kuhusu hilo la kuwa juu ya gari then ukaruka hata kama gari linatembea utatua palepale gari lilipofika so halitakuacha otherwise uwe uliruka kiupande (hiyo ipo proved kwenye physics). kuhusu satellite ni kwamba zipo juu sana ndio maana hutuzigongi.
kila satellite ina speed yake katika kuzunguka dunia na kumbuka kuwa kuna nguvu ya uvutano kati ya dunia(ni kwa sayari zote) na jua sasa satellite huwa zinawekwa pale katikati ambapo nguvu ya uvutano ya dunia na ya jua zinapokutania hivyo haziwezi kuvutwa na jua wala dunia, position pia huwa inategemea na spidi ya satellite husika.
na ndege mara zote husafiri ngani ya anga ambamo inakuwa ni kama inavutwa na dunia vile, sasa kwa mfano helicopter isimame angani kwa siku nyingi haiwezi kuachwa na dunia licha ya kwamba dunia inazunguka jua, dunia huwa anahama na kila kitu kilicho ndani ya eneo ambamo nguvu yake ya uvutano imeenea (earth's attraction force) labda ikotee hiyo helicopter imevuka hili eneo ndio itaachwa na tutabaki kusema ndege imepotelea angani.
Spidi ya dunia kuzunguka jua ni kubwa(kilometa 30 kwa sekunde) na mzunguko mmoja wa dunia kwenye obiti kuzunguka jua ni zaidi ya kilometa milioni 940, hivyo licha ya spidi kubwa dunia inachukua zaidi ya siku 365 kuzunguka jua mzunguko mmoja.
Kidogo nimeanza kushiba maelezo yako asante sana nasubiri kujazia nyama kwa wataalam wengine