Uchaguzi 2020 Je, ni kweli Bunge halikuhusishwa kwenye ununuzi wa ndege za ATCL?

Uchaguzi 2020 Je, ni kweli Bunge halikuhusishwa kwenye ununuzi wa ndege za ATCL?

Umeona wapi shirika linafanya biashara lakini ukaguzi hakuna.
Anzisha hiyo hoja wewe, tutakuja kukujibu, hii ni hoja inayojibu zile propaganda za mgombea Fulani hivi anayekataa Hansard za Bunge Kwa maksudi zilizoidhinisha manunuzi ya ndege.
 
Mkuu, ukimsikiliza mgombea anasema hakuna mbunge hata mmoja anayejua hata fedha zilizotengwa kununua hizo ndege. Hiyo ndiyo ilikuwa hoja yake kwenye clip hiyo kama umeisikiliza. Halafu baadaye anaonekana Mheshimiwa Halima Mdee akiijadili hoja hiyo akiwa Bungeni. Msinishambulie mimi kwakuwa mimi sio niliyesema hivyo na bahati nzuri nimeweka video yake. Mimi sigombei hata udiwani.
Screenshot_20200829_215552.jpg
 
Hii ndiyo hoja....

Hoja siyo kupitishwa ama kutopitishwa kwa fedha za ujenzi wa CHATO INTERNATIONAL AIRPORT...
Mkuu hii ni hoja yako ambayo ni nzuri kabisa. Lakini haikuwa hoja ya siku ya mgombea wetu. Ungeisikiliza kwanza hiyo video clip.
 
Wananchi wa chato waliulizwa kama wanauhitaji uwanja wa ndege wa chato na jibu lao lilikuwa HAPANA.

Wananchi wa maeneo mbalimbali wameulizwa kama wanahitaji midege aliyonunua Jpm na jibu lao ni HAPANA.
 
Kilichopelekwa bungeni ni bajeti ya manunuzi ambapo kama kawaida ya wabunge wa CCM ni ndiyoooo. Kilichotakiwa kupelekwa ni hoja ya kuzinunua na ijadiliwe shirika litaendeshwa vipi. Hata hayo ya reli ni bajeti tu zinapelekwa bungeni ila siyo hoja! Watu walitaka hoja ijadiliwe. Huwezi kujenga reli ya trilioni 6 aa kitanzania halafu uamue peke yako...
Kawadanganye wanachadema wenzako uliona wapi mchakato wa manunuzi unapelekwa bungeni? Bunge huwa linapitisha bajeti tu siyo manunuzi. Wakati mwingine mkubali tu kuwa mgombea wenu anachemka sana asifikiri watz ni wajinga kiasi hicho.
 
Mkuu, hoja ya Mgombea ni kwamba bunge halikuhusishwa kabisa, na ndivyo anavyotueleza wapiga kura wake.
Maswali hayo ya bunge kutohusishwa yaliulizwa wakati was uhai wa bunge, iweje majibu yasipatikane wakati huohuo yaje yatolewe sasa?
Serikali ya awamu ya tano imejikita zaidi katika uongo na ulaghai ila bahati mbaya ni wa kishamba zaidi ambao kila mwenye akili hawezi kudanganyika.
 
Mbunge litakuwa limehusishwa endapo tu report ya ukaguzi itarudishwa bungeni.

Je report ya manununuzi ya ndege za ATCL imewahi kufanywa na CAG na kupelekwa bungeni??
 
Devices alizowekewa na mabeberu ya Kibelgiji inampa shida!
Wabelgigi washenzi sana walimtesa Patrick Lumumba wakamgoa meno bila ganzi,harafu wakamtosa kwenye tindikali ya Sulphuric Acid akayeyuka kabisa.

Juzi binti yake ameomba serikali ya Belgium irudishe jino lake.Ukisikia wazungu washenzi ni hao.
 
Wabelgigi washenzi sana walimtesa Patrick Lumumba wakamgoa meno bila ganzi,harafu wakamtosa kwenye tindikali ya Sulphuric Acid akayeyuka kabisa.
Juzi binti yake ameomba serikali ya Belgium irudishe jino lake.Ukisikia wazungu washenzi ni hao.
Bora corona kuliko ccm.
 
Mimi nitoe ushauri wangu ambao hauegemei upande wowote. Juzi nimepanda Bombadier kutoka Dar mpaka Mwanza. Ujazo wa ndege hii ni abiria 72 lakini tuliopanda ndege ile ni kama abiria 30 tu ambayo kwa biashara ni hasara kubwa na hii inatokana na wananchi wengi hali zao za kiuchumi siyo nzuri.

Pili niliona dreamliner imeegeshwa pale terminal three na natumaini ni muda mrefu imeegeshwa pale bila kupaa. Huduma kwenye ndege siyo wa kuridhisha. Mtu unaambiwa kufika uwanjani saa tano na nusu na unakuja kufika Dar saa kumi kasoro robo.

Hakuna chochote anachopewa abiria na hata mkiwa angani hakuna hata kinywaji au hata chakula cha mchana mnachoambulia ni maji ya afya mills 300. Kama nilivyona kwa kweli ATCL wajitafakari vinginevyo Shirika litaingia kwenye hasara kubwa.
 
Maswali hayo ya bunge kutohusishwa yaliulizwa wakati was uhai wa bunge, iweje majibu yasipatikane wakati huohuo yaje yatolewe sasa?
Serikali ya awamu ya tano imejikita zaidi katika uongo na ulaghai ila bahati mbaya ni wa kishamba zaidi ambao kila mwenye akili hawezi kudanganyika.
Mkuu, hoja imeletwa sasa na mgombea akiwa kwenye kampeni za kuwania urais. Wakati bunge likiendelea hakukuwa na kampeni wala mgombea urais. Nadhani tukae sawa kwanza hapo.
 
Mimi nitoe ushauri wangu ambao hauegemei upande wowote. Juzi nimepanda Bombadier kutoka Dar mpaka Mwanza. Ujazo wa ndege hii ni abiria 72 lakini tuliopanda ndege ile ni kama abiria 30 tu ambayo kwa biashara ni hasara kubwa na hii inatokana na wananchi wengi hali zao za kiuchumi siyo nzuri...
Pole inaonekana ni mara yako ya kwanza kupanda ndege. Kwanza kuhusu huduma ya chakula imesimamishwa kutokana na Corona pia naomba nikujulishe kuwa ndege ikiweza kupakia 1/3 ya uwezo wake tayari hakuna loss hapo.
 
Back
Top Bottom