Hakuna kanuni inayowafaa watu wote kwa wakati mmoja. Wako watu wataona real estate ni dili, wengine wataona ufala.
Nitoa mfano. Ili ufanikiwe mwenye biashara unahitaji usimamizi wa karibu sana. Kama unamiliki biashara ya baa, kila siku asubuhi unahitaji kwenda kupiga hesabu na kukagua ili mhudumu wa kaunta asiingize stock yake. Pia jioni uwepo ili wahudumu wachangamkie wateja.. Ndo kusema huwezi kufanya shughuli nyingine maana panahitajika micromanagement.
Biashara hii ya baa haimfai mfanyakazi anayetaka kujiongezea kipato kupitia chanzo kingine. Mfanyakaz nyumba ya kupangisha yaweza kumfaa maana usimamizi wake ni kila baada ya miezi 3/6/12. Pia mfanyakazi ni rahisi kujenga maana hahitaji dhamana ya kitu ili kupata mkopo. Hata akifa, warithi hawadaiwi.