Uchaguzi 2020 Je, ni kweli Bunge halikuhusishwa kwenye ununuzi wa ndege za ATCL?

Uchaguzi 2020 Je, ni kweli Bunge halikuhusishwa kwenye ununuzi wa ndege za ATCL?

Komeo

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2011
Posts
2,498
Reaction score
1,172
Huko majukwaani tunasikia mengi, lakini mengine nadhani yanafanywa kwa makusudi ya kutafuta kura. Inawezekana ikawa ndio maana halisi ya kampeni kwa tafsiri yetu ya Kibongo tu.

Ukimsikiliza Lissu anasema hakuna mbunge hata mmoja anayejua hata fedha zilizotengwa kununua hizo ndege. Hiyo ndiyo ilikuwa hoja yake kwenye clip hiyo kama umeisikiliza. Halafu baadaye anaonekana Mheshimiwa Halima Mdee akiijadili hoja hiyo akiwa Bungeni. Msinishambulie mimi kwakuwa mimi sio niliyesema hivyo na bahati nzuri nimeweka video yake. Mimi sigombei hata udiwani.
 
Swali ni Je pesa zote zilizopitishwa na Bunge kununulia ndege zimenunulia ndege kweli kwa pesa ileile?

Kuambiwa Bunge limepitisha shilingi bilioni 400 kununulia ndege 3 au 4 haimaanishi pesa zote hizo zilinunulia ndege.

CCM wajibu hili kwa kutuonesha bank transactions kwamba kila ndege walinunua kiasi gani full stop!
 
..hoja siyo kama bunge lilihusishwa au halikuhusishwa.

..Tanzania hatukutakiwa kununua ndege kwasababu shirika la ndege ni biashara ya hasara.

..matrilioni ya fedha tulizotumia kununua ndege ambazo zinatutia hasara sasa hivi, yalipaswa kuelekezwa ktk sekta nyingine zinazogusa wananchi wengi zaidi.
 
Mkuu, hoja ya Mgombea ni kwamba bunge halikuhusishwa kabisa, na ndivyo anavyotueleza wapiga kura wake.
 
Swali ni Je pesa zote zilizopitishwa na Bunge kununulia ndege zimenunulia ndege kweli kwa pesa ileile????

Bunge kuambiwa zimepitishwa shilingi bilioni 400 kununulia ndege 3 au 4 haimaanishi pesa zote hizo zilinunulia ndege.

CCM wajibu hili kwa kutuonesha bank transactions kwamba kila ndege walinunua kiasi gani full stop!
DA yaani hii kitu nilikuwaga sijaisikia kumbe kila kitu kiliptia bungeni kuhusu ununuzi wa ndege kweli chadema ni wapumbavu wanataka kutufanya wajinga eti kila mtu hajui ndege zimenunuliwaje hawana hoja wanawadanganya watu wakati walipitisha wenyewe yaani na wewe unataka risiti ya ndege ? nenda ATCL utaonyeshwa
 
Naona watu tunatoa povu tu, baada ya kuona clip ya mgombea iliyounganishwa na hansard za aliyekuwa mbunge wetu wa Kawe.
Hivi vitu havihitaji hasira.
 
Kwa uongo huu mgombea atakuwa na tatizo kubwa kichwani mwake kuna uwezekano mkubwa anatumia bapa kwanza kabla ya kuanza kuhutubia.
 
Kilichopelekwa bungeni ni bajeti ya manunuzi ambapo kama kawaida ya wabunge wa CCM ni ndiyoooo. Kilichotakiwa kupelekwa ni hoja ya kuzinunua na ijadiliwe shirika litaendeshwa vipi. Hata hayo ya reli ni bajeti tu zinapelekwa bungeni ila siyo hoja! Watu walitaka hoja ijadiliwe. Huwezi kujenga reli ya trilioni 6 aa kitanzania halafu uamue peke yako.

Huwezi kuja tu unasema nanunua ndege 11 tena wewe ndiye unapanga ununue wapi na kwa muda gani na ulipeje. Hakuna nchi inaendeshwa hivyo! Ndiyo maana likawepo bunge.

Unajua Magufuli alikuwa ametufanya watanzania wote ni mazuzu kwamba yeye peke yake ndiye mwenye akili!
Tuseme No!
 
..hoja siyo kama bunge lilihusishwa au halikuhusishwa.

..Tanzania hatukutakiwa kununua ndege kwasababu shirika la ndege ni biashara ya hasara.

..matrilioni ya fedha tulizotumia kununua ndege ambazo zinatutia hasara sasa hivi, yalipaswa kuelekezwa ktk sekta nyingine zinazogusa wananchi wengi zaidi.

Hii ndiyo hoja....

Hoja siyo kupitishwa ama kutopitishwa kwa fedha za ujenzi wa CHATO INTERNATIONAL AIRPORT...

Hoja ni kwanini mabilioni ya fedha yakajenge uwanja wenye hadhi ya kimataifa kijijini kwa Rais ambako hakuna biashara yeyote inayoendelea huko na bila tenda ya ujenzi kutangazwa kwa uwazi? Ni nini hicho kama siyo ufisadi na wizi mtupu?

Sijui kina Polepole na mwenyekiti wake na CCM kwa ujumla hawaelewi kitu gani tu...!!

Nadhani wao ndiyo wanajaribu kutaka kuudanganya umma na wapiga kura.....
 
Kuna watu wamejaliwa kusema uongo, huyu mgombea anasema uongo bila hata kupepesa macho yaani akiwa rais tutadanganywa hadi tukome.
 
Mkuu, ukimsikiliza mgombea anasema hakuna mbunge hata mmoja anayejua hata fedha zilizotengwa kununua hizo ndege. Hiyo ndiyo ilikuwa hoja yake kwenye clip hiyo kama umeisikiliza.

Halafu baadaye anaonekana Mheshimiwa Halima Mdee akiijadili hoja hiyo akiwa Bungeni. Msinishambulie mimi kwakuwa mimi sio niliyesema hivyo na bahati nzuri nimeweka video yake. Mimi sigombei hata udiwani.
 
Back
Top Bottom