Katika ukristo kitendo chochote cha kutafuta msaada wa rohoni au mwilini kwa kupitia nguvu nyingine mbali na nguvu za Mungu, biblia inakiita Uchawi,…Na ni wazi kuwa hakuna nguvu nyingine iliyo kinyume na Mungu zaidi ya nguvu za shetani, Na uchawi kwa ujumla umebeba mambo mengi, kuloga, kuagua, kutazama utabiri wa nyota, kubashiri, kusihiri, kuabudu sanamu, hata kuamini baadhi ya movie au magemu ambayo yanatoa maagizo fulani kukuaminisha kuwa unaweza kupata maelekezo ya maisha yako mbali na nguvu za Mungu ni uchawi n.k. vipo vingi, kwa ujumla vyote hivyo vinaitwa uchawi.
Kumbukumbu 18:10 “Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.’’
Ufunuo 22:14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.
15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.
Ufunuo 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.”