Je ni kweli club ya Simba inahitaji mageuzi katika mfumo wa uendeshaji?

Je ni kweli club ya Simba inahitaji mageuzi katika mfumo wa uendeshaji?

barack2010

Member
Joined
Aug 25, 2014
Posts
22
Reaction score
22
Hivi karibuni club ya Simba inatarajia kufanya mkutano wa club, moja ya ajenda ya kikao hicho ni kufanya maamuzi ya namna ya uendeshaji wa club ya Simba. Kuna baadhi ya wanachama wa club wanakusanya maoni kutoka kwa wapenzi wa simba kuhusiana na uendeshaji wa club katika mfumo wa hisa na kisha kuyawasilisha maoni hayo katika mkutano mkuu wa simba. Kasi hii ya kutaka mabadiliko ya uendashaji wa club imekuja baada ya club ya simba kuboronga katika ligi kuu ya Vodacom, huku wengi wanaotaka mabadiliko haya wakiamini itakuwa hatua muhimu kwa club kufanikiwa. Mfumo wa hisa umebebewa bango baada ya mwanachama mmoja kutaka akabidhiwe club ile ailetee mafanikio, ndiyo baadhi ya wadau wa simba wakaja na hili pendekezo la kutaka yafanyike mabadiliko ya mfumo ya uendeshaji wa club uwe mfumo wa hisa. Nasita kushawishika kuwa endapo timu itaingia kwenye mfumo wa hisa, club ya simba itapata mafanikio inayoyakusudia.

Kwa mtazamo wangu kutofanya vizuri kwa club ya simba kumesababishwa haswa na;

1 ukosefu wa umoja ndani ya club: kuwepo kwa makundi yanayokinzana ndani club.

2 management.

3 Siasa kuingizwa katika usajili wa wachezaji pamoja baadhi ya wanachama kusajili wachezaji badala ya uongozi: usajili wa wachezaji unarembwa zaidi kwenye media kuliko uhalisia.

Hapo kabla ya misimu minne iliyopita simba ilikuwa inafanya vizuri kiasi chake katika ligi ya ndani na kimataifa na timu ilikuwa bado chini ya wanachama. Kinachohitajika sasa hivi ni umoja na mshikamano, uongozi dhabiti uiwezeshe timu ifanye vizuri katika mashindando ya ligi, uongozi uboreshe vyanzo vya mapato na kutafuta vyanzo vipya vya mapato ikiwa pamoja na wadhimini.

Timu ya simba ina wanachama na mashabiki wengi karibia nusu ya mashabiki wote wa mpira wa miguu nchini, kwa hali ya sasa club hii ni ya wanasimba wote. Kwa hivi sasa ni rahisi kwa wapenzi wengi wa simba (wasiyo wanachama) kupata uanachama kuliko kumiliki hisa. Je ni asilimia ngapi ya hawa wanasimba wataweza kununua hisa katika club? Kinachoelekea kufanyika hivi sasa ni kuiondoa club kutoka mikononi mwa wanachama (wanasimba) kuipeleka kwa watu wachache ambao hatuna uhakika kama watatuletea mafanikio tunayoyakusudi.

Nahitimisha mawazo yangu kwa kusema tusitumie haya mageuzi kufunika hoja ya msingi ambayo ni kuboronga kwa club yetu katika mashindano ya ligi kuu kwa miaka ya hivi karibuni. Club ya simba bado inaweza kufanya vizuri ikiwa chini ya wanachama kama uongozi utakuwa imara, tutaweka tofauti zetu pembeni, na kutanguliza maslahi ya club mbele. Kwa sasa wanasimba tunambulia presha kutokana na timu kufanya vibaya na kejeli kutoka kwa watani wetu. Lengo la msingi la club ya simba ni kutupa burudani sisi wanachama na wapenzi wa simba, na burudani tunayotarajia tutaipata kama timu itashinda vikombe.
 
