Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Ni kweli

Ijapokua rais Mwinyi alifungua milango mwaka 1985 na sasa ni miaka zaidi ya 30 imepita nadhani athari hizo zinatakiwa ziwe zimefifia bynow

Miaka 30 ni michache sana kuweza kufanya Watu wasahau madhila waliyopata kutokana na kutaifishiwa nyumba zao.Kumbukumbu hii mbaya kabisa ya kunyang'anywa nyumba Watu wengi bado wanayo akilini mwao, wazazi wangu pia ni wahanga wa tatizo hili.Mpaka Leo bado wameendelea kukumbuka nyumba zao mbili walizonyang'anywa, bado hawajasahau KWA sababu walijinyima sana mpaka wakafanikiwa kujenga hizo nyumba.
 
600,000 × 12 = 7.2m kwa mwaka.
150m ÷ 7.2m = 29 years ili pesa yako irudi. Hapo hijaweka hata senti tano ya services and replacements na usumbufu wa wale wapangaji jeuri.

Tuone kama utaweka fixed acc kwa walau 8% interest kwa mwaka.

8% times 150m = 12m
Kwa miaka 29 = 348.

After 29 years tuna watu wawili hapa baba mwenye nyumba na huyu Mzee wa fixed account...Haya wachumi tusaidieni hapa nani kapata zaidi?

Mmoja ana nyumba yake na mwingine ana 348m + 150m

Nani mjanja?? Wekeni na approx land value baada ya hiyo miaka 29.

Mjenzi ana nyumba 150m + vakue ya kiwanja after 29 years.
Mbona mnatupigia hesabu za UPE(Ualimu pasipo Elimu)? Yaan kwa miaka 29, kodi itakuwa hiyohiyo laki 6? Haiongezeki? Ni nani hapa amewahi kupanga nyumba na kulipa kiasi kile kile kwa miaka hata 5?

Inawezekana hii biashara ya nyumba za kupanga haina faida kivile. Basi tuipinge kwa hoja za kweli, sio za kuungaunga.
 
Kwa ujenzi huo ndo umpangishe mtu laki 6 Kwa mwezi?
Waulize wenzako chumba kimoja,choo,kijiko na sebule wanalipa shilling ngap dar? Ni kuanzia laki 2 na kupanda tena kama ipo karibu na mjini hiyo hiyo laki 4 na ni chakavu kabisa na watu wanapanga,wewe unasemaje kwani?
 
Nyumba ya kupanga ni mwamvuli wa future ya watoto, kwa mfano umetoweka hapa duniani paaah!!!!!, una nyumba zako za kupangisha kama 4 hivi, hapa watoto itakua umewawekea ulinzi wa uchumi
 
Hii biashara kichaa sio ya Kufanya kwa kutumia hela ya Mkopoo utakufa mawazooo...!! Una hela yako huna nayo kazii fanya hivii

Ni kweli mkuu. Hela ya ziada ndio yakufanyia haya mambo sio mkopo au NSSF
 
Nyumba ya kupanga ni mwamvuli wa future ya watoto, kwa mfano umetoweka hapa duniani paaah!!!!!, una nyumba zako za kupangisha kama 4 hivi, hapa watoto itakua umewawekea ulinzi wa uchumi

Siyo kwamba ndio umewaachia balaa LA kugombea urithi wa hizo nyumba?
Nyumba ndio itakuwa chanzo cha wao kuuana, kurogana, kugombana, NA kila aina ya vurugu.
 
Hata kupungua pia inawezekana kwa hiyo hiyo lakh 6 ni wastani wa kuongezeka na kupungua. Bado haujajua kuwa kodi ya pango imepungua kipindi hiki cha Jiwe?
Mbona mnatupigia hesabu za UPE(Ualimu pasipo Elimu)? Yaan kwa miaka 29, kodi itakuwa hiyohiyo laki 6? Haiongezeki? Ni nani hapa amewahi kupanga nyumba na kulipa kiasi kile kile kwa miaka hata 5?

