barack2010
Member
- Aug 25, 2014
- 22
- 22
Hivi karibuni club ya Simba inatarajia kufanya mkutano wa club, moja ya ajenda ya kikao hicho ni kufanya maamuzi ya namna ya uendeshaji wa club ya Simba. Kuna baadhi ya wanachama wa club wanakusanya maoni kutoka kwa wapenzi wa simba kuhusiana na uendeshaji wa club katika mfumo wa hisa na kisha kuyawasilisha maoni hayo katika mkutano mkuu wa simba. Kasi hii ya kutaka mabadiliko ya uendashaji wa club imekuja baada ya club ya simba kuboronga katika ligi kuu ya Vodacom, huku wengi wanaotaka mabadiliko haya wakiamini itakuwa hatua muhimu kwa club kufanikiwa. Mfumo wa hisa umebebewa bango baada ya mwanachama mmoja kutaka akabidhiwe club ile ailetee mafanikio, ndiyo baadhi ya wadau wa simba wakaja na hili pendekezo la kutaka yafanyike mabadiliko ya mfumo ya uendeshaji wa club uwe mfumo wa hisa. Nasita kushawishika kuwa endapo timu itaingia kwenye mfumo wa hisa, club ya simba itapata mafanikio inayoyakusudia.
Kwa mtazamo wangu kutofanya vizuri kwa club ya simba kumesababishwa haswa na;
1 ukosefu wa umoja ndani ya club: kuwepo kwa makundi yanayokinzana ndani club.
2 management.
3 Siasa kuingizwa katika usajili wa wachezaji pamoja baadhi ya wanachama kusajili wachezaji badala ya uongozi: usajili wa wachezaji unarembwa zaidi kwenye media kuliko uhalisia.
Hapo kabla ya misimu minne iliyopita simba ilikuwa inafanya vizuri kiasi chake katika ligi ya ndani na kimataifa na timu ilikuwa bado chini ya wanachama. Kinachohitajika sasa hivi ni umoja na mshikamano, uongozi dhabiti uiwezeshe timu ifanye vizuri katika mashindando ya ligi, uongozi uboreshe vyanzo vya mapato na kutafuta vyanzo vipya vya mapato ikiwa pamoja na wadhimini.
Timu ya simba ina wanachama na mashabiki wengi karibia nusu ya mashabiki wote wa mpira wa miguu nchini, kwa hali ya sasa club hii ni ya wanasimba wote. Kwa hivi sasa ni rahisi kwa wapenzi wengi wa simba (wasiyo wanachama) kupata uanachama kuliko kumiliki hisa. Je ni asilimia ngapi ya hawa wanasimba wataweza kununua hisa katika club? Kinachoelekea kufanyika hivi sasa ni kuiondoa club kutoka mikononi mwa wanachama (wanasimba) kuipeleka kwa watu wachache ambao hatuna uhakika kama watatuletea mafanikio tunayoyakusudi.
Nahitimisha mawazo yangu kwa kusema tusitumie haya mageuzi kufunika hoja ya msingi ambayo ni kuboronga kwa club yetu katika mashindano ya ligi kuu kwa miaka ya hivi karibuni. Club ya simba bado inaweza kufanya vizuri ikiwa chini ya wanachama kama uongozi utakuwa imara, tutaweka tofauti zetu pembeni, na kutanguliza maslahi ya club mbele. Kwa sasa wanasimba tunambulia presha kutokana na timu kufanya vibaya na kejeli kutoka kwa watani wetu. Lengo la msingi la club ya simba ni kutupa burudani sisi wanachama na wapenzi wa simba, na burudani tunayotarajia tutaipata kama timu itashinda vikombe.