Je, ni kweli asilimia kubwa ya watu mashuhuri na matajiri kwenye hii dunia, utajiri wao sio wa halali au umetokana na mambo ya kichawi au Masonic?

Unahakikishaje vitu hivyo vilitokea kwa sababu ya uchawi, na si kwamba wewe unafikiri tu vilitokea kwa sababu ya uchawi?

Kwanza hata huja define uchawi ni nini.

Uchawi ni nini?

Unajuaje unachofikiri uchawi ni uchawi kweli na si kitu ambacho hukifahamu tu?
 
Mimi sibishani na wewe kwa sababu kila mtu ana mapito yake kwenye haya maisha.

Sijasema hivyo ili nikuaminishe kama uchawi upo

Ila mimi nitaendelea kuamini kuwa uchawi upo mpaka kesho
 
Hawezi kukujibu huyo.kiranga heshima yako
 
Bila uthibitisho, katika chochote, hakuna hoja.

Kuna imani tu.

Imani si hoja.
Kwa mfano wewe umethibitisha kitu ila mim sijathibitisha. Je, hicho kitu kitabadili ukweli halisi kuwa si cha kweli kwa vile mim tu sijathibitisha?
 
Na nukuu " TAJIRI KUUONA UFALME WA MUNGU NI HERI NGAMIA KUPENYA KWNY TUNDU LA SINDANO YA MKONO....nadhan umepata concepts
Mkuu hii nukuu umeinukuu kutoka kwenye nini/kwa nani?[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Naomba uamini ya kwamba UTAJIRI wa mtu huja tu wenyewe wakati mwingine bila hata yeye kutarajia na baada ya hapo inabaki maarifa na juhudi zake kutunza na kuendeleza huo utajiri

Maswala ya uchawi na masonic wakati mwingine ni mambo ya kufikirika tu na watu wa hivyo ni wachache sana sana

Pia, si wengi sana duniani watakao pata utajiri,hivyo unaweza lazimisha kwa uchawi,ujambazi,huo sijui umasonic na bado ukaishia umaaikini tu

Wewe endelea na mishe zako kwa kulidhika kabisa bila tamaa na kama ipo itakuja tu,kama haipo utaishia kua kama ulivyo
 
Mimi sibishani na wewe kwa sababu kila mtu ana mapito yake kwenye haya maisha.

Sijasema hivyo ili nikuaminishe kama uchawi upo

Ila mimi nitaendelea kuamini kuwa uchawi upo mpaka kesho
Unaruhusiwa kuamini unachotaka.

Hiyo ni haki yako ya kikatiba.

Mimi siingelei imani, naongelea facts.

Umeshindwa hata ku define uchawi ni nini, achilia mbali kuthibitisha uchawi upo.
 
Kwa mfano wewe umethibitisha kitu ila mim sijathibitisha. Je, hicho kitu kitabadili ukweli halisi kuwa si cha kweli kwa vile mim tu sijathibitisha?
Mosi.Unathibitisha vipi mimi nimethibitisha, na sifikiri tu kwamba nimethibitisha?

Hili moja.

Pili, mimi nikithibitisha, kiukweli, kitu ambacho hakina ubishi, kwa mfano, square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2, na wewe usipokubali hilo, wewe kutokubali hakubadili ukweli.

Lakini, hapo tunarudi mwanzo kwenye mosi.

Kuhakiki kwamba, je, ni kweli square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2?

Kuhakiki hivi ni muhimu, kwa sababu, mimi kusema tu square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2 hakufanyi hilo liwe kweli.

Sasa hapo ndipo tunakuja kwa watu wanaosema uchawi upo.

Wanathibitisha vipi uchawi upo?

Kwa mtu asiyejua Chemistry, sumu inayoua kikemikali inaweza kuitwa uchawi.

Mababu zetu walioishi miaka 200 iliyopita walipoona wazungu wanaua kwa bunduki, waliona huo ni uchawi.

Wangeona redio, internet, TV, utabiri wa haki ya hewa, utabiri wa kupatwa jua leo, wangesema huu ni uchawi.

Sasa wewe unahakikisha vipi hayo mambo unayoyaita uchawi leo si mambo tofauti usiyoyaelewa tu?
 
Ukiipitia ile channel ya "Davistar Mata" kwenye You tube unaweza pata jibu la swali lako straight
 
Sio lazma awe mchawi au masonic,lakin wengi n wauwaji au wadhurumaji,mfano ibramovic wa Chelsea,bill gate na wengne wengi.
Ukishakuwa muuaji ndo uchawi wenyewe huo majini yanakunywa damu.
 
Mimi sibishani na wewe kwa sababu kila mtu ana mapito yake kwenye haya maisha.

Sijasema hivyo ili nikuaminishe kama uchawi upo

Ila mimi nitaendelea kuamini kuwa uchawi upo mpaka kesho
Wewe unayeamini uchawi upo upo sahihi na huyo anayesema uchawi haupo naye yupo sahihi kwasababu uchawi ni IMANI lakini pia uongo una nguvu kuliko ukweli vinginevyo Dunia isingetawalika.
 
Hayo ni mawazo ya cc maskin, hatufanyi kazi tunakaa vijiweni kuwajadili matajir wakati wao wanaendelea kufanya kazi.
 
Unaweza kudefine kajamba Nani ni Nini ?

Tuthibitishie ya kwamba Facebook ni mtandao wa kina Kajamba Nani

[emoji23][emoji23][emoji23]dah
Unajua kusoma kwa ufahamu?

Au unaharisha logical non sequitur tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…