Inawezekana hii biashara ya nyumba za kupanga haina faida kivile. Basi tuipinge kwa hoja za kweli, sio za kuungaunga.
 
Achana na hao
Nenda kwenye makampuni makubwa ya kibiashara Vodacom airtel benk n.k
Wote hawa huishia kupanga tu na sio kujenga mzee
Ujenzi ni dead project Mzee
Leo tunalaumu mifuko ya hifadhi za jamii kwakuwa mapesa yote wamepeleka kwenye maujenzi
Mojawapo ya demand for the 'stimulus package' pale USA ilikuwa ni wadau kuchukua pesa yao na kuizamisha kwenye ujenzi
Pata hela fanya biashara huwezi tia kwenye fixed account au kanunue hisa huko
Huwezi hayo yote ni bora upige tu chipsi zege na mayai na kuku sio ujenzi mkuu
Ujenzi iachiwe serikali yenyewe kupitia NHC na wenzako na magharama yao yasiyohimirika

Point nzuri sana

Mashirka makubwa yenye uwezo kama Tigo na Voda, NMB nk hawajengi nyumba za kuishi maxpatriates - wanapanga. Lazima kuna maana kubwa katika hii strategic decision
 
Usikope kuanzisha mradi ama biashara, kopa ili kuendeleza....si maneno yangu bali ni maneno ya kijana wangu mmoja aliepo makao makuu CRDB.

Mimi ni nani hata nikope bank, wacha nife maskini tu.

Hekima kubwa sana hiyo mkuu
 
Hakuna kanuni inayowafaa watu wote kwa wakati mmoja. Wako watu wataona real estate ni dili, wengine wataona ufala.
Nitoa mfano. Ili ufanikiwe mwenye biashara unahitaji usimamizi wa karibu sana. Kama unamiliki biashara ya baa, kila siku asubuhi unahitaji kwenda kupiga hesabu na kukagua ili mhudumu wa kaunta asiingize stock yake. Pia jioni uwepo ili wahudumu wachangamkie wateja.. Ndo kusema huwezi kufanya shughuli nyingine maana panahitajika micromanagement.
Biashara hii ya baa haimfai mfanyakazi anayetaka kujiongezea kipato kupitia chanzo kingine. Mfanyakaz nyumba ya kupangisha yaweza kumfaa maana usimamizi wake ni kila baada ya miezi 3/6/12. Pia mfanyakazi ni rahisi kujenga maana hahitaji dhamana ya kitu ili kupata mkopo. Hata akifa, warithi hawadaiwi.
 
Mimi wife ananiboa anaponiambia tujenge lijumba wakati mtaji wa kujenga nyumba naimarisha shamba langu la ng'ombe

Ng'ombe unauza maziwa unapata mahela bado ng'ombe yupo ndama yupo na mbolea juu.

Miradi inalipa sio majumba sijui ni matakataka gani na kaahidi tutaachana kama sitajenga

Mimi ndio kwanza nanunua ng'ombe mwingine na wengine watatu wanazaa next month yeye ananiletea mambo ya majumba

Bili ya lita mbili nakaa mjengo wa heshima hapa mjini

Nashuri uchumi ufundishe kuanzia std III

Wanawake wanapenda sana nyumba kwasababu wazazi wao wanawa pressure na wao wanapenda sana kuridhisha wazazi
 
Point nzuri sana

Mashirka makubwa yenye uwezo kama Tigo na Voda, NMB nk hawajengi nyumba za kuishi maxpatriates - wanapanga. Lazima kuna maana kubwa katika hii strategic decision
Sasa expatriate umjengee masaki or mikocheni ni sh ngapi?.kiwanja plus nyumba ya hadhi yake?
Rental ina faida kwa mda mfupi na haihitaji hela nyingi tofauti na kujenga hadi umalize
 
Mbona mnatupigia hesabu za UPE(Ualimu pasipo Elimu)? Yaan kwa miaka 29, kodi itakuwa hiyohiyo laki 6? Haiongezeki? Ni nani hapa amewahi kupanga nyumba na kulipa kiasi kile kile kwa miaka hata 5?

