Kiswahili ni very romantic language' lakini unapaswa utumie mifano ya mazingira halisi ya Kiswahili na si kutoa mifano au tafsiri kutoka Kiingereza au lugha zingine. Utamaduni ni mama wa lugha. Lugha ni sehemu na kielelezo cha utamaduni wa jamii husika, hivyo Kiswahili ni sehemu ya utamaduni wa 'Waswahili', yaani watu wa pwani ya Africa Mashariki na maeneo ya jirani. Kiingereza ni sehemu ya utamaduni wa 'Waingereza' na watu wa maeneo jirani nako. Unapotumia mifano ya sentensi au tafsiri ambazo asili yake ni kiingereza utakachokiona ni 'mahaba' ya kiingereza na sio ya kiswahili.
Kinachoonekana hapa ni kwamba mleta mada na wachangiaje wengine kwa kujua au bila kujua ni kwamba hawana maneno, misamiati ya kiswahili yenye kuashiria mahaba. Kukosekana maneno haya kwako haina maana kwamba 'Kiswahili Hakiko Romatic'
Mfano unaposema: 'Bye and take care' kwa kiingereza (kwa tafsiri ya lugha na utamaduni) inaeleweka vizuri sana, lakini ukiitafsiri kwenda kwenye Kiswahili haitafsiriki na haileti maana kwasababu unajaribu kuhamisha kitu kutoka utamaduni wa kizungu utakipelekea utamaduni wa Kiswahili. Maneno kwa mfano 'Mpenzi wangu pole na kazi', kwa mswahili inaeleweka vizuri sana, na kuna mahaba ndani yake, lakini ukiitafsiri kwa kiingereza 'pole na kazi' haileti maana kwasababu ndani yake kuna zaidi ya lugha - ni suala la utamaduni.
Maneno na misemo kama Bon appetit, take care, Shikamoo, pole, ugua pole, yanaakisi utamaduni zaidi kuliko lugha, hivyo chochote ufanyanyo baki kwenye msingi wa lugha moja usichanganye madawa.