio kila investment mtu anayofanya ni kwa ajili yake....

Swali la kizushi : Nyie mnaoona fahari kua mnapanga tu...hao wenye nyumba wenu wangekua na mawazo kama yenu ..mngekua mnaishi wapi?

Hitimisho: Tusijazane upepo wala kutiana ujinga... mwisho wa siku Nyumba/Kiwanja (kwa ajili ya biashara) ndo best way ya kuhifadhi pesa .., ila kwa anaetaka biashara yenye kurudisha faida haraka haraka..hio sio investment sahihi kwake.
umeongea pointi sana..
hasa hapo kwenye nyumba za kuishi mawazo yetu yamefanana
 
Ni kinyume na ushauri wa Mfalme Suleiman aliyesema "Imarisha shamba lako kabla ya nyumba yako"
Ni vizuri mtu ujenge mahala pakuishi kwanza then uje na ujenzi wa nyumba za kupangisha...na tena nyumba za kupangisha iwe ni unajega ghorofa hata floor mbili tu ili uanze kukusanya haraka kodi, pia nyumba za kupangisha kama upo eneo ni zuri usitumie gharama kubwaa kujenga maana itakuchukua muda kurejesha,
 
Kwa taarifa yako hamna watu wame invest Properties kwenye PRIMARY AREAS kama wahindi, ila wako very strategic. We angalia toka Askari monument, Samora Avenue mpaka unafika Clock Tower ni majengo mangapi ya wahindi ndio utapata jibu
Wahindi wengi nchini hawamiliki nyumba ila wamefikia utajiri wa kutisha. Sisi wabantu tunakimbilia kujenga Mapinga, sijui Mkuranga watoto tunawapeleka st.kayumba bado utegemee maajabu maishani
 
Hicho Kitabu naweza pata soft copy yake ?
Mkuu kuna kitu haujui kwenye real estate business.., nayo ni Other Peoples Money.., pia kitu kinaitwa Property Ladder..

Moja hakuna mtu wala sio busara kujenga nyumba kwa cash au pesa yako.. (it takes long kwa return on investment)

Hivyo basi katika hii real estate.., mtu anakopa benki anajenga nyumba hata ikichukua miaka 20 kurudisha ile pesa, hajengi moja..., hio aliyoshajenga anaiombea mkopo benki anajenga nyingine na nyingine na nyingine hii miaka 20 inakuwa sio ya kupata pesa ya kula bali wapangaji ndio wanaomnunulia hizo nyumba.., after the end of 20 years anakuwa amejenga nyumba bila kutumia senti yake hata moja.. (thus other peoples money)... na property ladder unaanza na nyumba moja unakopa unajenga ya pili, tatu, nne n.k.

Cha maana ni Location, Location, Location na sio muda wa kumaliza hio investment.., Walijisemea wachina wote tungetaka kupata kivuli cha miti tunayopanda hakuna mtu angepanda mti..., 20 years in nothing if someone else is paying..

nakuacha na msemo mwingine "As Safe as a House..."
 
1.Kwenye hiyo 150m angeweza kuweka Fixed Deposit ambapo kwa sasa hivi kama ni mzuri ktk bargaining anaweza akapata 13% ingawa competitive rate iko kwenye 11% mpaka 12% ambayo inamhakikishia more than 15m kwa mwaka

2. Anaweza akaweka FD ya hiyo 150m akaendelea ku enjoy interest ambapo ile Fixed Deposit Receipt/Certificate anaweza akaitumia kama collateral na kwa taratibu za kibenki FD ya Tshs 150m anaweza kupata mkopo wa Tshs 120m. Ambazo hizo 120m anaweza kujenga apartment units 2 au 3, anakuwa na double income(interest + rent)
Mara nyingi Mortgage loans huanzia miaka 5 mpaka 15 hivyo installments zake zinakuwa ndogo ndogo sana ambazo zinaweza kukufanya ktk miaka 5 zile units 2 au 3 na ile Fixed Deposit zikajiongeza ukawa una uwezo tena wa kuongeza unit nyingine
Utakuwa unaenda hivyo mpaka miaka 10 unajikuta una 5 au 6 units
Yaani kadri Mortgage outstanding amount inapopungua ndipo unapopata nafasi ya ku renew mikopo na kuongeza apartment unit nyingine
Suala la location ni muhimu sana unaweza chagua location za Uswazi ukajenga kwa gharama nafuu na wapangaji wengi, vyumba vingi nk
Au unaweza jenga sehemu za Kishua nyumba zenye gharama, wapangaji much knower wasiotabirika, na bei zisizotabirika za kodi. Tatizo la maeneo haya ya kishua uchumi ukitikisika kidogo kama hivi sasa rent nazo zinatikisika kitu ambacho huku Uswazi hakuna kwa sababu watu wanaoshindwa kulipa kodi Ushuani ndio hao hurudi huku kwa akina Yahe. All in all kuwa na mbinu madhubuti na kujua who is the right Financier ni kitu cha muhimu sana. Sio kila bank iko friendly ktk Mortgage Financing, unaweza kuta out of 58 registered banks tulizonazo ni 3 au 5 ndizo ziko friendly katika Mortgage Financing

Kwa maoni yangu mimi biashara ya nyumba mtaji wa chini kabisa unatakiwa uwe nao ili biashara ikuwe, watoto wasikose nyama, na loan installments zilipwe vizuri basi usipungue Tshs 350m
 
Back
Top Bottom