Mimi nawashauri sana wavuta bangi wasipende kukaa vijiweni. Bangi inapenda ukae peke yako uwaze plans zako za kimaisha au kama ni kufanya tafakari inasaidia sana. Bangi inakufanya kuwa mtu wa shukrani, mtu wa amani na inakujenga kiroho kama utaipenda kwa jinsi inavyokupa nguvu ya kuyatazama maisha katika mtazamo ambao ni clear. Bangi inafungua ile power iliyo ndani yako, hata hofu ya kesho inaondoka unaona unakuwa mtu wa matarajio makubwa katika kutafuta ndoto zako.
Lakini tatizo ni moja ukivuta bangi ukakaa kijiweni mnaanza kupiga story ambazo hazina uhalisia kabisa mwisho wa siku mtazungumzia na maisha ya watu tu, ona sasa mnaanza kumzungumzia Bibi ambaye hamna uhakika lakini mnahisi ni mchawi.
Unajua mkuu bangi ni kama amplifier, ukiamini kitu kwa udogo tu au ukiaminishwa utajijengea wazo mpaka utaamini vitu ambavyo havipo. Ona jamaa anavyoamini inafukuza wachawi. Wakati ni imani tu za mtaani.
Niliwahi kuzungumza na jamaa mmoja ambaye amejijenga kiroho sana, ingawa hatumii mjani, lakini anajitahidi kufuata na kuutafuta ukweli wa mambo mengi ya kidunia. Katika mazungumzo nikamuuliza swali kama hili, maana hata hapa jf watu wameuliza swali kama hili mara nyingi mno. Akaniambia viumbe kama majini wanavutiwa na baadhi ya tabia za kibinadamu ambazo sometimes ni anasa, kama pombe, bangi, ngono n.k. Hivyo kama wewe unatumia mjani jua kwamba kuna viumbe wanavutiwa na harufu yake na wanakuwa wanachill na wewe kipindi unavuta bangi.
Vilevile kuna nchi nyingi za kiafrika na huko majuu, waganga na wachawi ( kule nje ya Africa uchawi ni tasnia na taaluma siyo kulogana sana kama Africa) lazima wavute bangi ili wapate stimu ya kupandisha mashetani yao, hata ukiingia mtandaoni vitu kama hivyo utavikuta.
Sasa sijui kwanini waTanzania tumeamua kudanganyana kiasi hiki kuhusu bangi. Mara utaambiwa bangi inafanya uwe kichaa, mara ukivuta bangi punje ya mchele inakuwa jabali, ukivuta bangi ukawa mcheshi na watu, watu wanasema bangi hizo. Yaani mambo mengi ambayo kimsingi hayana uhalisia kabisa.