Kinau Michael
Member
- Aug 18, 2023
- 8
- 13
Siku hizi mtaani tunashuhudia watu wakivaa jezi za timu mbalimbali wanazozipenda na wengine huvaa zile zinazowavutia hata kama hawaipendi au kuifahamu klbau yenyewe.
Sina hakika kama wengi wanaifahamu klabu ya Palmeiras ya kule Brazili kwa akina Neymar Jr na Ronaldinho Gaucho, lakini Jezi yake imekuwa maarufu sana kwenye mitaa ya Manzese, Buguruni, Temeke na maeneo mengine mengi tu ya Dar es salama.
Kwa takwimu ambazo sio rasmi, kati ya watu 10 unaokutana nao wenye kuvaa jezi basi watatu mpaka wanne wamevaa jezi zenye neno "Crefisa" na hapo ndio nikajiuliza maswali ikiwemo kwanini wengi wameioenda jezi hiyo?
Kama ilivyo jadi yangu napenda kuuliza, wale niliobahatika kuwauliza walinambia "huu uzi wenyewe ni Og." wakimaanisha haujachakachuliwa na umezingatia ubora. Wengine wakanambia hawajui ila tu wameipenda jezi imewavutia.
Sasa nisaidieni hapa nijue, ubora wa jezi unapimwa kwa mvuto wake au malighafi liyotumika kutengeneza vazi husika (jezi)