Inawezekana hii biashara ya nyumba za kupanga haina faida kivile. Basi tuipinge kwa hoja za kweli, sio za kuungaunga.

Mkuu uko makini. I like your attention to details
 
Hakuna kanuni inayowafaa watu wote kwa wakati mmoja. Wako watu wataona real estate ni dili, wengine wataona ufala.
Nitoa mfano. Ili ufanikiwe mwenye biashara unahitaji usimamizi wa karibu sana. Kama unamiliki biashara ya baa, kila siku asubuhi unahitaji kwenda kupiga hesabu na kukagua ili mhudumu wa kaunta asiingize stock yake. Pia jioni uwepo ili wahudumu wachangamkie wateja.. Ndo kusema huwezi kufanya shughuli nyingine maana panahitajika micromanagement.
Biashara hii ya baa haimfai mfanyakazi anayetaka kujiongezea kipato kupitia chanzo kingine. Mfanyakaz nyumba ya kupangisha yaweza kumfaa maana usimamizi wake ni kila baada ya miezi 3/6/12. Pia mfanyakazi ni rahisi kujenga maana hahitaji dhamana ya kitu ili kupata mkopo. Hata akifa, warithi hawadaiwi.

Angalizo lako nila muhimu sana
 
Wanawake wanapenda sana nyumba kwasababu wazazi wao wanawa pressure na wao wanapenda sana kuridhisha wazazi
Nyumba inaleta security kwa familia
Mnakua huru hata kama hamna kipato
Sio kwa sababu ya wazazi

Mwanamke unakua free nyumbani kwako
Unapendezesha hata weeekend jumuiya na nini au shoga zako waje kikao cha kikoba ujinafasi

Kwenu mnaweza kupaendeleza kupakarabati nk...si kwenu bwana

Kwa hio mmezaa watoto bado hamjipangi hata kununua kiwanja muwe na kwenu?..

Jmn heshimuni nyumba ya familia usiolipia hata 100...ni kwakoo...hata watoto wakikua hawajakaa sawa wana pa kuanzia maisha

Mkiwa watu wazima vipato vikayumba mna pa kukaa
Mtu hadi miaka 60 upange we muhindi?..
 
Waulize wenzako chumba kimoja,choo,kijiko na sebule wanalipa shilling ngap dar? Ni kuanzia laki 2 na kupanda tena kama ipo karibu na mjini hiyo hiyo laki 4 na ni chakavu kabisa na watu wanapanga,wewe unasemaje kwani?
Sio Dar ninayoijua makazi holela kibao-kodi mpaka elfu 5/chumba/mwezi, middle-class ni ndogo sana (changa) na wengi wameeelekea dom (saudia). Tuendako wengi wenu mtarudi vijijini
 
Mimi huwa naamini nyumba hazipandi thamani bali hela yetu inashuka thamani na kusababisha vitu kuwa ghali hivyo nyumba nayo inapanda bei. Ibadili kwa dollar ndio utajua huwa haipandi bei
Safi sana mkuu,

Yani Hilo somo watu hawelewi na hawatakuja kuelewa, wanapoona enzi hizo nyumba kariakoo inauzwa 30,000/= wanalaumu babu zao kwa nini hawakununua, Yani wanasahau kabisaaa inflation na kwamba ukifactor hiyo kitu utagundua Bei haijabadilika

Hiyo nyumba unayosema utauza kwa milioni 300 baada ya miaka 20, purchasing power ya hiyo pesa itakuwa ndogo au sawasawa na mil. 150 ya wakati huu
 
Back
Top Bottom