Biashara ya daladala ukiifanya kistaarabu inavyotakiwa in hasara.Nauli sio realistic zimepangwa kisiasa kuwafurahisha wananchi.Serikali inammudu kuthibiti nauli lkn sio bei ya mafuta na vipuli hivyo gharama za uendeshaji zipo juu sana. Wamiliki ili wapate faida wanaifinyanga biashara utaona hakuna ajira Ila hesabu ya siku, kujaza abiria kuliko kiwango,kutozingatia sheria za barabarani ili trip ziwe nyingi, konda na dreva kufanya kazi masaa mengi dei worker nk Jiulize ni sawa nauli ya daladala kuwa ndogo kuliko hata bei ya maji au soda, MTU anatoka Tegeta mpaka Mbagala kwa nauli ambayo haifiki hata elfu moja.Hata Mwendo kasi wasiporuhusiwa kutoza nauli zinazokidhi gharama baada ya muda watafilisika au ndio kama hivyo tumeanza kusikia malalamiko ya kujaza kupita kiasi