Je, ni kwanini Ugonjwa wa Kansa, Figo, Ini unaonekana kuwa ni tatizo Tanzania ?

Mada nzuri sana, pia usisahau na viuatilifu, dawa za kuua wadudu mashambani, zinazopigwa kwenye mazao kama nyanya, matango, cabbage, karoti, matikiti, parachichi, matunda aina zote na mboga mboga! Dawa za kuua wadudu zinachangia sana kueneo kwa saratani!

Pia dawa za kuhifadhia samaki na hata nyama zisiharibike kwenye majokofu! Wengine wanahifadhia dawa za maiti isiharibike!

Bila kusahau madawa na chanjo za mifugo kama kuku, bata, kanga, kware, sungura, mbuzi, ng'ombe na nguruwe! Hawa wanyama wanapewa madawa mengi sana ya kuwanenepesha haraka hata kupewa dawa za kupunguza makali ya H.I.V yaani ARV's na pia chanjo za kuzuia magonjwa ambazo nyingine ni hatari kwa afya ya mlaji...!

Kwakweli watanzania tunalishwa sumu nyingi sana! Mungu tu atusaidie!

Adios Amigo!
 
Ni tatizo la dunia
 
Duuh
Duuh,tuvute Jamaa zako tusiangamie Mkuu!Tuje Canada.
 
Unalima kama wazee wako?
Unatembea kama wao ama kila sehemu lazima uende na gari??

Waliandaa nafaka zao wenyewe
Tofautisha mbege (natural) na spirits hizi kali sijui Hennesy sijui Kvant
Lifestyle ni tatizo
Mtu akiwa na hela anakuwa limbukeni badala ale vitu natural zaidi
 
Dokta, bandiko lako ni very sensitive lakini limekosa hata quotes 5?, sasa sisi vijana wenu wa veta wataandikaje?
 
Supermarket ni pa kununua dawa za washroom na tissue paper
Tununue vitu fresh masokoni
Ngano ni ya kupunguza kama sio kuachana nayo kabisa
 
Huu ndo mtihani mkubwa mana tunaelezwa tule natural
Vya natural vyenyewe sasaaa🙌🏽
 
Mkuu umepiga mle mle.
KILIMO: Viatilifu vinavyotumika mashambani ni fake, lknkuna swala la hili la kilimo biashara ambapo mkulima anataka kuzalisha zaidi kwa gharama ndogo ,hii hupelekea kutumia madawa zaidi, mfano 2-4-D kemikali inayosemekana kuwa kisababishi cha kansa. Usiombe uone kilimi cha nyanya, viazi mviringo, tikiti , hutatamani ule.

MIFUGO: Inafugwa na kunenepeshwa kwa vitu visivyo , kuanzia kuku, na wanyamwa wa kuchinjwa
MADAWA: Dawa sub standard zinaingizwa na mamlaka zipo tu,nakumbuka mtu aliyekamatwana madawa fake ya kilimo utajiuliza yalipitaje?
GMO: Huko vijijini sasa mbegu za zamani hazipo tunatumia mahindi kwa mfano ya kulima mara moja huwezi kupanda generation ya pili
Yapo maembe ya ajabu yanapata matunda mara 2 au 3. Imeisha, nilishangaa kuona embe linabeba tunda likiwa urefu wa sm 20,(very drwalf) Huzi tasisi zetu kazi kubariki tafiti za watu wengine wa nje bila kujihoji.
MTINDO WA MAISHA. Ujinga umeenea kwenye jamii usiopimika ukiuliza kwanini unakunywa hiyo energy drink unapata nini? Eti ni sifana heshima, wakati namna za maisha zimebadilika,kazi na shughuli za maisha watu wanashindwa kubadili wale na wanywe nini? Wengi wanapata uzito usio na maana, vyakula vilivyosindikwa au kuondolewa virutubisho, halafu serkali imeruhusu kuondoa vorutubisho bna baadae kufanya fortification so what?.
MAMLAKA ZA KUTHIBITI UBORA. Hizi ni kama hazipo
Sasa serkali itatumia hela nyingi kutibu magonjwa yasiyoambukizwa kuliko ya kuambukizwa.
Anyway tujiandae kila mmoja ni mtahiniwa wa hayo ila unaweza kupunguza. Tumia akili
 
Mafuta ya Alzeti yamekuwa promoted sana ila nayo ni tatizo
Mi natumia Butter tu sikuhz
Ni kweli mafuta mengi tunayotumia hutuletea shida yakiwemo na hayo ya alizeti, mafuta mengi tunayotumia tunapata omega 6 kwa wingi zaidi kuliko omega 3. Hata hiyo Butter hufaa ile ya asili kuliko ya kugandishwa viwandani.
 
Ni kweli mafuta mengi tunayotumia hutuletea shida yakiwemo na hayo ya alizeti, mafuta mengi tunayotumia tunapata omega 6 kwa wingi zaidi kuliko omega 3. Hata hiyo Butter hufaa ile ya asili kuliko ya kugandishwa viwandani.
Natural butter napata wapi hapa TZ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…