Je, ni kweli kinyonga hupasuka na kunguru hana damu?

Je, ni kweli kinyonga hupasuka na kunguru hana damu?

Kuna aina mbili za vinyonga. Yupo anaye taga mayai na yupo anaye zaa. Ila kusema lazima apasuke sijawahi kufanya huo utafiti. Ila kuona anamimba nimewahi muona kipindi tunachunga mifugo. Niliwahi mpiga akapasuka nikakuta vitoto vya kinyonga ndani viwili.
 
Unatetea kitu ambacho nahisi hukifahamu vizuri...kunguru ana miguu miwili...current ikipita kwa mguu mmoja inaenda kwa mguu mwingine inaenda zake(closed circuit)...sasa huu waya mmoja we unaousema ni upi?
Hembu jaribu kushika high voltage wire kwa kidole chako tu halafu uje hapa jamvini kutoa ushuhuda, Jaribu kutofautisha kati ya vifaa vya umeme na waya unaopitisha umeme!!
jay jay yupo sahihi,umeme una namba..1-5.huwezi kunasa kwa kushika namba moja
Kwa umeme huu wa nyumbani ambao ni 220v-240kwa kila namba,na'kunguru yy anakanyaga namba moja,ila utarushwa tu
.....karibu kama hujaelewa
 
jay jay yupo sahihi,umeme una namba..1-5.huwezi kunasa kwa kushika namba moja
Kwa umeme huu wa nyumbani ambao ni 220v-240kwa kila namba,na'kunguru yy anakanyaga namba moja,ila utarushwa tu
.....karibu kama hujaelewa

Nashukuru kwa taarifa lakini kwanini iwe ni kunguru tu...ndege kama popo hunasa why? Ntafurahi nikieleweshwa
 
Mkuu kwa uelewa wangu mdogo kuhusu
Kunguru ni kuwa ana damu ila huenda
uliwahi kumwona kwenye nyaya za umeme
amesimama na hakunasa.


Ni kuwa kwenye miguu yake kuna magamba
yanayomfanya hata asimama kwenye nyaya
inakuwa km vile mti mkavu. Lakini mwili
wake wote una damu.

Kiasi naweza kuwa nimekuelewesha ila
watakuja wengine na mambo mazuri ili
nasi tuyajue ya Kunguru.


Kuhusu Kinyonga hata nami huwa nasikia
hii habari ila nami naungana nawe kungoja
majibu sasa.

Hiyo sio methali ni kitendawili edit kwa msaada
 
Nashukuru kwa taarifa lakini kwanini iwe ni kunguru tu...ndege kama popo hunasa why? Ntafurahi nikieleweshwa

Popo sio ndege yeye tupo nae ktk kundi la mammalia na anazaa kama binadam na hatagi mayai ana vnyweleo
 
Jamani nazidi kupata changamoto nyingi na majibu mazur ya wadau,na nazidi kutafakari hawa viumbe wanavyozd kuchanganya umma wa walimwengu.
 
Swali lako la kwanza ni Ukweli kabisa,kinyonga anapotaka kujifungua ni lazima apande juu ya mti mrefu na kujiangusha ili apasuke tumbo na mtoto atoke.
Hapo mama mtu hufa na mtoto huendelea kuishi.
Na ndio maana kuna methali isemayo "huuawa na uzao waje" ambalo jibu ni Kinyonga.

Kuhusu swali lako la pili,sina uhakika nalo sana japo nami nimewahi kusikia hayo.

Kama ni hivyo watoto, ambaao ni wachanga and very delicate kwa nini wasife nao? Imagine paka apande mnazi mreeefu na aanguke mpaka chini na apasuke, watoto wake watapona kweli? Kunguru ni kundi la ndege kama kuku sasa asipokuwa na damu ataishije? Kingine hebu tujenge utaratibu wa kujisomea jamani,siku hizi mambo yamerahisishwa sana kupitia mitandao ya simu zetu, unaweza ku google hata kwa kiswahili kama sijakosea.
 
Nashukuru kwa taarifa lakini kwanini iwe ni kunguru tu...ndege kama popo hunasa why? Ntafurahi nikieleweshwa

Nyayo za kunguru ni kavu mno, damu ni almost negligible kwenye nyayo za kunguru. Pia nyayo za kunguru zina magamba ambayo yana very high resistance kwa umeme. Ni tabia za umeme kama kuna njia mbili za kupita, umeme mwingi utapita kwenye njia ambayo ina low resistance na kuacha ile yenye very high resistance (au kupita kidogo mno). Tabia hii inamfanya kunguru kuwa salama akitua kwenye nyaya za umeme wa kawaida. Mara chache huwa wanapigwa shoti kwenye umeme mkubwa kama ule unaotoka moja kwa moja kidatu kabla haujapunguzwa nguvu.

Nyayo za popo ni tofauti sana na za kunguru. Popo anadamu nyingi zaidi kwenye nyayo.
 
Unatetea kitu ambacho nahisi hukifahamu vizuri...kunguru ana miguu miwili...current ikipita kwa mguu mmoja inaenda kwa mguu mwingine inaenda zake(closed circuit)...sasa huu waya mmoja we unaousema ni upi?
Hembu jaribu kushika high voltage wire kwa kidole chako tu halafu uje hapa jamvini kutoa ushuhuda, Jaribu kutofautisha kati ya vifaa vya umeme na waya unaopitisha umeme!!
mkuu nadhani hiyo underlined inakuhusu sana wewe kuliko yeye. asante
 
sikubahatika kuona kinyonga live zaidi ya kwenye tv tu na kuhusu kunguru acha wataalam wa umeme watupe darsa
 
Habari wana jf,
Nina maswal mawili yanayonichanganya kchwa chang ktk maisha yang;
1.nimesikia kwamba kinyonga anapozaa huwa amapanda kwenye mti mrefu na kujiachia na tumbo kupasuka watoto kutoka na mama hufa.
2.Ni kweli kua kunguru hana damu?

