Je, ni kweli Kiswahili hakiko Romantic?

Je, ni kweli Kiswahili hakiko Romantic?

data

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2011
Posts
26,858
Reaction score
23,768
Inadaiwa kuwa lugha ya Kiswahili haiko 'romantic'.

Je, ni kweli?

Lets share.
 
Si kweli! Kiswahili kipo Tanzania na sio romantic,kwani mkuu hujui kiswahili kilianzia wapi? Kiswahili ni lugha inayopatikana Afrika mashariki hususani Tanzania huko Roma wanazungumza lugha zao ila na kiswahili kwa uchache hivyo kiswahili pia kinapatikana roma japo kwa uchache mfinyu Sana hivyo ni jukumu letu kisaidia kiswahili kufika huko romantic.
 
Si kweli! Kiswahili kipo Tanzania na sio romantic,kwani mkuu hujui kiswahili kilianzia wapi..?
Kiswahili ni lugha inayopatikana Afrika mashariki hususani Tanzania huko Roma wanazungumza lugha zao ila na kiswahili kwa uchache hivyo kiswahili pia kinapatikana roma japo kwa uchache mfinyu Sana hivyo ni jukumu letu kisaidia kiswahili kufika huko romantic.
Tunakifanyaje kiwe na mvuto wa kimahaba...

Tuachane na MAKABURU..
 
Jibu.
Awwww baby, What a surprise!!!!! Thank you.
Loooh baby, mbona mshangao. Asante sana.

Ni kweli KISWAHILI hakina misamiati...yaahh kii maahhbbuubahh!?
 
Wapi watoto wa Pemba... Pangani..

Kiswahili fasahaa
 
Tunakifanyaje kiwe na mvuto wa kimahaba...

Tuachane na MAKABURU..
Ahaa sikuelewa ndo tabu ya kunyoa kipara sitanyoa Tena😎

Mbona lugha yetu imekaa kimahaba! Tatizo linapokuja mnataka zile tafsiri za kimahaba ktk lugha nyengine mnataka mzitafsiri kwa kiswahili na zi sounds kimahaba!! Hilo ni kosa!!
Kila lugha kuna namna inavyo tamkwa na inasifa zake kimatamshi..
Pia mnapotafsiri angalieni sana maana na sio maneno mfano kwa kiingeleza mtu akisema "I miss you!" Ukitafsiri kichwa kichwa mtu unaweza sema "nimekukosa"😂 lkn neno zuri hapo na tamu ni "nimekuhamu" au Nina hamu na wewe" mbona inasound good na ipo romantic..

Lugha pia inaeleza tamaduni mfano sisi haswa Afrika hatuna tamaduni za kusheherekea siku za kuzaliwa ni tumerithi tu! Pia mapenzi sio Jambo la kuonyeshana hadharani kama wenzetu na ndio maana unaona tunakosa baadhi ya misamiati ya kimahaba ila natumai ikawepo kwenye kamusi za kiswahili.. lugha huongea tamaduni za watu husika.
Tusitafsiri tu neno bali maana surprise mtu unasema mshangao wkt alietamka anamaanisha zawadi!!
Kiswahili ni kitamu sana haswa ukikutana kwenye nyanja ya mashairi ya kimahaba..
Hata wkt wa tendo lenyewe kuna baadhi ya maneno mtoto wa kike akiisema dah! Unajihisi dunia yote ni yako hapo hata kama ulikuwa huna hamu itakuja tu😂.. mkuu kuna vitu havisemeleki hata havielezeki mtoto unakuta anakuambia "mpenzi weka yote" "taratibu",unaniumiza anatoa na tumguno fulani tutamutamu hlf unaniambia lugha yetu haipo romantic kwa kufuata misingi ya lugha nyengine hapo sikuelewi😜
 
Jibu.
Awwww baby, What a surprise!!!!! Thank you.
Loooh baby, mbona mshangao. Asante sana.

Asante sana sio Thank you.
What a surprise sio Mbona mshangao.

Ni kweli, Kiswahili hakipo kimahaba.... hata kunako 6*6 zile miguno (screams) za kiswahili ni hazina mzuka.
 
