POTOSHI Je, ni kweli Heche amesema anahitaji milioni 30 ili zimuongezee motisha?

POTOSHI Je, ni kweli Heche amesema anahitaji milioni 30 ili zimuongezee motisha?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Nimekutana na hii video Insta wanasema, "wanachadema haujawapatia majibu ya million 900 zilipoenda kwa ujasiri Unakuja mbele za watu eti unaomba mil 30 kwaajili yako zikupe motisha, motisha gani akati umeshawaibia wanachadema mil 900 na hutaki kusema zilipo

Kwa tunavokufahamu wewe ingekua sio kweli lazima ungesema kuwa sio kweli ila badala yake unafukuza wote wanaohoji ili uwanyamazishe, wewe na mnyika wote ni wezi wakubwa"



1784012198435.png
 
Tunachokijua
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, Julai 11, 2026, aliwashukuru watanzania na wafuasi wa CHADEMA kwa ujumbe faraja alioupokea kupitia mitandao ya kijamii na simu ya mkononi kutokana na kifo cha dereva wake, Suez Maradufu.

Madai

Kumekuwapo na video inayosambazwa mtandaoni na kudai kuwa Heche amesema "Nahitaji milioni 30 ziniongezee motisha"

Je, ni upi uhalisia?

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kupitia marejeo ya video umejiridhisha kuwa kipande hicho cha video kimekatwakatwa na kuunganishwa isivyostahili hivyo kupotosha ujumbe halisi uliotolewa na Heche.

Katika video halisi Heche alisisitiza kuwa badala ya watu kumchangia yeye binafsi kama ambavyo baadhi ya viongozi na wanachama walivyokuwa wamependekeza, Heche ameomba michango hiyo ielekezwe moja kwa moja kwenye akaunti za chama kwaajili ya kufanikisha mkutano wa Baraza Kuu.

Alisema kuwa tarehe 15 Septemba kutakuwa na mkutano wa Baraza Kuu la CHADEMA ambao unatarajiwa kufanya uamuzi mkubwa wa kihistoria kuhusu mwelekeo wa nchi, ajenda ya Katiba Mpya, na hatua za kuhakikisha mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu anakuwa huru.
​
Back
Top Bottom