Ni biashara nzuri sana kama ukinunua gari mpya, gari kama Eicher hurudisha hela kati ya miaka 1 na miezi 8_ 2yrs. Na ukiiangalia gari iliotumika miaka 2 ni bado iko poa sana! Mimi nina Eicher yenye miaka 3.9 mpaka sasa, huwa IPO servs j.Pili tu na siku zote za kazi IPO barabarani. 130,000 @ day"
Nakuhakikishia mkuu inafaida!
Wanaofilisika ni wale wanaonunua magari second hand, gari limetumika mtu karudisha hela yake na kapata na faida akiona tu injini linaanza kupungua nguvu hasubiri kufanya overhall, analiuza anapata faida zaidi na ananunua jipya lingine, anaeenda kuumia ni mnunuaji ambaye baada ya muda labda miezi 6 ya kupata hela vzr,
Linaanza season ya natengeneza mengi makubwa yanayohitaji hela nyingi na kama hakua amejipanga ndo hao wanaofilisika'
Na anaweza sema kalogwa kwsbb kila akitengeneza hiki kiazuka kile! MB🙁kwenye gari ukiona injini imechoka ujue vitu vingi vikubwa navyo vitafuatia!)
Na kitu lingine ktk daladala ni hesabu, ukiwa kubwa gari inachoka haraka sana na gari zenye hesabu ndogo ndo zile unaziona mchana imepaki wanakula,
Usiku unakuta imeoshwa vzr imepaki mapema na inakuwa haina Shida sana na trafiki (vyeti) ksb haina sababu ya kuvunja sana sheria za barabarani.