Kiswahili ni very romantic language' lakini unapaswa utumie mifano ya mazingira halisi ya Kiswahili na si kutoa mifano au tafsiri kutoka Kiingereza au lugha zingine. Utamaduni ni mama wa lugha. Lugha ni sehemu na kielelezo cha utamaduni wa jamii husika, hivyo Kiswahili ni sehemu ya utamaduni wa 'Waswahili', yaani watu wa pwani ya Africa Mashariki na maeneo ya jirani. Kiingereza ni sehemu ya utamaduni wa 'Waingereza' na watu wa maeneo jirani nako. Unapotumia mifano ya sentensi au tafsiri ambazo asili yake ni kiingereza utakachokiona ni 'mahaba' ya kiingereza na sio ya kiswahili.

Kinachoonekana hapa ni kwamba mleta mada na wachangiaje wengine kwa kujua au bila kujua ni kwamba hawana maneno, misamiati ya kiswahili yenye kuashiria mahaba. Kukosekana maneno haya kwako haina maana kwamba 'Kiswahili Hakiko Romatic'

Mfano unaposema: 'Bye and take care' kwa kiingereza (kwa tafsiri ya lugha na utamaduni) inaeleweka vizuri sana, lakini ukiitafsiri kwenda kwenye Kiswahili haitafsiriki na haileti maana kwasababu unajaribu kuhamisha kitu kutoka utamaduni wa kizungu utakipelekea utamaduni wa Kiswahili. Maneno kwa mfano 'Mpenzi wangu pole na kazi', kwa mswahili inaeleweka vizuri sana, na kuna mahaba ndani yake, lakini ukiitafsiri kwa kiingereza 'pole na kazi' haileti maana kwasababu ndani yake kuna zaidi ya lugha - ni suala la utamaduni.

Maneno na misemo kama Bon appetit, take care, Shikamoo, pole, ugua pole, yanaakisi utamaduni zaidi kuliko lugha, hivyo chochote ufanyanyo baki kwenye msingi wa lugha moja usichanganye madawa.
 
Kiswahili kinakuwa siyo romantic pale kinapokosewa kutamkwa ipasavyo au kuandikwa ipasavyo mfano neno LAFIKI badala ya RAFIKI.
 
Ahaa sikuelewa ndo tabu ya kunyoa kipara sitanyoa Tena😎

Mbona lugha yetu imekaa kimahaba! Tatizo linapokuja mnataka zile tafsiri za kimahaba ktk lugha nyengine mnataka mzitafsiri kwa kiswahili na zi sounds kimahaba!! Hilo ni kosa!!
Kila lugha kuna namna inavyo tamkwa na inasifa zake kimatamshi..
Pia mnapotafsiri angalieni sana maana na sio maneno mfano kwa kiingeleza mtu akisema "I miss you!" Ukitafsiri kichwa kichwa mtu unaweza sema "nimekukosa"😂 lkn neno zuri hapo na tamu ni "nimekuhamu" au Nina hamu na wewe" mbona inasound good na ipo romantic..

Lugha pia inaeleza tamaduni mfano sisi haswa Afrika hatuna tamaduni za kusheherekea siku za kuzaliwa ni tumerithi tu! Pia mapenzi sio Jambo la kuonyeshana hadharani kama wenzetu na ndio maana unaona tunakosa baadhi ya misamiati ya kimahaba ila natumai ikawepo kwenye kamusi za kiswahili.. lugha huongea tamaduni za watu husika.
Tusitafsiri tu neno bali maana surprise mtu unasema mshangao wkt alietamka anamaanisha zawadi!!
Kiswahili ni kitamu sana haswa ukikutana kwenye nyanja ya mashairi ya kimahaba..
Hata wkt wa tendo lenyewe kuna baadhi ya maneno mtoto wa kike akiisema dah! Unajihisi dunia yote ni yako hapo hata kama ulikuwa huna hamu itakuja tu😂.. mkuu kuna vitu havisemeleki hata havielezeki mtoto unakuta anakuambia "mpenzi weka yote" "taratibu",unaniumiza anatoa na tumguno fulani tutamutamu hlf unaniambia lugha yetu haipo romantic kwa kufuata misingi ya lugha nyengine hapo sikuelewi😜
Nimekuham..!! Haaha
 
Back
Top Bottom