Una mawazo mazuri,ila tukitaka kulipeleka soka letu liwe la kisasa zaidi lazima tukubali hayo mageuzi ya KIMFUMO
 
Una mawazo mazuri,ila tukitaka kulipeleka soka letu liwe la kisasa zaidi lazima tukubali hayo mageuzi ya KIMFUMO

Mageuzi ya kimfumo sio kumpa mtu timu,Mageuzi ni kuwashirikisha wanachama wengi kwenye uendeshaji wa klabu
 
......Simba inahitaji mabadiliko usijidanganye!, unapozungumzia ukosefu wa umoja ndani ya klabu nani anaesababisha? Poor results!, management mbovu ndio hao hao viongozi, kuleta siasa ndani ya klabu nani anaesababisha?, again Uongozi!.

Matatizo yote ya Simba sasa kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na uongozi, usajili wa magumashi, wachezaji kucheleweshewa mishahara na mengine.

Hii ndio nafasi wana Simba tumeipata, tuitumie!, ni bora Simba iendeshwe na mtu mmoja iwe na muelekeo,kuliko kuendeshwa na kundi la watu wasioeleweka, wenye kuitumia timu kwa malengo yao binafsi!.
 
Mageuzi ya kimfumo sio kumpa mtu timu,Mageuzi ni kuwashirikisha wanachama wengi kwenye uendeshaji wa klabu

how?!

hawa anachama wetu wasio na uwezo hata wa kulipia kadi za uanachama?!, wanaoshinda klabuni siku nzima kusubiri kupiga watu mizinga!

Acha utani, hawa wanachama masikini ndio chanzo cha Simba kufanya vibaya, sababu wanatumika/shawishika kirahisi sana na kundi lililopo madarakani,halafu mwisho wa siku timu ndio inayoumia, tusijidanganye, wanachama wa timu zetu huwezi kuwalinganisha na wanachama wa klabu za nje!, wengi upepo tu!
 
Tatizo la Simba kwa sasa ni Uongozi mbovu. Simba limewachagua watu wasio ijua simba na watu wenye malengo binafsi. Simba Iliongozwa na wazee wanywa kahawa tu lakini walikua na mapenzi na Klabu yao na timu ilikua ikiheshimika Afrika nzima.
sasa ina vionozi wanao jifanya wasomi lakini hawana uwezo kuingoza klabu. maamuzi yanafanya baa na wachezaji wanaitwa baa kupewa mikakati huku wakinywa.
uendeshaji wa wa klabu hauwezi kufanya Avacado Bar kule Kawe. Klabu tumeikabidhi walevi kwa sababu wana vijisenti vya kitapeli
 
nyie mnaijua hela nyie? hela sabun ya roho.... majiran wametulia maana kuna hela ngoja nae mwenye hela zake aondoke... hata huyu anaeleta hela simba anaweka hela yake with management ya kutosha mnafikir anaakili mbovu ya kuweka 20bln bila kujua zitaendeshaje team...
 
how?!

hawa anachama wetu wasio na uwezo hata wa kulipia kadi za uanachama?!, wanaoshinda klabuni siku nzima kusubiri kupiga watu mizinga!

Acha utani, hawa wanachama masikini ndio chanzo cha Simba kufanya vibaya, sababu wanatumika/shawishika kirahisi sana na kundi lililopo madarakani,halafu mwisho wa siku timu ndio inayoumia, tusijidanganye, wanachama wa timu zetu huwezi kuwalinganisha na wanachama wa klabu za nje!, wengi upepo tu!

Hakuna uongozi ambao umewahi kuwashirikisha wanachama kwenye uendeshaji wa klabu.Hivi unajua wanachama wa Simba hata 20,000 hawafiki ? Simba/Yanga zina uwezo wa kuwa na wanachama hai 5 million kila timu kama watapata uongozi mzuri

Watu wanapenda hizi timu tatizo kubwa hazijapata viongozi makini
 
Deal za watu hizo kaka katika vilabu mind your business dont waste time time is money
 
Mpira ni biashara mpira sio mapenzi tena mpira sio kujitolea....inafika kipindi tukubali kwamba dunia inabadilika na mambo yanabadilika,ifike kipindi sisi wanasimba tukubali mabadiliko,hata kama timu Ingekua unafanya vizuri katika ligi ya ndani na nje kutoka na mda haya mabadiliko hayaepukiki.
Timu inahiyaji wacheza waziri
Timu I nahitaji kiwanja na hostel mzuri za wachezaji
Timu inaitaji kujiendeleza kibiashara zaidi.
Bila kuwa na mageuzi ya kimfumo na kimuundo hayo yote hayawezi kifanyika.
Tukubali tu kwamba mda sio rafiki tena simba ya Leo sio Sunderland ile timu umekua na inaitwa iache familia ikajitegemee..
 