3-hivi ni kweli kuwa kunguru akifa huwa haozi bali anakauka? maana inasemekana kuwa mwili wake una sumu na wadudu huwa hawamgusi
 
interesting!! kwanza kabisa, si kweli kwamba kinyonga hujirusha na kupasuka. that is simply a myth

pili, the only reason kunguru harushi na umeme ni kwasababu anapokanyaga waya wa umeme huwa ha-complete circuit. meaning, hakuna earth component ya kusafirisha umeme through mwili wake kwnda ardhini. "incomplete circuit"
hata wewe unaweza kushika umeme as long as huna earth connection (meaning unaelea) hutarushwa. fact
 
kunguru anayo damu ila kiwango chake ni kidogo. hiyo kukanyaga waya za umeme ni kuwa anakanyaga waya mmoja sio mbili kwa hiyo sakiti(circuit) inakuwa haijakamilika.angekuwa na uwezo wa kukanyaga nyaya zote mbili angemalizwa mara moja. nimeshaona kunguru akipigwa shoti kwenye transformer.

mjomba tukikupa waya mmoja uushike uko ready. Si utakua hujakamilisha circuit na hizo waya ushike randomly bila kuambiwa ipi ni ipi muhmu ushike mmoja tu
 
Huu Uzi umenipa changamoto kidogo ila kikubwa tuwe wafuasi laini kwanza
 
jay jay yupo sahihi,umeme una namba..1-5.huwezi kunasa kwa kushika namba moja
Kwa umeme huu wa nyumbani ambao ni 220v-240kwa kila namba,na'kunguru yy anakanyaga namba moja,ila utarushwa tu
.....karibu kama hujaelewa
niliwahi kuwa mwalimu veta wa umeme, hii ya umeme kua na namba 1-5 ndo nasikia! acheni mambo ya kwenye kahawa, ktk utaalamu. ndege yeyote hanaswi katika waya, sababu yeye hutua juu ya waya mmoja tu, hivo hafanyi complete circuit, akiwa mkubwa saa anatua au anaondoka akagusa waya ya pili kwa mabawa anapigwa shot,anakua amekamilisha complete circuit. jaribu kusimama juu ya ubao, uwe mkavu, ukigusa waya mmoja tu hutapata madhara,
 
jamani mbona wasahaulifu hivyo,kunguru kwenye vidole vyake kuna kama 'cover' ya plastick ambayo inamsaidia kusiwe na mawasiliano kati yake na 'phase' ila juu kidogo ile plastiki ile'plastick inaishia ndo maana wakati mwingine akitua vibaya kwenye 'nakeod phase' habari anaipata,hana tofauti na miguu ya kuku wa kienyeji...kwa wale wanaowanyonyoa kikwetu wanajua..lakini wale wa kufanyiwa kila kitu daa hili
Limewapita....
Mnasahau kitu kimoja.. ili patoke short circuit, ni lazima moja ya hayavyafuatayo yatokee..
1. line (phase) na line zigusane
2. line na neutral zigusane
3. Line na earth zigusane
sasa kinachomsevu kunguru ni kwa sababu hasababishi mgusano wowote wa waya katika hiyo migusano niliyoitaja hapo juu.

Hii hata kwa binadamu.. kama utagusa line mmoja tu na usiguse ardhi au earth point au neutral kwa wakati huo huo huwezi dhurika.. na hii ni kwa sababu hujaikamilisha circuit. na wakati mwingine si mpaka uguse hizo wire.bali hata ukiwa ndani ya ionised area ya wire mbili zenye umeme unapigwa shork kwa sababu hapo ni as good asvukeshika tu.

kwa hiyo kinachomsevu kunguru siyo magamba yake, bali namna ya ugusaji waya anaoufanya. kuna insulators za aina mbalimbali na magamba ya kunguru hayamo kwenye hizo aina. na vile vile kuna insulators zenye uwezo tofauti tofauti... za LV haziwezi tumika kwenye HT
 
Nyayo za kunguru ni kavu mno, damu ni almost negligible kwenye nyayo za kunguru. Pia nyayo za kunguru zina magamba ambayo yana very high resistance kwa umeme. Ni tabia za umeme kama kuna njia mbili za kupita, umeme mwingi utapita kwenye njia ambayo ina low resistance na kuacha ile yenye very high resistance (aIu kupita kidogo mno). Tabia hii inamfanya kunguru kuwa salama akitua kwenye nyaya za umeme wa kawaida. Mara chache huwa wanapigwa shoti kwenye umeme mkubwa kama ule unaotoka moja kwa moja kidatu kabla haujapunguzwa nguvu.

Nyayo za popo ni tofauti sana na za kunguru. Popo anadamu nyingi zaidi kwenye nyayo.
Uechanganya madesa.. kina chomwokoa kunguru siyo high resistance ya magamba yake...bali ni kwa kugusa only a single phase ...

we fikiri.. kwa udogo ule wa kunguru ukilinganisha na distance between wires hizo za kidatu atanasa saa ngapi?

halafu hii dhan ya umeme unarusha mnaichanganya sana.. pale unaruka wewe mwenyewe kwa mshituko ni kama wengine wanavyomwona nyoka halafu wakaruka halafu aje mtu aseme nyoka ajarusha.. HAPANA BANA
 
Back
Top Bottom