Je, ni kweli asilimia kubwa ya watu mashuhuri na matajiri kwenye hii dunia, utajiri wao sio wa halali au umetokana na mambo ya kichawi au Masonic?

Je, ni kweli asilimia kubwa ya watu mashuhuri na matajiri kwenye hii dunia, utajiri wao sio wa halali au umetokana na mambo ya kichawi au Masonic?

commm

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2019
Posts
1,709
Reaction score
1,963
Bhasi habari za wakati huu wana JF wote poleni na hongera katika kuendelea kupambana na hizi changamoto za haya maisha.

Bhasi bhana leo nikiwa naendelea na mapumziko ya sikukuu hiii ya Christmas.

Huku nikiwa nina uchovu wa ajabu nikasema siku ya leo sio mbaya nikatumia na wadau wangu wa hapa mtaani katika kubadilishana mawazo labda huenda nikapata jambo jipya la kujifunza.

Niende moja kwa moja kwenye mada ni kwamba hawa jamaa zangu walikua wanajadili mada ya kuwa hakuna tajiri yoyote kwenye hii dunia na Tanzania hapa ambaye anaendesha utajiri wake pasipo kuhusisha na mambo ya kichawi au MASONIC State.

Jambo ambalo kwa upande wangu nilijaribu kuwapinga nikasema, kweli wapo lakini kuna wengine utajiri wao ni wa halali kabisa.

Lakini wao walijaribu kupinga na kusema wachezaji maarufu kama C. Ronaldo, L. Messi eti na Bill Gates ni watu ambao wanahusika au utajiri wao unaendeshwa na hawa Masonic.

Na kwa hapa Bongo walijaribu kuwataja wasanii maarufu pamoja na matajiri maarufu wakisema katika utajiri wao kuwa na Imani za kishirikina.

Sasa hawaaa jamaaa nimejaribu kuwaapuuza kwa kuona kama ni propaganda fulani hivi, na kutokana wao wenyewe bado hawana maisha, sasa wanajaribu kuhusisha kila aliyefanikiwa na mambo ya kichawi.

Je, ni kweli kwamba asilimia kubwa ya watu wenye mafanikio kwenye hii dunia bhasi hutumia ushirikina katika kuendesha utajiri wao?
 
Asilimia kubwa inaqnzia ngapi na unaweza kuthibitisha uchawi upo kweli?
Mkuu mimi nimewauliza nyie mnipe maoni yenu.

Kuhusu uchawi mimi ninaaamini upo kwa asilimia 100.
 
Na nukuu " TAJIRI KUUONA UFALME WA MUNGU NI HERI NGAMIA KUPENYA KWNY TUNDU LA SINDANO YA MKONO....nadhan umepata concepts
 
Hayo ni mawazo ya Masikini, kuhalalisha Umasikini, Kwa kuona kwamba ni haki yao kufa Masikini Kwa kuwa eti bora wafe Masikini kuliko kuingia Freemason kitu ambacho ni story za Vijiweni zilizokuzwa na Magazeti ya Udaku!

Hivi Messi au Ronard wana U Masonic gani jamani!? Tunawaona kila week wakicheza mpira Kwa Viwango vya juu, tunajua mpaka mishahara yao Kwa week! Ni Masikini wa Akili tu anaweza kuamini hili.
 
Mkuu mimi nimewauliza nyie mnipe maoni yenu

Kuhusu uchawi mimi ninaaamini upo kwa asilimia 100
Unaamininuchawi upo au unajua uchawi upo?

Kuamini ninhaki yako ya kikatiba, unaruhusiwa kuamini hata uongo.

Uchawi ni nini?

Unaweza kuthibitisha uchawi upo kweli?
 
Sio lazma awe mchawi au masonic,lakin wengi n wauwaji au wadhurumaji,mfano ibramovic wa Chelsea,bill gate na wengne wengi.
 
Unaamininuchawi upo au unajua uchawi upo?

Kuamini ninhaki yako ya kikatiba, unaruhusiwa kuamini hata uongo.

Uchawi ni nini?

Unaweza kuthibitisha uchawi upo kweli?
Mkuu naona kama unataga ligi hivi.

Mimi kuna vitu ambavyo vimeshanitokea kwenye maisha yangu na kusababisha maisha kuyumba kwa kiasi kikubwa ni kwa sababu ya uchawi,
So mimi naongea kutokana na experience yangu, ila sikushawishi wewe uamini kama hivi vitu vipo.
 
Moja ya kitu Mungu alimwagiza mwanadamu ni kuja kutawala mali na rasilimali zote zilizopo duniani. Ole wako usiwe na mali utakua umekaidi amri ya Mungu..na unajua kiburi ni chukizo mbele ya Sir.
Ndio uone biblia inakupiga kila "Engo"😀
Na nukuu " TAJIRI KUUONA UFALME WA MUNGU NI HERI NGAMIA KUPENYA KWNY TUNDU LA SINDANO YA MKONO....nadhan umepata concepts
 
Back
Top Bottom