Mageuzi ya kimfumo sio kumpa mtu timu,Mageuzi ni kuwashirikisha wanachama wengi kwenye uendeshaji wa klabu

Pia ni lazima kuuza hisa kwani wanachama hata wakishirikishwa ni vigumu kujitoa hasa kiuchumi angalia simba ina wanachama wangapi,wangapi wanaolipia ada zao,wangapi wanachangia gharama za uendeshwaji wa club swala la mageuzi kimfumo na kiutendaji haliepukiki kama tunataka maendeleo ya club na kusonga mbele zaid
 
Mo kajipanga kuwekeza simba na nimefurahi alivyosema simba inahitaji muwekezaji na sio mfadhili lakini viongozi na wanachama wapo tayari kwa mabadiliko ya kimfumo? Mpira wa sasa ivi ni pesa sio bla bla kwasababu simba ina miaka takribani 80 lakini hata uwanja wa mazoezi hamna
 
Hata familia ya grazer ijekuimiliki simba hakuna cha maana watakachoonesha zaid ya kushangilia tim za kigeni tu
 
Pia ni lazima kuuza hisa kwani wanachama hata wakishirikishwa ni vigumu kujitoa hasa kiuchumi angalia simba ina wanachama wangapi,wangapi wanaolipia ada zao,wangapi wanachangia gharama za uendeshwaji wa club swala la mageuzi kimfumo na kiutendaji haliepukiki kama tunataka maendeleo ya club na kusonga mbele zaid

Simba/Yanga haziendeshwi na wanachama zinaendeshwa na viongozi hata 20 hawafiki na viongozi hawajawahi kuwashirikisha wanachama.Jiulize kwa nini vyama vya siasa huwa wanafanya kampeni kwa wanachama na kutembea nchi nzima ?
 
Hakuna uongozi ambao umewahi kuwashirikisha wanachama kwenye uendeshaji wa klabu.Hivi unajua wanachama wa Simba hata 20,000 hawafiki ? Simba/Yanga zina uwezo wa kuwa na wanachama hai 5 million kila timu kama watapata uongozi mzuri

Watu wanapenda hizi timu tatizo kubwa hazijapata viongozi makini

....hii issue itahitaji muda, nadhani na katiba pia itatakiwa kurekebishwa,kuwakusanya hao wanachama mil. 5 sio kazi rahisi,na je wote watakuwa tayari kuichangia klabu?, isije kuwa tunaisemea mioyo ya watu tu, sababu ya mapenzi yetu kwa klabu!

Mpango ni je, kwa sasa tutafanyaje ili kuinusuru klabu itoke hapa ilipo?, na sisi tuanze tena kushiriki mashindano ya kimataifa?
 
Mageuzi ya kimfumo sio kumpa mtu timu,Mageuzi ni kuwashirikisha wanachama wengi kwenye uendeshaji wa klabu

Hivi TP Mazembe inamilikiwa na wanachama?? Mbona wanafanikiwa sana?
 
......Simba inahitaji mabadiliko usijidanganye!, unapozungumzia ukosefu wa umoja ndani ya klabu nani anaesababisha? Poor results!, management mbovu ndio hao hao viongozi, kuleta siasa ndani ya klabu nani anaesababisha?, again Uongozi!.

Matatizo yote ya Simba sasa kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na uongozi, usajili wa magumashi, wachezaji kucheleweshewa mishahara na mengine.

Hii ndio nafasi wana Simba tumeipata, tuitumie!, ni bora Simba iendeshwe na mtu mmoja iwe na muelekeo,kuliko kuendeshwa na kundi la watu wasioeleweka, wenye kuitumia timu kwa malengo yao binafsi!.
Huyo MO aliishindwa African Lyon,simba ataiweza????
 
Mageuzi ya kimfumo sio kumpa mtu timu,Mageuzi ni kuwashirikisha wanachama wengi kwenye uendeshaji wa klabu
Kwanini usiwe muwaz tu kuwa uongoz ulioko madarakani ndo tatizo kwa simba? Kabla ya hawa watu mbona simba ilikuwa poa?
 
Back
Top Bottom