Je! Ni Conte au Mourinho FA Cup?

Je! Ni Conte au Mourinho FA Cup?

Kudo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2017
Posts
1,821
Reaction score
6,119
Habarini Chiefs

Binafsi tangu mwanzo timu hizi zilipofuzu kuingia semi final ya FA cup nilishindwa kujua nani hasa ataweza kuchukua hiko kikombe,kulingana na aina ya uchezaji wa timu zote

Tumeshuhudia timu zote zikiwa zinapata Matokeo tata kwenye misimu miwili ya Epl,huku mourinho akiwa na kikosi kizuri lakini aina ya mbinu zake imekuwa ni kero kwa mashabiki wengi wanaopenda soka safi la akili na uwezo wa wachezaji,huku Conte akiwa na kikosi kinachotegemea zaidi timu pinzani kuamka na bundi gani ili wao wapate matokeo,huku kila mara akionekana kupanga kikosi kinyume na matarajio ya wengi,

Je enyi wapenda soka jumamosi hiyo kabla haijafika unahisi nani atakuwaa mbabe wa mwenzie

Nb mechi hii sitegemei iwe na magoli mengi kutokana na aina za uchezaji wa timu zote mbili
 
Mimi ninachojua ni kwamba Conte ashinde F.A cup au asishinde atafurumushwa mapema tu mara baada ya fainali na mmiliki wa timu.
 
Mimi ninachojua ni kwamba Conte ashinde F.A cup au asishinde atafurumushwa mapema tu mara baada ya fainali na mmiliki wa timu.

Lakini hadi sasa hapana tetesi zozote juu ya hilo ama huoni kama wanaeza mpa muda tena maana kama mafanikio aliwapa msimu uliopita!?
 
mourinho ni tactician ambaye anaamini kwenye ulinzi.amekuwa akizikomesha timu nyingi ambazo ni offensive
 
Back
Top Bottom